Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa
Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama
cha mapinduzi CCM akimkabidhi Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz
Bano fomu ya kuwania kinyang'anyiro hicho baada ya kuchukua fomu hiyo
jana na kurejesha huku akisisitiza kuwa endapo atafanikiwa kupitishwa na
chama hicho au laa atashirikiana na wananchi pamoja na wanaCCM katika
kuleta maendeleo katika jimbo hilo ambalo lipo mikononi mwa chama cha
Demokrasia na maendeleo( CHADEMA)Habari Picha na Pamela Mollel wa
jamiiblog)
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa
Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama
cha mapinduzi CCM akionyesha fomu ya kuwania nafasi ya ubunge baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano jana katika ofisi za CCM wilaya
Hapa
Mustafa Panju akiandika jina lake katika fomu yenye majina ya waliokuja
kuchukua fomu kupitia chama hicho kwa Katibu wa CCM wilaya ya Arusha,
Ferooz Bano ,kushoto ni mke wake aliyemsindikiza kuchukua fomu
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano akionyesha kadi ya mgombea ubunge kupitia chama cha CCM Mustafa Panju
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini
Arusha Mustafa Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha
mjini kupitia chama cha mapinduzi CCM akishikana mikono na kamati yake
ya ushindi kulia ni Kassim Mamboleo katibu wa kamati ya ushindi pamoja
na mwenyekiti wa kamati hiyo
Kassim
Mamboleo ambaye ni katibu wa kamati ya ushindi ya mgombea Mustafa Panju
akiteta jambo na Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano
Mustafa Panju akiingia
katika eneo la CCM wilaya huku akinyoosha mkono juu kusalimiana na
wanaCCM baada ya kukamilisha taratibu za kujaza fomu yake ya kuwania
ubunge jimbo la Arusha mjini
Mgombea
ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM Mustafa Panju akiongea na vyombo
vya habari kuhusu nia yake ya kutaka kuliongoza jimbo hilo
Picha ya pamoja na wadau,familia waliomsindikiza kuchukua fomu ya kuwania ubunge jimbo la Arusha mjini
Mustafa Panju akipiga picha na mmoja wa viongozi wa chama hicho kulia ni mke wake
Timu ya Mustafa Panju ikiondoka eneo la CCM wilaya baada ya kumaliza taratibu zote za kujaza fomu na kurudisha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni