Mbunge
 wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akizungumza katika uchaguzi wa 
kumpata Mbunge pamoja na Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia
 na maendeleo(CHADEMA)jijini Arusha ambapo aliibuka kidedea kwa kura 255
 sawa na asilimia 93.06% (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mbunge
 viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joyce 
John Mukya alipata kura 39 sawa na asilimia 73.6% katika kinyang'anyiro 
hicho hivyo kumfanya kuwa Mbunge wa viti maalum,aliwataka wajumbe wa 
mkutano huo kuvunja makundi ili kuhakikisha chama kinashinda katika 
uchaguzi wa Urais,Ubunge na udiwani 
 Mgombea 
kupitia chama cha Demokrasia na maendelao (CHADEMA)Noel Olevaroya 
akizungumza mara baada ya kutangazwa kushika nafasi ya pili  kwa kupata 
kura 13 sawa na asilimia 4.74% katika kinyang"anyiro hicho ambapo 
aliwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi kumpa Mbunge Lema 
shilingi laki tano kwaajili ya kampeni ya kuhakikisha  chama hicho 
kinapata ushindi wa kishindo
Mgombea
 nafasi ya Ubunge,Nsajigwa Mwakatobe aliyepata kura 6 sawa asilimia 
2.18% akiwashukuru wajumbe wa mkutano pamoja na wanachama wa chama hicho
PIPOOOOZ!Mgombea
 nafasi ya Ubunge viti maalum Grace Macha alipata kura 3 katika 
kinyang'anyiro hicho , akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi 
kushirikiana nao 
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akisaini fomu ya uchaguzi,pembeni ni Mbunge wa Rombo na mwenyekiti wa uchaguzi huo Joseph Selasini
Mbunge wa Rombo na mwenyekiti wa uchaguzi huo Joseph Selasini akitaja washindi katka kinyang'anyiro hicho
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa na mtoto wake aliyemkimbilia mara baada ya baba yake kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo







Hakuna maoni:
Chapisha Maoni