MSIMU MPYA WA KANDANDA NDANI YA DSTV KUTIMUA VUMBI WIKI IJAYO.


IMG_0388
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa msimu mpya wa kandanda kwa wateja wa DStv jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
IMG_0397
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na huduma za DStv. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi.
IMG_0422
Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu, akielezea huduma za kuunganishwa kwa wateja wapya wa DStv, ambapo ving'amuzi pamoja na dishi vinapatikana kwa gharama nafuu kabisa ya Sh.99,000/- kwa mawakala wote wa DStv nchini.
IMG_0443
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi ya begi kwa mwandishi wa habari, Joseph Michael baada ya kuchezesha droo kwa waandishi waliohudhuria mkutano huo. Wanaoshuhudia kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia ni Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
IMG_0454
Furaha Samalu na Barbara Kambogi wakikabidhi zawadi ya begi Super Sport kwa mpiga picha wa ITV, Abdallah Kaniki aliyeibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa na Multichoice Tanzania wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kulia Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
IMG_0458
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi akikabidhi zawadi ya T-shirts kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Imani Makongoro.
IMG_0419
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Andrew Chale, modewjiblog
Msimu mpya wa Soka 2015/16, unatarajia kuanza rasmi Jumapili ijayo kwa kushuhudia ligi mbalimbali Duniani zikichezwa na kurushwa moja kwa moja kupitia SuperSport ambayo imejipanga kukuletea burudani kabambe kwa mashabiki wa soka barani Afrika.
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania , Ronald Baraka Shelukindo mapema jana akizungumza na vyombo vya habari amebainisha kuwa, Wateja wa DStv wakae tayari msimu huu kwenye Ulimwengu wa Mabingwa ambapo timu mbalimbali zimejiimalisha katika kuakikisha zinatwaa ubingwa.
“Ligi ya mwaka zitakuwa za kasi na kuvutia kwa kila timu. Barcelona wanajiandaa kutawala dunia kwa mara nyingine, huku Manchester United wanahitaji kurudisha kiti chao cha Ubingwa Uingereza. Jose Mourinho analenga kuhakikisha Chelsea inabaki juu, wakati huo huo , Hispania inajiandaa kuhakikisha wanashinda kwa mara ya tatu kombe la Euro 2016.” Ameeleza Baraka Shelukindo.
Ameogeza kuwa, Watazamaji wa SuperSport watakuwa na nafasi ya kipekee kushuhudia mechi kwenye ubora wa HD, ikiwa ni pamoja na michuano ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) , Ligi ya Hispania (La Liga) , Ligi ya Mabingwa wa Ulaya(UEFA) na Ligi ndogo ya Ulaya ( Europa) ,mechi za FIFA za kirafiki za kimataifa na Klabu Bingwa ya Dunia , Kombe la Ujerumani , Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey) , Kombe la FA na zaidi.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi anaeleza kuwa, Katika msimu huu , Ulimwengu wa Mabingwa itakuwa ikionyesha mechi zaidi ya 900 za kimataifa. Wateja wa DStv Compact Plus wataweza kufurahia baadhi ya mechi zaidi ya 450 ‘live’, huku Wateja wa DStv Premium watazawadiwa mechi zote ‘Live’ zitakazorushwa katika chaneli zote za SuperSport .
“Kuanzia msimu huu na kuendelea, vituko vyote vya Ligi Kuu ya Uingereza vitakuwa vikiletwa kwenu kupitia SuperSport 5 ( SS5 ) inayopatikana kwenye kifurushi cha Premium. SS5 sasa itakuwa ni nyumba ya soka la Afrika kwa ligi kuu ya Uingereza huku ikijumuisha mechi 3 ‘Live’ kila Jumamosi na Jumapili. Kuambatana na mechi kutakuwa na vipindi maalum vya soka kama PLTV Kick Off, Match Day Live, Fan Zone, Saturday/Sunday Review, Football Today, Classic Matches, Netbusters na Mech za Wiki” Amebainisha Barbara Kambogi.
Moto wa La Liga utawashwa ndani ya SuperSport 3 ( SS3 ). Chaneli hii itakuwa inakuletea mechi hadi tatu za ligi ya Hispania ‘ Live’ kwa siku ya Jumamosi na Jumapili . Wateja wa DStv Premium na Compact Plus watapata nafasi ya kuangalia mechi za michuano ya Kombe la mashindano Uingereza ndani ya SS3 sambamba na mechi za Jumamosi mchana za Ligi kuu ya Uingereza , mbadala wa mechi inayorushwa ndani ya SS5, pamoja na Ratiba zote za Jumatatu usiku na vipindi vya mahojiano vya studio.
Pamoja na Mechi za ‘Live’ ndani ya SS3 , itakuwa inakuonyesha vipindi muhimu vya shoo za magazeti , yanayojiri ndani ya La Liga, pamoja na vipindi maalum vya ligi za soka . Makombe yote ya mpira wa miguu, Mabingwa wa Ulaya na Ligi ya Europa, Kombe la FA , Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey), Kombe la Ujerumani , Euro 2016 na mechi za kirafiki za kimataifa zitaendelea kutapatikana kwenye SS3 .
Kwa habari zaidi za michezo na ratiba za mechi kwenye SS5 na SS3, tafadhali tembelea www.supersport.com

KIDOTI :VIJANA WA JIJI LA ARUSHA CHANGAMKIENI FURSA ZA KIJASIRIAMALI



 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Jokate Mwegelo  (kidoti) akiwa na mabalozi wake aliwapata ndani ya mkoa wa Arusha tayari kwa kwenda mtaani kutangaza bidhaa zake zake za kidoti zilizoingia jijini Arusha kwa mara ya kwanza 



 warembo wa Kidoti wakiwa wako katika pozi wameshikilia baadhi ya bidhaa za Kidoti 


 mmoja wa mabalozi wa kidoti  aliyejulikana kwa jina la Anolia Agustino akiwa anaongea na waandishi wa habari


 Meneja masoko wa kampuni ya kidoti Peter Kasija akiwa anaongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya triple A hii leo wakati walivyokuja jijini Arusha kutangaza bidhaa za kampuni yao
 mabalozi wa kidoti   wakiwa kazini
 baadhi ya bidhaa zinazosambazwa nakidoti jijini Arusha
 hizi ndizo ndala za kidoti
 mawigi ya kidoti ndio haya




Na Mahmoud Ahmad wa Manyaraleo Blog

Wito umetolewa kwa vijana ndani ya jiji la Arusha kujitokeza katika
kuchangamkia fursa za kijasiriamali zinazojitokeza ili kuweza
kuwaepushia vijana na matendo maovu yanayoweza kuwafanya ndani ya
jamii kukosaa thamani.
Wito huo umetolewa na Joketi Mwigelwa (kidoti) wakati akichagua vijana
wajasiriamali ndani ya jiji la Arusha katika ukumbi wa triple A jijini
hapa ambapo anatarajia kuwapata wajasiriamali vijana ambao
hatawaingiza katika fursa ya wajasiriamali kwa kupitia kampuni yake ya
kidoti.



Alisema  kuwa amevutiwa  kuja kuwekeza ndani ya jiji la Arusha  katika
nyanza za ujasiriamali kwa kuwa anaelewa kuwa vijana wa jiji la Arusha
hususa ni wasichana wana muitikio mkubwa katika swala zima la
ujasiriamali na maendeleo binafsi.



Aidha alibainisha kuwa katika  mchakato huo wanatarajia kupata
wajasiriamali wapatao 13 ambapo tofauti na kujiingizia kipato cha
ujasiriamali pia watakuwa mabalozi wa kutangaza bidhaa zilizo chini ya
kampuni ya kidoti.
“ndugu mwandishi unavyowaona hawa wote hapa ni vijana kutoka mkoa
mzima wa arusha na mikoa ya jirani tunawafanyia usaili na kupata
vijana ambao wanakithi vigezo vya kuingia katika ujasiriamali ,utakao
wapelekea wao kufanya kazi na kampuni ya kidoti pamoja na kujiajiri
binafsi” alisema kidoti



Pamoja na hayo alisema kuwa kampuni hiyo kwa mwaka huu imeamua
makusudi kusogeza huduma za  ikiwemo bidhaa zake katika mikoa ya nje
ya jiji la Dar Es Salaam ili kuwapa furusa watu wa mikoani ambao
walikuwa hawazipati huduma za kidoti.



Kwa upande wa mmoja wa washiriki waliojitokeza katika mchujo huo
Anolia Agustino  alimpomgeza kidoti kwa hatuqa aliofikia ya kuwaajiri
vijana haswa wasiochana kwani   ,jambo hili litawasaidia wanasichana
wengi kupata ajira pamoja na kujiajiri binafsi.



Aidha alisema kuwa  mbali na kupata ajira pia kampuni hii itawasidia
kujifunza ujasiriamali pamoja na kujiajiri binafsi kwani ,bidhaa za
kidoti ni za bei na fuuu na unaweza kuanza kujiajiri kwa kutumia mtaji
mdogo.
Kwa upande wa mshiriki mungine ambaye teari alikuwa amenufaika na
kampuni ya kidoti aliyejitaja kwa jina la Anjela Mushi alisema kuwa
kampuni hii imemsaidia sana kwani alikuwa anakaa nyumbani bila kazi
lakini alivyoona kwenye mtandao wa kijamii aliamua kujitafuta
mawasiliano na kuanza  na mtaji mdogo na kwasasa ivi mtaji wake
umekuwa.



“mimi nilianza kuona bidhaa za kidoti katika mitandao ya kijamii kama
intagramu  nikaamua kutafuta mawasilano kwakeli nilipata na nilikuwa
na mtaji mdogo kwani nilianza na mtaji wa shilingi laki moja na sasa
na shilingi laki nne na biashara yangu nilianza mwezi wa tano na sasa
ni mwezi wa saba  kwa hadi sasa nina mienzi mitatu nashukuru mungu
mtaji wangu umekuwa”alisema Anjela.
Alimalizia kw akumpongeza kidoti na kumsihi aendelee kuwasaidia
wasichana kwani hivi sasa kumekuwa na changamoto ya ajira kwani ajira
imekuwa ni ngumu.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MABALOZI WA KENYA NA MSUMBIJI IKULU DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania, Dkt. Vicente Veloso baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam , leo Julai 31, 2015, wakati Balozi huyo alipofika kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi.  Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania, Dkt. Vicente Veloso, aliyefika Ofisini kwa Makamu wa Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 31, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR
Add captionMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Chirau Ali Mwakwere, aliyefika Ofisini kwa Makamu wa Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 31, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Chirau Ali Mwakwere, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam , leo Julai 31, 2015.  Picha na OMR  

PAISHA YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR

Mgeni rasmi ambae pia ni rais wa Makampuni ya Convivium Africa Investment, Ndg Alfonso ippolito akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa platform mpya ya matangazo iliyozinduliwa hapo jana katika hoteli ya serena.Paisha ni platform ya matangazo ambayo inapatikana kupitia simu za mkononi yaani smartphone na kupitia tovuti ambapo watumiaji wa simu za smartphone wanaweza kuipakua kupitia google play and playstore bure kabisa.
Meneja bidhaa wa Paisha, Godfrey Fataki akizungumzia jinsi paisha inavyofanya kazi na faida zake wakati wa uzinduzi wa platform hiyo uliofanyika jana katika hoteli ya serena
 Mgeni rasmi akifungua pazia kuashiria kuwa Paisha imezinduliwa rasmi 
Mtangazaji wa Redio Clouds Ephraim Kibonde akiwa katika picha ya Pamoja na Balozi wa Paisha wakati wa uzinduzi wa platform mpya ya matangazo iliyozinduliwa jana katika ukumbi wa Marquee Serena Hotel.
 Mdau akiwa pembeni ya mfano wa simu ya Iphone ambayo inaonyesha application ya Paisha.Paisha inapatikana kupitia playstore na google store bure na endapo utakuwa na application hiyo utaweza kufahamu na kupata huduma zote zitolewazo nchini huku wateja takribani Milioni 1 wameshajiunga huku watumiaji wakipata urahisi wa huduma hizo
tukipata selfie
 Black ryhino akipata selfie na mabest zake wakati wa uzinduzi huo
 Ni mwendo wa selfie tu
 Wadau wakifuatilia uzinduzi wa application ya Paisha
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Paisha ni platform ambayo inapatika katika simu za smartphone pamoja na tovuti platform hii ni kwaajili ya watoa huduma na wauzaji wa bidhaa ambao wanapenda kuwafikia wateja wao kirahisi,Paisha inapatikana kupitia google play na playstore huku watumiaji wa paisha wananufaika kufahamu sehemu ambapo wanaweza kupata huduma mbalimbali kama vile maduka na hata huduma nyingine sehemu ambapo watuamiaji hao sio wenyeji au wenyeji lakini hawafahamu baadhi ya bidhaa zinapatikana wapi.
Ukiwa na application ya paisha katika simu inakusaidi kufahamu kuanzia ramani alipo mtoa huduma huyo pamoja na mawasiliano yake mfano umeenda tegeta na umepata pancha na haufahamu sehemu ilipo gereji ukiwa na paisha kwenye simu yako itakusaidia kufahamu ilipo gereji ambapo itakuonyesha jina la gereji iliyopo karibu na wewe hapo huku ikikuonyesha na ramani pamoja na mawasiliano ya gereji hiyo vilevile kwa bidhaa na huduma nyingine.
Ni application ambayo inawalete urahisi watumiaji na watangazaji wa bidhaa hizo kupitia paisha.kufahamu zaidi kuhusu paisha unachotakiwa kufanya ni tembelea tovuti yao yawww.paisha.co.tz na vilevile unaweza kupakua application hiyo kupitia playstore na google play sasa
Kuweza kupata faida zaidi

HAYA SASA MPYA:..CHADEMA KIMENUKA, JANA TU HATA SIKU HAIJAISHA.DR.SLAA, JOHN MNYIKA NA TUNDU LISSU WANENA MAZITO KUHUSU UJIO WA LOWASSA


The fact that Dr. Wilbord Slaa, John Mnyika and Tundu Lissu did not show up on yesterday Lowassa-Ukawa press conference is very crucial… I mean there must be something going on behind the curtains, let’s just wait and see!

KUMEKUCHA: Siasa ni tamuu! Nasikia Dr Wilbroad Slaa amekataa katakata kukubaliana na maamuzi ya kumleta Lowassa Sijui ni kweli Au?!


Anasema bora akae bila Chama kuliko kukaa chama kimoja na Lowassa. Na inaonesha anaungwa Mkono na Lissu, Mnyika na wengine wengi. Utakuwa mchezo wa kupishana huyu anatoka huyo anaingia! Ngoja tusubirie tuone mwisho wake:

MGOMBEA UBUNGE ARUSHA ,MUSTAFA PANJU APANDIKIZA MBEGU YA UPENDO,AMANI