MADIWANI wa
baraza la halmashauri ya wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro waliohitimisha muda wao wa kukaa madarakani kwa kipindi cha miaka
mitano Julai 7, mwaka huu wamesema kutokana
na kushirikiano na watendaji wa halmashauri,wilaya imepiga hatua kubwa ya
kimaendeleo ikiwa na kufikia lengo la ujenzi wa maabara .
Diwani
zamani wa Kata ya Kisawasawa , Hasaan Goagoa pamoja na Hassan Kidapa wa Kata ya Chita, kwa
nyakati tofauti walisema ushirikiano
baina ya madiwani bila kujali itikati ya chama , na watendaji wa halmashauri kupitia mkurugenzi mtendaji wake
umewezesha kuibadiri wilaya iwe ya kimaendeleo katika nyanja ya kiuchumi, kielimu na kijamii.
Madiwani wa
baraza hilo walishiriki Kikao maalumu cha baraza kilichofanyika Julai 7, mwaka huu ,
mjini Ifakara , ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa mkoa , Dk Rajab Rutengwe.
Pamoja na
kushiriki kikamilifu kuhamaisha ujenzi wa maabara, walisema wanajifunia kuiacha
halmashauri ikiogoza kuwa na hati safi kwa muhula minne mfululizo hadi kufikia
mwaka wa fedha wa 2013/2014 .
Kwa upande
wake Mweyekiti wa halmashauri hiyo aliyemaliza muda wake ambaye alikuwa Diwani
wa Kata ya Sanje, David Lugazio,alisema kwa ushirikiano
huo uliwezesha kuongeza kasi ya ukusanyaji
wa mapato ya ndani mwaka hadi mwaka.
“ Mapato
haya yamesaidia kuongoza nguvu za wananchi kwa kutoa fedha za saruji na mabati
kwa kila shule za sekondari ya kata kujenga vyumba vitatu vya maabara ya masomo
ya sanyansi na wilaya imekuwa ya kwanza kukamilisha kimkoa” alisema Ligazio.
Awali, Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri hiyo, Azimina Mbilinyi, alisema halmashauri iliendelea
kujenga uwezo wa kukusanya mapato ya ndani ambapo kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015, imekusanya kiasi
cha sh 5,013,479,000 sawa na asilimia 81 ya makisio ya kukusanya kiasi cha sh
5,473,840,000.
Hata
hivyo alisema, kutokana na kuwepo kwa makusanyo mazuri na usimamizi wa
matumizi sahihi ya mapato hayo, halmashauri imeweza kununua vifaa vya
aina mbalimbali vya kuhudumia jamii ikiwemo na mitambo ya ujenzi wa
barabara za halmashauri hiyo.
Baadhi ya Maofisa Tarafa za halmashauri ya wilaya ya Kilombero akisikiliza jambo.
Dereva wa Greda akionesha uwezo wake.
Hassan
Goagoa , aliyekuwa Diwani mkongwe na wamuda mrefu wa Kata ya
Kisawasawa, akibadilishana mawazo na Mkuu wa mkoa, Dk Rajab Rutengwe,
Julai 7, mwaka huu mjini Ifakara.
Viongozi mbalimbali wangalia mitambo mipya ya ujenzi wa barabara.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( mwenyesuti) akibadilishana
mawazo na baadhi ya Madiwani waliomaliza muda wao wa halmashauri ya
wilaya ya Kilombero.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( suti ) akifurahia jambo pamoja
na watendaji wa halmashauri ya Kilombero na madiwani waliomaliza muda
wao.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( wa kwanza kulia) akiangalia
onesho ya mitambo ya ujenzi wa barabara iliyonunuliwa na halmashauri ya
wilaya ya Kilombero.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, akizundua mitambo ya ujenzi wa barabara ya halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( katikati walikaa) akiwa katika
picha ya pamoja na madiwani waliomaliza muda wao sambamba na watendaji
wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni