KUTOKANA
na hali ya huduma ya miundombinu ya usafirishaji kuwa duni na ya aghali
imeshindwa kukuza biashara na uchumi katika kiwango kinachotegemewa
katika mataifa mengi ya barani Afrika. Sekta ya huduma ya miundombinu
ambayo ni kichocheo kikubwa katika kukua kwa uchumi imeshindwa kuleta
mageuzi ya kutosha.
Taarifa
hiyo imebainishwa katika Ripoti ya UNCTAD ya Maendeleo ya Kiuchumi
Barani Afrika ya Mwaka 2015 iliyozinduliwa Jijini Geneva na kusoma
katika baadhi ya mataifa ya Afrika. Akifafanua ripoti hiyo nchini
Tanzania, Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Uchumi UN, Laura
Paez alisema huduma za miundombinu ni muhimu katika kufikia malengo ya
maendeleo endelevu yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya
2016-2030 na kujenga jukwaa kwa ajili ya ukuaji mpana barani Afrika.
Alisema
katika ripoti hiyo inayotoa mwangaza wa uchumi wa Afrika imebainisha
huduma za miundombinu kama vile maji na afya zinahusishwa zinahusishwa
na malengo muhimu ya maendeleo endelevu katika kufikia matokeo ya
maendeleo ya kijamii na endelevu. Alisema huduma kama vile umeme,
mawasiliano ya simu na usafiri huchangia katika tija pia huamuwa
ushindani wa makampuni ya Afrika.
“Afrika
inawakilisha asilimia 15 ya idadi ya watu duniani lakini inatoa
asilimia 2.2 tu ya huduma za mauzo ya nje kimataifa, hali hii inaonesha
kutotumika kikamilifu kwa sekta hiyo,” anafafanua Katibu Mkuu wa UNCTAD
Mukhisa Kituyi akizungumzia ripoti hiyo ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani
Afrika ya Mwaka 2015.
Aliongeza
kuwa ripoti ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika ya Mwaka 2015
inasisitiza umuhimu wa mataifa ya Afrika kukabiliana na changamoto za
mapungufu mbalimbali katika udhibiti wa sera, ambayo yamechangia
kukosekana kwa ufanisi wa kuweza kutumia kikamilifu sekta ya huduma
kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Ripoti
hiyo pia inabainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2009-2012 sekta ya
huduma barani Afrika ilikuwa kwa kiwango cha asilimia 4.6 ikilinganishwa
na asilimia 5.4 katika nchi zinazoendelea. Sekta ndogo za kihuduma
zilizokuwa kwa kasi zaidi zilikuwa usafiri, uhifadhi na mawasiliano.
Hata
hivyo sekta ya huduma katika Afrika iliongoza ukuwaji wa pato la taifa
katika chi 30 kati ya nchi 54 katika kipindi cha 2009-2012, huku kati ya
nchi 45 ambapo pato la sehemu ya huduma lilipanda, 30 zilipata tatizo
la kupungua kwa uzalishaji viwandani kuanzia kipindi cha 2001-2004 hadi
kipindi cha 2009-2012.
Aidha
alisema baadhi ya nchi za Afrika zimeendeleza huduma za viwanda vyao
kwa mafanikio na hata zinapeleka huduma zake katika masoko ya Afrika
huku akizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na Mauritius na Nigeria ambapo
zinafanya vizuri sekta ya huduma za kifedha na kibenki. Alisema
kibiashara katika sekta ya usafiri wa anga nchi za Ethiopia, Kenya na
Afrika ya Kusini zinafanya vizuri huku huduma za elimu ni Uganda, huduma
za mawasiliano ya simu Misri na huduma za Bandari ni nchi ya Djibouti
na Kenya.
Baada
ya ufafanuzi huo ripoti imeshauri masuala kadhaa ikiwemo kuwa na kanuni
ya ufanisi wa huduma ya miundombinu. Alisema pamoja na hayo mataifa
mengi yapo chini katika uhuru udhibiti sekta zote na mifano ya viwango
vya kimataifa vya udhibiti wa miundombinu havitumiki barani Afrika
ilhali vyombo vingi vya udhibiti vipo katika hatua za awali za maendeleo
na bajeti ya kawaida na mara nyingi hata hukosa wafanyakazi wenye sifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni