Kikosi kipya cha wanajeshi kutoka Afrika kitaweza kukabiliana na wale wanaowatishia raia 
Maelfu ya raia walilazimika kutafuta hifadhi katika ofisi za Umoja wa Mataifa wakati wa mapigano ya mwezi Julai 
CHANZO BBC
………………………………………………………………………………………
Baraza
 la usalama la Umoja wa Mataifa limesema linajiandaa kuiwekea Sudan 
kusini vikwazo vya silaha , ikiwa itajaribu kuzuia kupelekwa kwa 
wanajeshi wa ziada wa kulinda amani nchini humo.
Hata hivyo Bw Kiir amesema 
hataruhusu Umoja wa Mataifa kuchukua udhibiti wa nchi yake na 
hatashirikiana tena na umoja huo. Kikosi hiki cha Umoja kitakachoundwa 
na askari wa Afrika kitakuwa na majukumu makubwa zaidi ya askari zaidi 
ya 12,000 wa Umoja wa Mataifa ambao wako tayari katika taifa hilo.
Mapigano baina ya vikosi hasimu ya mwezi Julai yaliwauwa mamia ya watu na wengine maelfu kadhaa kuyakimbia makwao.
Vikosi vya Umoja wa Mataifa 
vinakabiliwa na kazi ngumu ya kuwalinda raia ambapo zaidi ya watu 35,000
 walikimbilia kwenye makao makuu yake mjini Juba.
Tofauti na kikosi cha kulinda 
amani kilichopo nchini humo kikosi cha Afrika kitakachokua chini ya 
Umoja wa Mataifa kitaweza kukabiliana na wale watakaowatishia raia
Hata hivyo haijawa wazi ikiwa kikosi hich
ilichopo nchini humo, kikosi cha Afrika kitakachokua chini ya Umoja wa Mataifa kitaweza kukabiliana na wale watakaowatishia raia
Hata hivyo haijawa wazi ikiwa kikosi hicho kitaweza kufanya kazi bila ushirikiano na Sudan kusini.
Zaidi ya raia 100,000 wa Sudan 
kusini kwa sasa wamekimbilia katika nchi jirani kufuatia mapigano ya 
hivi karibuni, linasema shirika la la wakimbizi la Umoja wa Mataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni