RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA NA GAVANA MKUU WA NCHI HIYO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la lililoandaliwa kwa heshima yake huku akipigiwa mizinga 21 alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiutambulisha ujumbe wake kwa Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai, 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili kwenye jumba la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015 na kukutana na kufanya mazungumzo na Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove aliyesimama nyuma yake pamoja na Mama Salma Kikwete na Mke wa Gavana huyo Mama Cosgrove.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa chakula cha mchana kwenye jumba la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove. PICHA NA IKULU

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni