Hifadhi
ya Manyara iko umbali wa kilometa 125 magharibi mwa mji wa Arusha,
chini ya ukuta wa bonge la ufa, Hifadhi hii in ukubwa wa kilometa za
mraba 330, ambapo kati ya hizo 230 ni Ziwa Manyara.
Hifadhi
hii inayo makazi makubwa ya aina nyingi za ndege na wanyama kutokana na
ukuta wa bonde la ufa, msitu wa asili ya maji ndani ya ardhi, mapori ya
migunga na maeneo ya wazi ya mbuga.
Mnyama
wa kuvutia kuliko wote katika hifadhi ya ziwa manyara ni simba wapandao
miti, ambao mara nyingine huonekana katika matawi ya migingu.
Wanyama
wengine wanaopatikana katika hifadhi ya ziwa manyara ni pamoja na
tembo, chui, swala, viboko na mamilioni ya ndege maji (korongo) , ziwa
linawavutia ndege wengi kuwepo katika hifadhi ya ziwa manyara.
Hifadhi ya Ziwa Manyara inayo idadi kubwa ya Tembo katika kila kilometa moja.
Huduma kwa wageni;
wapendao kwenda Ziwa Manyara unaobwa kupiga simu +255767492623 na email:info@zlinda.8m.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni