Mkurugenzi
wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la
Arusha kwa tiketi ya CCM akiwaonyesha kadi ya CCM inayoonyesha imani ya
mwanachamana kwa wanahabari pamoja
na wadau mbalimbali jijini Arusha, pia alizungumzia kuhusu mchakato wa
ndani ya chama kumpata mgombea wa Ubunge wa jimbo la Arusha kupitia CCM
siku moja baada ya kumalizika kwa mchakato wa kuzunguka katika kata 25
za kuomba kura kwa wananchama wa chama hicho,aliwataka wananchi
kumchagua mwanachama watakaoonyeshwa na Mungu na siyo kwa kushawishiwa
kwa pesa,pia alionyesha furaha yake kwa kuweza kupandikiza mbegu bora
ya Upendo,Amani na Mshikamano kwa wagombea wenzake pamoja na Wanaarusha
kwa ujumla(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mkurugenzi
wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la
Arusha kwa tiketi ya CCM akizungumza na waandishi wa habari pamoja na
wadau mbalimbali jijini Arusha ,ambapo aliwashukuru wagombea
wenzake 12 wanaowania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Arusha kwa
kumaliza mchakato wa kuzunguka katika kata 25 jimbo la Arusha kwa
Amani,Upendo na mshikamano na pia alionyesha furaha yake kwa kupandikiza
mbegu bora ya Upendo,Amani na Mshikamano
Sehemu
ya wadau wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa
Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM
Mkurugenzi
wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la
Arusha kwa tiketi ya CCM akisisitiza wananchi kwa ujumla kuwa na
Upendo,Amani na Mshikamano na kusisitiza kuwa atamuunga mkono mgombea
yeyote atakayepitishwa na chama cha mapinduzi,kulia nia Kassim Mamboleo
katibu wa kamati ya Ushindi
Mwenyekiti
wa kamati ya Ushindi Godfrey Mhando akizungumza ambapo alisema kuwa
kila mtu anahaki ya kumchagua kiongozi anayeona anafaa na siyo
kurubuniwa kwa fedha
Kassim Mamboleo katibu wa kamati ya ushindi
akizungumza na wanahabari pamoja na wadau ambapo alitoa rai kwa
Watanzania kuwa makini katika mchakato huu kuelekea uchaguzi mkuu
Mkurugenzi
wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la
Arusha kwa tiketi ya CCM akisoma imani inayopatikana katika kadi yake
ya CCM ,moja ya imani ni pamoja na Upendo,Amani na Ushirikiano
Mchambuzi
wa kisiasa na Mwanahabari mkongwe hapa Nchini Abrahamu Gwandu
akizungumza katika mkutano huo alisisitiza wananchi kuwa na Umoja,Upendo
na kuchagua kiongozi bora kuelekea uchaguzi mkuu ili kuepusha uvunjifu
wa Amani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni