Naibu
 waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mh. Dk. 
Hamisi  Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha 
COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY- (CHESA) kilichopo 
Upanga, Wilayani  Ilala, jijini Dar es salaam.
Ziara
 hiyo ya kushtukiza inafuatia baada ya hatua ya Naibu Waziri huyo wa 
Afya  Dk.Kigwangalla  kuendelea kufanya ukaguzi wa Asasi mbalimbali 
zisizo za kiserikali zikiwemo NGO’s na CBO zenye makosa ya kiutendaji na
 kimfumo  ambayo ni tofauti na taarifa zao katika usajili wa Serikalini 
na namna ya uendeshaji wa  wao.
Mbali
 na hayo kituo hicho cha CHESA kinashukiwa kuhusika na vitendo vya 
uhamasishaji wa mahusiano ya mapenzi ya Jinsia moja (USHOGA), ambayo ni 
kinyume na mila na Desturi za kitanzania pamoja na Katiba na sharia za 
Nchi.
“Mahusiano
 ya jinsia moja si kinyume na mila na desturi zetu tu. Bali hata sheria 
na katiba ya nchi yetu haziruhusu mfumo huo wa kimahusiano”  amesema  
Dk..Kigwangalla
Aliendelea
 kubainisha kuwa : “Sisi kama Serikali hatujawahi kusaini mikataba 
yoyote ya kimataifa inayoruhusu  ushoga hivyo kwa taasisi yoyote hapa 
Nchini inayofanya hivyo ni kuvunja sheria za Nchi na inapaswa 
kuchukuliwa hatua kali za kisheria na hata kufutiwa usajili wake” 
aliongeza Dk. Kigwangalla.
Katika
 ukaguzi wa kituo hicho, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla  akiwa 
ameambatana na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara
 anayoiongoza, Bw. Julius Mbilinyi pamoja na Mkuu wa Upelelezi  Mkoa wa 
Ilala, Hassan Selengu  pia wamefanya ukaguzi katika kituo hicho ili 
kubaini kama kuna uwepo wa vilainishi vinavyotumiwa na watu wenye 
mahusiano ya jinsia moja ambavyo hivi karibuni Serikali ilipiga marufuku
 matumizi yake hapa nchini.
“Serikali
 ilikifuta kituo cha ‘SISI KWA SISI’ kwa sababu kilihusika na tuhuma za 
ushawishi wa mahusiano ya jinsia moja ambacho pia wewe ulikuwa 
Mkurugenzi wake. Sasa tumeamua kuchunguza na kituo hichi ili tujue kama 
mnahusika na vitendo hivyo ili tuchukue hatua endapo itabainika ama la” 
ameeleza Dk. Kigwangalla.
Aidha,
 Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amemtaka Mkuu wa upepelezi  Bwana 
Hassan Selengu afanye uchunguzi wa kina katika kituo hicho ili kubaini 
pesa za misaada katika kituo hicho zinatokea wapi lakini pia ni kubaini 
kama kituo hicho kinajihusisha na ushawishi wa watu kujiunga na 
mahusiano ya jinsia moja.
“Tunawasiwasi
 kuwa mnapokea pesa nyingi  na misaada mingi kutoka katika Taasisi 
mbalimbali lakini pesa hizo zinatumika kuhamasisha mapenzi na mahusiano 
ya jinsia moja.
Mbali
 na hayo.  taarifa za usajili wa kituo hichi zinakinzana na malengo na 
miradi inayofanyika hapa.  Pia ipo miradi mbalimbali ambayo 
haijasajiliwa wala hujaitaja katika maelezo yako  lakini inafanyika 
katika kituo hichi” alihoji  Dk. Kigwangalla huku akimtajia baadhi ya 
miradi hiyo ambayo Serikali inaitambua.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).
Tazama hapa MO TV, kuona tukio hilo:
 Upekuzi ukiendelea..
Naibu
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. 
Hamisi Kigwangalla akionyesha moja ya kijarida kwa Mkuu wa upepelezi wa 
Mkoa wa Ilala, Bwana Hassan Selengu na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za 
kiserikali kutoka Wizara hiyo, Bw. Julius Mbilinyi juu ya kukifanyia 
uchunguzi wa kina kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND 
ADVOCACY-(CHESA)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni