AIRTEL YAZINDUA MASHINDANO YA KUSAKA VIPAJI

  Meneja wa Airtel Kanda ya Nyanda za juu kusini, Straton Mushi akitoa taarifa ya uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji maarufu kama Airtel Rising Stars yaliyofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

   Katibu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya(MREFA), Suleiman Haroub akitoa utambulisho katika sherehe za uzinduzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars.

    Makamu Mwenyekiti wa MREFA, Omary Mahinya akizungumza jambo katika uzinduzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars.

    Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini sherehe za uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji Mkoa wa Mbeya(Airtel Rising Stars).

   Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Airtel Mbeya wakiwa kwenye sherehe za uzinduzi wa mashindano ya kusaka vipaji katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

    Afisa Uhusiano wa Airtel Makao makuu, Jane Matinde akiwa meza kuu akifuatilia sherehe za uzinduzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars.

   Timu za mpira wa miguu za wanawake za Mbalizi Queens na Mbaspo academy zikiwa zimejipanga uwanjani kwa ajili ya kufungua dimba la mashindano ya kusaka vipaji.

   Mwenyekiti wa Soka la Vijana kutoka TFF, Ayoub Nyenzi akitoa shukrani kwa niaba ya Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) kwa Kampuni ya Airtel kwa kudhamini mashindano ya kusaka vipaji.

    Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa akitoa hotuba ya uzinduzi wa mashindano ya airtel Rising Stars ambapo alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.

   Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa pamoja na wageni wengine wakikagua timu kabla ya kuanza mtanange wa kusaka vipaji ulioandaliwa na kampuni ya Airtel.

  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa pamoja na wageni wengine wakielekea uwanjani tayari kwa kuzindua mashindano ya Airtel Rising Stars.

   Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya kusaka vipaji ya Airtel Rising Stars.

    Wachezaji wa Timu ya wanawake ya Mbaspo academy wakiwa katika picha ya pamoja.

    Wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Mbalizi Queens wakiwa katika picha ya pamoja.

    Afisa uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mashindano ya kuibua vipaji kwa vijana wa chini ya umri wa miaka 17.



KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Airtel imezindua msimu wa tano wa mashindano ya kusaka vipaji kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 yanayojulikana kana Airtek Rising Stars.
Mashindano hayo yalizinduliwa juzi katika uwanja wa kumbu kumbu ya Sokoine jijini Mbeya kwa mara ya pili mfululizo na kuzikutanisha timu mbili za wanawake katika mechi ya ufunguzi.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa mashindano hayo, Meneja wa Airtel Kanda ya Mbeya, Straton Mushi alisema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji ambavyo huitumika na vilabu vikubwa vya mpira wa miguu pamoja na timu ya Taifa.

Akisema Kampuni ya simu ya Airtel imeamua kudhamini mashindano hayo kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa wateja wake kupitia michezo ambapo vijana wanaoibuliwa hutokea katika jamii ambayo ni wateja wao.

Aliongeza kuwa Changamoto wanayokumbana nayo tangu mashindano hayo yanaanze miaka mitano iliyopita ni klabu kubwa kushindwa kuwatumia wachezaji wanaoibuliwa na kuwaendeleza.

Kwa upande wake Nwenyekiti wa Soka la Vijana wa TFF,Ayoub Nyenzi, aliipomgeza kampuni ya Airtel kwa kudhamini mashindano hayo na kuongeza kuwa jambo hilo lingezirahisishia timu zinazocheza ligi daraja la kwanza na la pili kuepuka kutumia gharama kubwa kusajili wachezaji na badala yake ingewatumia wanaoibuliwa.

Naye mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa mashindano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Abbas Kandoro alisema Airtel inachokifanya ni kuisaidia serikali katika suala la kuendeleza michezo.

Alisema adhma ya serikali mi uleta mapinduzi katika sekta ya michezo hususani katika mpira wa miguu kwa kutumia sayansi ya Soka.

Alisema ni vema vijana wanaoibuliwa wakafikiriwa kwenda kucheza mpira nje ya nchi kuliko kufikiria kuwapeleka katika timu za Simba na Yanga jambo ambalo halitalisaidia taifa kupata vipaji vizuri.

Aliongeza kuwa ii timu ya taifa iweze kupata malengo mazuri na hatimaye kucheza kombe la dunia ni vema kuwekeza katika soka la vijana kwa kuwatafutia nafasi za kucheza nje ya nchi.

Aidha alitoa wito kwa Wachezaji na makocha kujiendeleza kielimu ili waweze kupata mafanikio makubwa na kuendana na mfumo wa uchezaji wa mpira wa kisayansi.

Mwisho. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni