Kaimu Mganga Mkuu wa
Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed (kushoto), akizungumza na waandishi
wa habari wakati akifungua semina hiyo Dar es Salaam. Kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Maafa na Dharura, Dk.Elias Kwesi.
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo
cha Maafa na Dharura, Dk.Elias Kwesi (kulia), akizungumza katika semina
hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali,
Dk. Mohamed Ally Mohamed kufungua semina hiyo.
Ofisa Mradi wa Usalama
Barabarani wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Marry Kessy (kushoto),
akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa mada kwenye semina
hiyo.
Mkaguzi wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Mossi Ndozero (kulia), akitoa mada kwenye semina hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Safe Speed Foundation, Henry Bantu akizungumza kwenye semina hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Dharura
na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mary Kitambi akitoa
mada kuhusu sekta ya Afya inavyokabiliana na changamoto za utoaji huduma
kwa wagonjwa wanaopata ajali.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
Na Magreth Kinabo
Imeelezwa kwamba ajali za barabarani yanasababisha vifo vya watu milioni 1.24 kila mwaka duniani.
Aidha watu kati ya 20 milioni na 50 milioni huumia kutokana na ajali za barabarani.
Hayo
yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki wa Huduma Bora za
Afya Dk. Mohamed Ali Mohamed kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)ya mwaka 2013
,wakati wa semina ya waandishi wa habari kuhusu usalama barabarani
iliyofanyika jijini Dares Salaam.
Semina
ambayo inaambatana na wiki ya Umoja wa Mataifa ya Usalama Barabarani
ambayo imeanza Julai 9 na kilele chake Julai 15 katika Shule ya Msingi
ya Uhuru Mchanganyiko iliyopo jijii humo, ambapo mwaka huu imelenga
kupunguza ajali za barabarani kwa watoto.
Aliongeza
kwamba asilimia kubwa (90%) ya vifo vya ajali za barabarani yanatokea
katika nchi ambazo zina uchumi wa kati na wa chini.
Hali
ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kwa nchi ambazo ziko chini
ya Jangwa la Sahara ni (24.1 kwa kila vifo 100,000) ukilinganisha na
idadi ya vifo kwa dunia nzima (18 kwa kila vifo 100,000). Hii
inachangiwa kwa kiasi kikubwa na hali mbaya ya barabara zetu.
Alisema
taarifa ya polisi inaonyesha kuwa katika kipindi cha 2008 mpaka 2013
nchini Tanzania kumekuwa na magari yaliyosajiliwa ni 500,000 ongezeko
hili linaenda sambamba na ongezeko la vifo vinavyotokana na ajali
nchini, kutoka vifo 309 mwaka 2008 mpaka vifo 930 mwaka 2012.
Aidha
Dk .Mohamed alisema ripoti ya Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) inaonyesha asilimia 95% ya ajali za barabarani zinasababishwa
na matumizi mabaya ya barabara.
“Sekta
ya Afya ina mchango mkubwa katika kukabiliana na majeruhi wa ajali,
aidha wingi wa ajali na kupelekea majeruhi wengi ni changamoto katika
sekta ya afya. Madhara yanayotokana na hizi ajali hupunguza maendeleo ya
nchi.
“Hivyo ni muhimu sote kwa pamoja tuweke juhudi za dhati kupunguza ajali za barabarani,” alisema.
Kwa
mujibu wa Dk. Mary Kitambi kutoka Wizara hiyo alisema ajali za
barabarani huigharimu Serikali sh. bilioni 3.4 kila mwaka kwa ajili ya
matibabu ya watu waliojeruhiwa.
Mwakilishi
kutoka WHO, ambaye ni Afisa Miradi, Mary Kessi alisema kwa mujibu wa
ripoti ya shirika hilo ya mwaka 2010 watoto 186,300 hufariki kila mwaka
kwa ajali za barabarani.
Aliwataka waandishi wa habari kuripoti kwa kufanya utafiti juu ya vyanzo vya ajli za barabarani badala ya madhara pekee.
Kwa
upande wake Mkaguzi wa Polis Mossi Ndozero aliwataka jamii kujenga
tabia ya kutii sheria bila shuruti ili kuweza kupunguza ajali ya
barabarani na kutoa taarifa za madereva wanaokiuka sheria za barabara
kwa kutumia namba za simu 0800 757575 na 0682 88
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni