Viongozi wa UVCCM mkoa wa Arusha wakiwa wanatembelea shule ya Sekondari ya NaNja ilioungua na moto July 2 mwaka huu
mwenyekiti wa
UVCCM mkoa wa Arusha Sabaya Lengai wa pili kushoto akiwa anaangalia bweni la shule ya Nanja lililoungua na moto
Mwenyekiti wa UVCCM Arusha akiwa na
wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Nanja ilioungua na moto hivi karibuni
wakati alipoenda kutembelea shule hiyo na kutoa mifuko 100 ya simenti
kwa ajili ya ujenzi wa bweni la shule hiyo lililoungua na moto
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Umoja
wa vijana Wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Arusha wamehaidi mifuko 100 ya
simenti kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Nanja iliopo
wilayani Monduli mkoani Arusha iliyounguliwa bweni na moto mapema july
2 mwaka huu
Akiongea
na wanafunzi wa shule hiyo mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Sabaya
Lengai alisema kuwa wao kama vijana wa ccm mkoani hapa wameguswa sana na
tukio hilo ndio maana wakaamua kujikusanya na kwenda kutembelea shule
hiyo pamoja na kuwapa mifuko 100 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa bweni
ambalo limeungua.
Alisema
kuwa wao kama vijana wanamoyo na wananguvu hivyo wako tayari kuwasaidia
wadogo zao ambao wapo mashuleni na ndio maana wameamua kutoa mifuko
hiyo.
"unajua
atuna ela nyingi lakini tumeamua kuwapa msaada hawa wadogo zetu ili
wasome kwa raha na wasiwe na mawazo kabisa kuhusia na tatizolililo
wakuta na ndio maana wameamua kuwapa msaada huo"alisema Sabaya
Alisema
kuwa mchawi hatoki mbali ivyo ni wajibu wa kila mwanafunzi kufanya
uchunguzi na iwapo ata jua nani alisababisha bweni hilo likaungua watoe
taarifa katika ngazi usika.
Aliwatoa
hofu wanafunzi hao kwa kuwasihi wasiwe na wasiwasi wa kuishi shuleni
hapo kwani serekali ya chama cha mapinduzi chini ya Rais wake John
Magufuli ipo makini katika swala zima la ulinzi na imeimarisha ulinzi
shuleni hapo hivyo wasome wakiwa na amani kabisa wakijua kuwa kunawatu
wanawalainda.
Kwa
upande wake katibu wa UVCCM wilaya ya Arusha Ezekiel Molel aliwasihi
wanafunzi hao kuzingatia masomo kwani amna urithi wowote wanaoweza
kupewa na walimu wao zaidi ya elimu
Aliongeza
kuha haya yanayotokea ni matatizo ya kawaida ivyo wasiyaweke akilini
bali waangalie swala la kusoma na fate sana elimu maana bila elimu amna
kitu chochote ambacho wanawezakukipata katika miaka hii .
"serekali
ya sasa hivi aina mambo ya kona kona hivyo wadogo zangu naomba niwasihi
msome sana mzingatie elimu maana bila elimu hamna kitu chochote
kinachoweza kufanyika kwanielimu ni kila kitu kwa kipindi hata
mnavyotuona sisi hapa sisi wenyewe tumesoma na tunakazi na ndio maana
leo hii tumeweza kuja kuwapa pole na kuchangia hiyo mifuko 100 tungekuwa
atuna elimu hata kuja hapa au kufanya hizi kazi tusingeweza "alisema
Molell
Aliwaambia
kuwa ata vitabu vya dini vimeaandika waishikilie sana elimu na
wasiiacha iende zake hivyo ni wajibu wao kuweka akili zao katika swala
zima la elimu na sio kungine ,aliongeza kuwa sasa ivi kuna gonjwa hatari
la ukimwi hivyo ni wajibu wao wanafunzi ambao ni taifa la kesho
kuhakikisha wanaepuka vishawishi mbalimbali ambavyo vinaweza jitokeza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni