Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa
Ndege wa kijeshi wa Fairbairn mjini Canberra katika siku ya mwanzo ya
ziara yake Rasmi ya siku nne ya Kiserikali nchini Australia.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembezwa katika jumba
la Makumbusho ya Taifa ya vita - Australian War Memorial - mjini
Canberra zilikohifadhiwa kumbukumbu mbalimbali ambayo zinazoonesha
jinsi Australia ilishiriki kwenye vita mbalimbali katika siku ya mwanzo
ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australi.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua na kutoa heshima katika
kaburi la askari wa Australia wakati alipotembelea jumba la Makumbusho
ya Taifa ya vita - Australian War Memorial - mjini Canberra
zilikohifadhiwa kumbukumbu mbalimbali ambayo zinazoonesha jinsi
Australia ilishiriki kwenye vita mbalimbali katika siku ya mwanzo ya
ziara yake ya Kiserikali nchini Australia.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Watanzania waishio Australia
alipkutana nao na kuongea nao katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya
Kiserikali nchini Australia.
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ambaye aliondoka nchini usiku wa Jumamosi, Julai 25, 2015, amewasili
nchini Australia na kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne kesho,
Jumatatu, Julai 27, 2015.
Rais
Kikwete anafanya ziara hiyo rasmi ya Kiserikali katika Jumuia ya Madola
ya Australia (The Commonwealth of Australia) kwa mwaliko wa Mheshimiwa
Jenerali Sir Peter Cosgrove AK MC (Mstaafu), Gavana Jenerali wa Jumuia
ya Madola ya Australia.
Wakati
wa ziara yake, Rais Kikwete ambaye mara ya mwisho alitembelea Australia
kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Nchi za Jumuia ya Madola
mjini Perth mwaka 2011, atatembelea mji mkuu wa Australia wa Canberra na
miji ya Newcastle na Sydney.
Mara
baada ya kuwasili mjini Canberra kesho, Rais Kikwete atapanda Mti wa
Kumbukumbu katika Bustani ya Taifa ya Miti ya Australia na kutembelea
Makumbusho ya Taifa ya Vita ya nchi hiyo kabla ya kukutana na Watanzania
wanaoishi katika Australia.
Kesho
kutwa, Jumanne, Julai 28, 2015, Rais Kikwete atafanya mazungumzo rasmi
ya Kiserikali na Waziri Mkuu wa Australia, Mheshimiwa Tony Abbot (MB) na
pia kukutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake Gavana Jenerali Sir Peter
Cosgrove ambaye alipata pia kuwa Mkuu wa Majeshi ya Australia.
Aidha, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa GaiBrodtmann (MB), Waziri Kivuli wa Ulinzi wa Australia.
Maeneo
makuu ambako mazungumzo kati ya Rais Kikwete na viongozi hao wa
Australia yanatarajiwa kujikita ni katika eneo la madini na uchimbaji
wake, fursa za elimu ya juu na mafunzo ya ufundi, masuala yanayohusu
Bahari ya Hindi (The Indian Ocean Rim) na usalama wa Bahari hiyo, ugaidi
na masuala ya usalama wa nchi za Afrika Mashariki.
Rais
Kikwete pia atatumia nafasi hiyo kuwashukuru na kuagana na viongozi wa
Australia, nchi ambayo kwa miongoni mitano iliyopita imekuwa na uhusiano
wa karibu na Tanzania katika maeneo ya uchumi, ulinzi, siasa, jamii na
masuala ya usalama.
Jioni
ya siku hiyo, Rais Kikwete atahudhuria dhifa ya kitaifa ambayo
itaandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake, Gavana Jenerali Sir Peter
Cosgrove na baada ya dhifa hiyo, Rais Kikwete na ujumbe wake wataondoka
mjini Canberra kwenda Sydney, mji mkuu wa kibiashara wa Australia.
Jumatano,
Julai 29, 2015, Rais Kikwete atakwenda mjini Newcastle ambako
atatunukiwa Digriii ya Uzamivu ya Heshima ya Sheria (Degree of Doctors
of Laws Honoriscausa – honorary LLD) na Chuo Kikuu cha Newcastle. Rais
atatunukiwa digrii hiyo ya heshima kwa kutambua uongozi wake uliotukuka
na mchango wake katika maendeleo ya Tanzania na Afrika na jitihada zake
za kuleta amani.
Chuo
Kikuu cha Newcastle ni moja ya vyuo ambavyo vimekuwa vinatoa nafasi za
masomo kwa wanafunzi wa Tanzania, chini ya sera ya miaka mingi ya
Australia kusaidia elimu katika Tanzania.
Wanafunzi
26 wa Tanzania tayari wamemaliza masomo katika chuo hicho na kurejea
nyumbani katika maeneo ya madini, elimu ya juu, vyombo vya habari,
masuala ya fedha na masuala ya serikali. Wanafunzi 45 bado wanaendelea
na masomo yao katika chuo hicho.
Rais Kikwete na ujumbe wake wataondoka Australia asubuhi ya Alhamisi, Julai 30, 2015 kurejea nyumbani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni