Mbunge
wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia wapiga kura wake kama
ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kutangaza kutogombea tena ubunge wa
jimboni humo wakati wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa
Singida.
Na Modewjiblog team, Singida
MBUNGE wa Singida mjini na
mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amesema hatagombea ubunge
wa jimbo hilo tena baada ya kulitumikia kwa miaka 10 na kuwezesha
maendeleo makubwa katika sekta ya elimu na afya.
Mbunge huyo alisema hayo akihutubia
maelfu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa People's Club (MB)
wakati wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka
2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa jimbo.Katika utekelezaji
huo ametumia shilingi bilioni 5.
Miradi hiyo ni pamoja na kusaidia
kuongeza shule za sekondari kutoka mbili hadi 15, kuwapo kwa vituo vya
afya na kupeleka shule watu wenye mazingira magumu elfu 15.
Alisema ametekeleza majukumu yake ya
kusukuma maendeleo katika jimbo lake la uchaguzi kwa ushirikiano mkubwa
na kufanikisha vipaumbele vya wakati huo ikiwamo elimu na Afya
Alisema kwamba kujiondoa kwake katika
siasa za jimboni kunatokana na majukumu ya biashara zake kuwa makubwa
pamoja na kutaka kuwa karibu na familia yake baada ya miaka 10 ya
kuwatumikia wananchi wa Singida.
"Ukichukulia kuongezeka kwa-mvi kichwani,
ukilinganisha wakati wa awamo ya kwanza, nafikiri ni busara sasa
kutimiza majukumu haya ya familia ambayo niliyabania nafasi yake kwa
kipindi cha miaka 10.
"Pia siyo siri kwamba majukumu ya
biashara zangu yamebadilika katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.
ukuaji wa biashara zangu umeambatana na kuongezeka kwa majukumu, hususan
mahitaji ya muda zaidi.
Mtazamo huu wa kuipa biashara muda zaidi
ni muhimu sana kwa sababu mafanikio yangu kwenye biashara ndiyo
yaliyoni-wezesha kuwatumikia, na yatakayo-niwezesha kuendelea
kuwatumikia wananchi wa Singida kwa vitendo." alisema.
Akizungumzia sekta ya afya alisema
wananchi wa Singida walifanikiwa kukabiliana vilivyo na ugonjwa hatari
wa Malaria kwa kugawa vyandarua zaidi ya vyandarua 6000 kwa mama
wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
"Kwa kusambaza vyandarua hivi,
tulifanyikiwa kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa asilimia
hamsini" alisema akishangiliwa.
Aidha alishirikiana na mamlaka husika
kupambana na ugonjwa sugu wa mtoto wa jicho kwa kupeleka madaktari
bingwa na kufanya kambi kwenye hospital ya mkoa, waliotoa huduma ya
upasuaji wa jicho na kutoa miwani kwa zaidi ya wananchi 1,000.
"Tulifanikiwa kujenga wodi ya macho,
ndani ya hospitali yetu ya mkoa. Tulifanikiwa kuchangia ujenzi, wa
zahanati za Mungumaji, na Manga ambazo zimekamilika! na zahanati ya
kijiji cha Ititi ambao bado ujenzi unaendelea." alisema
Pamoja na ujenzi huo pia alielezea
mafanikio ya kusaidia baiskeli kwa walemavu na kufunga solar panel,
pamoja na majokofu ya kutunzia dawa, kwenye zahanati za Manga na
Unyambwa!
Akifafanua zaidi katika sekta ya elimu
alisema kwamba walijenga vyumba vya madarasa, kuweka matangi ya maji ya
kuvunia maji ya mvua, vyoo, na kusambaza madawati katika shule mbali
mbali za msingi na sekondari jimboni Singida mjini.
Aidha alichangia vitabu zaidi 1000, vya
masomo ya sayansi na sanaa, kwa shule zetu zote, za serikali ndani ya
manispaa, ya Singida na tulifanikiwa, kuwapeleka wanafunzi wa shule ya
msingi Ukombozi kwenye ziara ya kujifunza bungeni.
Akizungumzia sekta ya maji walifanikiwa
kuchimba visima viwili kwenye mtandao wa Suwasa na vingine 45 ndani ya
baadhi ya vitongoji vyetu vya manispaa ya Singida.
Aidha alisema alifanikiwa kusukuma mradi
wa visima 10, unaofadhiliwa na benki ya dunia, akisisitiza kuwa wakati
akiingia mwaka 2005 upatikanaji wa maji safi na salama ulikua asilimia
23 na sasa upatikanaji wa maji umefikia asilimia 81.
Pia alisema amefanikiwa kuisukuma
serikali, kujenga barabara za kiwango, cha changarawe ndani ya manispaa
na kufanya manispaa kuwe na barabara zinazopitika kwa kipindi chote!
Mkazi wa Singida mjini akimwomba Mbunge wake asiache ngazi kwa maana bado wanamuhitaji baada ya kutangaza kutogombea tena.
Akiwashukuru wananchi wa Singida alisema
kwamba: "kuwatumikia ninyi imekuwa ni tunu kubwa sana niliyo-barikiwa
katika kipindi hiki cha miaka 10, na najisikia kuwa nimependelewa kwa
kujifunza mambo mengi yanayohusu Singida na uongozi bora, na hususan
mapungufu yake, ikiwemo mimi mwenyewe."
Alisema dhamira yake kwa wananchi
haitokani na nafasi yangu kama mbunge ama mwanasiasa, akisisitiza kuwa
dhamira yake ya uzaliwa inayotokana na mapenzi aliyonayo kwao na imani
aliyonayo juu ya uwezo wa kuijenga Singida.
"Mapenzi yangu na imani yangu kwenu
hayapimiki, na ninapenda kuwahakikishia leo kuwa, haya yatajitokeza
katika njia nyingine nyingi tu."
Alisema pamoja na kutokugombea katika muhula wa tatu, lengo lake kuu la kutumikia wananchi wa Singida linabaki pale pale.
"Naomba nitoe ahadi kwenu! nitaendelea
kushirikiana, na kada wa CCM, mtakaomchagua, kwenye nafasi hii ya ubunge
katika shughuli zote za maendeleo ya jimbo letu! kwani dhamira yangu,
ya kushirikiana nanyi, kujiletea maendeleo, haikuwa lazima mimi niwe
mbunge, bali ilitokana na mapenzi yangu, kwa Singida na watu wake! "
Mwanamama huyu akiwa haamini macho yake
huku machozi yakimlenga lenga baada ya kusikia Mbunge wake kutogombea
tena ubunge wa jimbo la Singida mjini.
Watoto hawa machozi yakiwalenga na
kuonyesha huzuni baada ya kumsikia mbunge wao akitangaza kuachia ngazi
jimbo la ubunge wa Singida mjini.
Wananchi wa Singida wakisikiliza hotuba ya mbunge wao.
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed
Dewji akisalimiana na mkazi wa kijiji cha Kinyampembe kata ya Meria
ambaye ni mlemavu wa macho na miguu aliyefahamika kwa jina moja tu la
Kangariga wakati wa hafla ya mkutano wa kuwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka ya ubunge wake, ambapo aliitumia
nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena jimbo la Singida mjini jana
katika viwanja vya People's Club.
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akiingia jukwaani na dancers wake kuwapa burudani wananchi wa Singida mjini.
Mwanamuziki wa kimataifa nchini,
Diamond Platnumz akitumbuiza wananchi wa Singida mjini wakati wa mkutano
mkubwa wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka
2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa jimbo hilo.
Pichani juu na chini ni Diamond Platnumz na ma-dancers wake wakishambulia jukwaa.
Umati wa wananchi wa Singida ukiwa uchizika na burudani ya Diamond Platnumz.
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote na
dancers wake wakitia mbwembwe kwenye show ya kukata na shoka katika
viwanja vya People's Club, Singida mjini.
Chibu Dangote akishambulia jukwaa na dancers wake.
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote katika hisia kali kuwapa raha maelfu ya wananchi wa Singida mjini.
Umati wa maelfu ya wananchi wa Singida
mjini uliokusanyika katika viwanja vya People's Club kusikiliza taarifa
ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya ubunge wa Mh. Mohammed
Dewji.
Vijana wakimshangilia Chibu Dangote.
Kijana wa Singida mjini (mwenye vest) akiimba jukwaa moja na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote.
Ngolololo...cha ngololo now, show me how the do ngololo...Chibu Dangote akionyesha madoido yake kwa wananchi wa Singida mjini.
Shangwe za wananchi wa Singida mjini.
Chibu Dangote akiwapa mikono wakazi wa Singida mjini wakati akiwaaga mara baada ya kutumbuiza.
Kijisehemu cha maelfu ya wakazi wa
Singida mjini waliojitokeza katika mkutano uliotishwa na Mbunge wao Mh.
Mohammed Dewji ambaye amewaaga rasmi.
Kwenye moja na mbili alihusika DJ, Rommy Jones (kulia) akishow love na mmoja wa ma-dancers wa Diamond, Moses Iyobo.
Videographer wa MO kutoka Sofia Production, Yusuf Kissoky akichukua matukio muhimu ya kumbukumbu.
Msafara wa Mh. Mohammed Dewji na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote ukiondoka katika viwanja vya People's Club.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni