Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikumbatiana na Dkt. John Pombe Magufuli, mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, mchana huu hapa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convition Centre, Mjini Dodoma. Dkt. Magufuli ameibuka kidedea kwa jumla ya kura 2104, wakati wapinzani wake Amina Salum Ally, akiibuka na kura 253 na Dkt. Asha-Rose Migiro, akipata kura 59. Viongozi wakuu wameenda kwenye kikao hivi sasa cha kujua nani atakuwa Mgombea Mwenza wa Urais. hivyo tutaendelea kuwajuza zaidi, endelea kuwa jirani na Libeneke lako pendwa la Globu ya Jamii. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni