Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula akiwa na Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula akiwa na Mkuu wa Utawala, Bi Lilian Munanka, ambaye
Balozi amemwelezea kama Afisa Mkuu Mwandamizi, mweledi, mchakapakazi,
anayejituma na mwajibikaji, mwenyeuzoefu mkubwa na nguzo ya
kutegemewa na ambaye amewapokea Mabalozi wengi.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula akiwa na baadhi ya maafisa na wafanyakazi wa
Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa wakiongonzwa na
Balozi Ramadhani Mwinyi.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula, amewaaga watanzania waishio nchini Marekani, kwa
kuwataka kujivunia utanzania wao na kutoionea aibu lugha yao ya taifa,
Kiswahili.
Mwishoni
mwa wiki, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Marekani, uliandaa hafla ya aina yake ya kumpongeza, kumshukuru na
kumuaga Balozi Liberata Mulamula ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Hafla
hiyo iliyowajumuisha watanzania wa kada mbalimbali wakiwamo maafisa na
wafanyakazi wa Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa, wakiongozwa na Balozi Ramadhan Mwinyi,
ilipambazwa kwa nasaha mbalimbali na salamu za kumtakia kheri Balozi
Mulamula katika jukumu lake jipya.
Pamoja
na kusikiliza salamu kutoka kwa wawakilishi wa makundi ya kijamii,
na kupokea zawadi, Katibu Mkuu, Balozi Mulamula naye alipata fursa
ya kuzungumza mawili matatu.
Katika
salamu zake kwa watanzania waliojumuika katika makazi yake. Moja ya
mambo muhimu aliyoyazungumza ni pamoja na kuwaasa watanzania waishio
nchini Marekani, kujivunia utanzania wao, umoja wao na kubwa zaidi
kutoona aibu kuizungumza na kuiendeleza lugha ya taifa Kiswahili.
“Niwaombeni
jambo moja, msione aibu kuzungumza lugha yetu, lugha yenu ya
Kiswahili, miaka kadhaa iliyopita watanzania waughaibuni walikuwa
hawazungumzi Kiswahili , waliogopa kujitambulisha kwa lugha yao,
lakini sasa hali imebadirika sana, unakutana na watanzania kila kona
wanazungumza Kiswahili hili ni jambo la kujivunia sana na ninawaomba
tuendeleze utamaduni huu wa kuzungumza Kiswahili, kuwa ugenini
hakumaainishi uachane na lugha yako” akasisitiza Balozi Mulamula na
kushangiliwa na watanzania.
Katika
kutilia mkazo wa lugha ya Kiswahili, Balozi Mulamula aliwataka
wana DMV kuendelea na darasa la kuwafundisha watoto lugha hiyo ya
Kiswahili na maeneo mengine kuiga mfano huo.
Jambo
jingine ambalo Balozi alililowasisitizia watanzania hao ni kuhusu
upendo, mshikamano, kuheshimiana, kusaidia na kutobaguana kwa misingi ya
dini, kabila, eneo ambalo mtu anatoka au kwa misingi ya itikadi za
kisiasa.
“
Ninaondoka baada ya miaka miwili ya kuwa Balozi wenu, na katika
miaka hii miwili nimejifunza mengi sana kutoka kwenu, mmeshirikiana nami
na Ubalozi katika mambo mengi yakiwamo ya kuchangia maendeleo yenu
wenyewe na maendeleo ya watanzania wenzenu endeleeni na moyo huu”.,
Kaongeza
“nitakuwa nanyi na kama mjuavyo tunakitengo kizima kinachoshughulia
masuala ya diaspora, na kama ningekuwa mwanasiasa basi nyie
wanadiaspora mngekuwa mtaji wangu, jimbo langu”. akabainisha na
kuamsha tena vifijo kutoka kwa wana-diaspora hao.
Katika
hatua nyingine, Katibu Mkuu, Balozi Mulamula amewahimiza watanzania
walioko nje, kumchangamkia hasa kwa wale wenyekutaka kujaza fomu za
maombi ya pasi zao za kusafiria ambazo zimekwisha muda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni