MAFUNZO YA TAKWIMU KWA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAFANYIKA ARUSHA



SAM_3683
Mkurugenzi wa Taasisi ya Takwimu nchini Dr Albina Chuwa akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha katika mafunzo ya siku tano  kuhusu suala la takwimu zinazohusu hali ya mazingira, ikiwemo uharibifu unaotokana na uchafuzi wa maji, hewa chafu na kupotea kwa uoto wa asili ,Mafunzo hayo yameudhuriwa  na viongozi kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(Habari Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog)
SAM_3677
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja
SAM_3680
Mkuu wa kitengo cha takwimu katika Umoja wa Mataifa, Reena Shah amesema idara yake ina mkakati maalum wa kusaidia nchi hizo katika ukusanyaji wa takwimu za mazingira ambazo kwa sasa ni muhimu sana katika kuweka ajenda na mipango ya maendeleo endelevu.
SAM_3689
Mkurugenzi wa Takwimu Nchini Burundi Mohamed Feruz akizungumza na vyombo vya habari kuhusu takwimu katika nchi yake
SAM_3671
Washiriki wakifwatilia mafunzo kwa ukaribu zaidi
SAM_3670
Washiriki wa mafunzo ya Takwimu kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
SAM_3672
Meneja wa idara ya Takwimu Mkoani Arusha Margeret Mutaleba  akizungumza katika mafunzo hayo jijini Arusha
SAM_3669
Prof.Innocent Ngalinda akizungumza katika mafunzo hayo

Mkurugenzi wa Taasisi ya Takwimu nchini Dr Albina Chuwa amesema kuwa suala la takwimu zinazohusu hali ya mazingira, ikiwemo uharibifu unaotokana na uchafuzi wa maji, hewa chafu na kupotea kwa uoto wa asili bado ni ngeni katika nchi zinazoendelea, hususan za bara la Afrika na kwamba kuna umuhimu wa kutoa mafunzo maalum kwa wafanyakazi wa idara za takwimu nchini.

Aliyasema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki jijini Arusha uliohudhuriwa na viongozi wa Takwimu wa nchi hizo

Bi.Chuwa alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia hali ya tabia nchi na mazingira huku akisisitiza kuwa Takwimu za mazingira zinahitaji watu wawe na uwezo mkubwa yaani elimu pamoja na rasilimali fedha na vifaa huku akitoa rai kwa Jumuiya ya Afrika mashariki kuangalia tasnia hiyo kwa kupewa kipaumbele kama sekta zingine

Naye mkuu wa kitengo cha takwimu katika Umoja wa Mataifa, Reena Shah amesema idara yake ina mkakati maalum wa kusaidia nchi hizo katika ukusanyaji wa takwimu za mazingira ambazo kwa sasa ni muhimu sana katika kuweka ajenda na mipango ya maendeleo endelevu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Takwimu nchini Burundi Mohamed Feruz alisema kuwa katika nchi yake bado hawajaweza kuwa na vifaa vya kisasa vya kuweka kumbukumbu

“Hatujapata mafunzo ya namna ya kufanya hizi takwimu kwa ufasaha bado ni changamoto kwetu”alisema Feruz

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni