MKUTANO WA WADAU WA MAWASILIANO (Connect 2 Connect) WAFANYIKA DAR ES SALAAM.

????????????????????????????????????
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura akizungumza wakati wa ufungzi wa Mkutano wa Connect 2 Connect unafanyika katika Hotel ya Ramada jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa Kimataifa unafanyika kwa mara ya tatu hapa nchini ambao unawashirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano, viongozi wa serikalini na taasisi binafsi, mawaziri kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, watoa huduma za mawasiliano na watengenezaji wa vifaa vya mawasiliano.
“Mkutano huu wa tatu kufanyika Tatanzania tuna bahati kwamba tumejenga mkongo, faida ya mkongo kila mtu anaijua, utakuta kuna punguzo la zaidi ya asilimia 90, na watu hawa wamenufaika hata nje ya nchi kama kabla ya mkongo bei ya kupiga simu ilikuwaje na sasa ikoje, bei ya intanet ilikuwaje na sasa ilikuwaje na leo bei ikoje. Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, Malawi, Uganda zamani ukitaka kupata mawasiliano ya nje lazima uende nje kutumia setelaiti lakini kwa sasa unapata kupitia mkongo wetu huna haja ya kwenda nje,”alisma Kazaura.
…………………………………………………………….
Picha zote na Philemon Solomon-Fullshangweblog
????????????????????????????????????Wadau mbalimbali wa masuala ya mawasiliano, viongozi wa serekalini na taasisi binafsi, watoa huduma za mawasiliano na watengenezaji wa vifaa vya mawasiliano wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa tatu uliopewa jina la Connect to connect (C2C) uliofanyika katika hoteli ya kimataifa ya Ramada iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
6Mkuu wa Idara ya Mkongo wa Taifa Bw. Adin Mgendi akipokea tuzo kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Selina M. Lyimo iliyotambua mchango wao mkubwa katika sekta ya mawasiliano wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa tatu uliopewa jina la Connect to connect (C2C) uliofanyika katika hoteli ya kimataifa ya Ramada iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????Mkuu wa Idara ya Mkongo wa Taifa Bw. Adin Mgendi akionyesha tuzo aliyopewa na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Selina M. Lyimo(kulia) iliyotambua mchango wao mkubwa katika sekta ya mawasiliano wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa tatu uliopewa jina la Connect to connect (C2C) uliofanyika katika hoteli ya kimataifa ya Ramada iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) Dr. Ally Yahaya Simba akijadili jambo na Meneja wa Mawasiliano TCRA wakati wa mkutan.
????????????????????????????????????Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Selina M. Lyimo akizungumza na waandishi wa habari.
????????????????????????????????????Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura akizungumza na waandishi wa habari.
11
Makamu wa rais wa Masoko ya teknolojia Huawei akifafanua kuhusu teknolojia ya 5G wakati wa mkutano mkuu wa Conncect to Connect (C2C) uliofanyika katika hoteli ya kimataifa ya Ramada iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam. Kampuni ya Huawei ni wadau wakubwa wa teknolojia hapa nchini ambapo pia walikabidhiwa zawadi na Wizara ya mawasiliano sayansi na teknolojia kutambua mchango wao katika sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini.
12Wadau wa sekta ya teknolojia na mawasiliano wakimsikiliza Makamu wa rais wa Masoko ya teknolojia Huawei(hayupo pichani) wakati wa mkutano mkuu wa Connect to Connect (C2C) uliofanyika katika hoteli ya kimataifa ya Ramada iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam. Kampuni ya Huawei ni wadau wakubwa wa teknolojia hapa nchini ambapo pia walikabidhiwa zawadi na Wizara ya mawasiliano sayansi na teknolojia kutambua mchango wao katika sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni