ANGALIA PICHA ZA EDWARD LOWASSA AKITANGAZA RASMI KUJIUNGA CHADEMA

 
Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na mkewe mama Regina Lowassa  wamejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach  jijini Dar es Salaam.

Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu na aliyepata kuwa kada wa Chama cha Mapinduzi, Edward Lowassa atangaza rasmi kukihama Chama Cha Mapibnduzi (CCM) na kujiunga na Chama Kikuu cha Upinzani cha Chadema . 



Lowassa ametangaza rasmi hii Leo na kueleza namna mchakato mzima wa kumpata mgombea wa CCM ulivyo kuwa. 
Lowassa na mkewe wamekabidhiwa kadi zao za uanchama  mbele ya viongozi wa vyama vya upinzani vya CUF,NLD na NCCR Mageuzi na matangazo hayo yanaoneshwa moja kwa moja na Azam TV pamoja na ITV. 

 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akizungumza na mamia wakati wa kutangaza adhima yake ya kujiunga na Chadema katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
 Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa (mwenye umvi) akiwa na viongozi wa UKAWA katika Hoteli ya Bahari Beach  jijini Dar es Salaam.
 Mh.Edward Lowassa akiwa katika hadhara ya mamia kujibu maswali katika Hoteli ya Bahari Beach  jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimpa kadi ya uanachama Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Regina Lowassa  katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho,Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Mh.Lowassa akiingia kwenye Hoteli Bahari Beach  kwa ajili ya kutangaza adhima yake ya kujiunga na UKAWA. Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa ametangaza kujiunga rasmi na Umoja wa Katiba (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) .

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika Hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam jana jioni hii alipokuwa akitangaza azma yake ya kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA.
Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba  katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni