Mtia
nia ya ubunge kwa CCM Philemon Mollel akizungumza katika mkutano wa
kujinadi mbele ya wana CCM wa kata ya Sinoni jijini Arusha ili kuomba
ridhaa yakuteuliwa na chama chake kuwania ubunge wa jimbo la Arusha
katika uchaguzi wa mwezi Oktoba Mwaka huu.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mkurugenzi
wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ya ubunge wa jimbo
la Arusha kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake mbele ya wanachama wa
chama hicho katika kata ya Sakina jijini Arusha ili kuomba ridhaa ya
kuteuliwa kuwamgombea wa ubunge jimbo la Arusha kupitia CCM.
Mtia
nia ya ubunge kupitia CCM mwanasheria Victor Njau akimwaga sera zake
mbele ya wana CCM wa kata ya Sinoni jijini Arusha ili kuomba ridhaa
kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu.
Wanachama
na waasisi wa CCM wa kata ya Sakina jijini Arusha wakisikiliza kwa
umakini sera zinazotolewana watia nia ya ubunge wa jimbo la Arusha
walipokua wakijinadi kwao ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chaa chao
kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani
utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kada
wa CCM Mosses Mwizarubi anayeomba ridhaa yakuteuliwa na chama chake
kuwania ubunge wa jimbo la Arusha akisisitiza jambo katika mkutano wa
kujinadi uliofanyika katika kata ya Ngarenaro jijini Arusha.
Mtia
nia ya ubunge wa jimbo la Arusha kupitia CCM Hamis Migire akijieleza
mbele ya wanachama wa CCM wa kata ya Sokon One jijini Arusha ili kuomba
ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti hicho kupitia CCM.
Mmoja
wa wanachama wa CCM wa kata ya Sakija jijini Arusha ambaye hakujulikana
jina lake mara moja akipitia kwa umakini kipeperushi chenye maelezo
binafsi na mikakati ya kazi za ubunge cha mtia nia ya ubunge wa chama
hicho Mustafa Panju wakati wa mkutano wa kujinadi wa watia nia hao
uliofanyika katika kata hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni