|
Pichani ni washiriki wa semina ya Ujasiriamali iliyoandaliwa na Zebra Promotion kwa wakazi wa Kata ya Kimandolu jijini Arusha ambapo kampuni hiyo inaendesha mafunzo hayo kwa kata zote 25 za jiji la Arusha yenye lengo la kuitikia kauli ya mh Rais Magufuli ya Tanzania ya Viwanda ambapo wajasirianali hao walipata mafunzo ya vitendo na uelewa wa biashara ya kuchakata mazao.picha zote na mahmoud ahmad arusha |
|
Washiriki wakifuatilia masomo kwa ukaribu hapa wakipata somo la kitalu nyumba(GREEN HOUSE)ambapo eneo dogo unaweza kuzalisha mazao mengi na kupata faida kubwa sana ambapo washiriki hao zaidi ya 150 walipata elimu hiyo na kuzawadiwa vyeti. |
|
Afisa Tarafa wa Arusha mjini Felician Karugendo akimpatia cheti mmoja wa washiriki wa semina hiyo ambaye pia alikuwa ni mgeni rasmi wa Semina hiyo kwenye siku ya ufungaji. |
|
Mgeni Rasmi katika Semina hiyo Afisa Tarafa wa Arusha Mjini Felician Kangero alikemea fedha zinazotolewa na Halmashauri ya Jiji la Arusha kutolewa kwa misingi ya itikadi za vyama na kuwataka watendaji kuepuka hilo kwani atakula nao sahani moja. |
Mama huyu mkazi wa Kata ya Kimandolu ambaye ni mjasiriamali ameitaka serikali kuondoa urasimu kwenye mikopo inayotolewa na halmashauri ya jiji la Arusha kwa kinamama na vijana kwa kuitowa kwa wakazi wa jiji hilo bila kuwagawa kwa itikadi za kisiasa
Mshiriki akiwa na matumaini ya kwenda kuanzisha mradi wa ufugaji wa Sungura aliopata mafunzo yake katika semina hiyo jijini Arusha
|
Mratibu wa semina hiyo Zuberi Mwinyi kulia kwa mgeni Rasmi felician Kangero wakiwa kwenye meza kuu wakati wa utoaji vyeti ambapo alisema kuwa kauli mbiu yao kwenye mafunzo yao ni TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA |
mjasiriamali akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujasiriamali baada ya mafunzo ya siku mbili yaliondaliwa Taasisi ya Zebra Promotions
|
Wajasiriamali hao waimetaka serikali kuisaidia kwa ukaribu Kampuni hiyo ili iweze kutoa elimu kwa wakazi wa jiji la Arusha na baadae Tanzania kwa ujumla itakayowasaidia kuzalisha bidhaa zenye ubora na ushindani wa ndani na nje ya nchi mafunzo hayo yalidhaminiwa na kampuni ya Kase Bookshop ya jijini Arusha |
|
baadhi ya wajasiamali wamewataka wenzao kujitokeza ilikuweza kujikwamua kiuchumi na kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo zitashindana kwenye soko la kimataifa na humu nchiniNa Mahmoud
Ahmad Arusha
Waitaka serikali ya Rais dkta John Magufuli kuangalia kwa ukaribu suala zima la mikopo ya wakinamama na vijana hususani inayotolewa na halmashauri za wilaya,miji,manispaa,na majiji hapa nchini kuacha kugawa fedha kwa itikadi za vyama na badala yake kuangalia jamii nzima bila ubaguzi.
Akizungumza baada ya kutoa vyeti kwenye semina ya kuwafunda wajasiriamali iliyoandaliwa na taasisi ya Zebra promotions yenye maskani ya jijini hapa Afisa Tarafa wa jiji la Arusha Felician Rutahengerwa alisema kuwa atayashughulikia malalamiko hayo na mtendaji atakayebainika ataenda na maji.
Alisema kuwa madai hayo yaliotolewa na wajasiriamali si yakufumbiwa macho hata kidogo na anayachukulia kwa umakini mkubwa katika kuhakikisha fedha zinazotengwa na halmashauri zinawafikia walengwa bila kubagua raingi,dini wala itikadi za vyama kwani ni za watanzania wote.
“Juzi nimesikia malalamiko ya baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha wakilalamikia kuhusu fedha zinazotolewa kwa vijana na kinamama kwenye halmashauri yetu zikidaiwa kugaiwa kwa itikadi za kisiasa hili sintalifumbia macha hata kidogo”alisema Rutahengerwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Zebra Promotions Zuberi Mwinyi alisema Teyari kampuni yao imeshaanza kutoa semina kwa wajasiriamali kwenye kata ya Olasiti nah ii ni ya pili kweny kata hii ya Kimandolu.
Alisema kuwa kauli mbiu ya semina hiyo Tanzania ya viwanda inawezekana yenye lengo la kuwapa mafunzo wajasiriamali wakati na wadogo ni kuibua fursa za kuweza kujikwamua kutoka hatua moja kwenda nyingine na kuunga mkono kauli mbiu ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dkta John Magufuli ya Tanzania ya viwanda.
“Semina hizi tunaziendesha hapa jijini Arusha kwenye kata zote 25 na baadae tutaenda wilaya nyingine za mkoa huu na Tanzania kwa ujumla kuweza kuwapa ufahamu wajasiriamali kuweza kutumia fursa mbali mbali za kiuchumi lengo tufikie uchumi wa kati”alisema Mwinyi
Nae mkurugenzi wa Kase Bookshop ambao walikuwa wadhamini wa semina hiyo alisema wao kama wajasiriamali wameona ni fursa kwao kweza kudhamini semina kama hizo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za mh.Rais wetu wa Tanzania Dkta John Magufuli.
Alisema wameidhamini kampuni hiyo licha wajasiriamali hao kutokuwa na uwezo wa kulipia mafunzo hayo ambapo kampuni ya zebra promotions inakabiliwa na changamoto za vifaa kama projector na vipaaza sauti hivyo nawaomba makampuni mengine kuwasaidia ilikuweza kuinua hali za watanzania na taifa kwa ujumla wake kiuchumi.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni