
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amenusurika kifo 
baada ya ndege aina ya helikopita aliyokuwa amepanda kudondoka akiwa 
katika ziara katika jimbo lake lilipo mkoani Arusha.
 Hakuna aliyepoteza 
maisha katika ajali hiyo, na Mbunge Nassari pamoja na Rubani wake wako 
Hospitali ya Seriani mkoani Arusha kwa matibabu baada ya kupata majeraha kwenye ajali hiyo.
Joshua Nassari pamoja na 
abiria wengine wawili na rubani wao wamenusurika kifo baada ya helkopta 
waliyokuwa wakisafiria kuhamasisha uandikishaji Jimboni kuanguka jioni  Taarifa zinaeleza kuwa helkopta hiyo imeanguka katika kijiji cha Leguruki Wilayani Arumeru Mashariki baada ya hali ya hewa kuwa mbaya.
Nassari na majeruhi wengine wamewahishwa hospitali ya Selian Jijini Arusha kwa matibabu ya majeraha kiasi waliyoyapata.
Blog hii inaendelea kufuatilia tukio hili kwa karibu na kukujuza kila kitu.
![]()  | 
![]()  | 
  


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni