SOKO LA FILAMU NA MUZIKI LAPOROMOKA KWA KASI NCHINI

SAM_3481Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Taifa wa umoja wa wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini, yaani ‘Tanzania Audio Visual Works Distributors,’ Baraka Nyanda akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha  juu ya kushuka kwa ubunifu miongoni mwa wasanii nchini ambako kumepelekea uwepo wa sinema na miziki hafifu isiyoweza kusahimili ushindani wa soko la kazi za burudani duniani anayefatia ni katibu wa shirika hilo Frank Martin ,watatu ni James Mollel katibu tawi laArusha pamoja na Gabriel Simbeye mjumbe.
SAM_3485 katibu wa shirika la Tanzania Audio Visual Works Distributors Frank Martin amebainisha kuwa tasnia ya filamu na muziki nchini ilikuwa na mafanikio kuanzia mwaka 2005 ambapo kazi Zaidi ya 300 zilikuwa zinafyatuliwa kila mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Media for Development International ya 2011.

SAM_3493Mwandishi wa habari kutoka Daily News Marc Nkwame akiuliza swali
SAM_3490Ramadhani Mvungi kutoka starTV akifwatlia jambo katika kamera yake
SAM_3495Muonekano ndani ya ukumbi
SAM_3497Jamiiblog ilifanya jitihada za kumtafuta Msanii mkongwe wa filamu hapa Nchini, Simon Mwapangala maarufu kama ‘Rado,’kuzungumzia hali halisi ya kushuka kwa soko la sanaa hapa Nnchini ambapo alisema kuwa hata kampuni za usambazaji  filamu zinachangia kuua tasnia hiyo kwa kuwapa waandaaji malipo finyu
SAM_3499Mmiliki wa Jamiiblog Pamela Mollel akishow love na Msanii mkongwe wa filamu, Simon Mwapangala maarufu kama ‘Rado
Muziki na Filamu zinazorekodiwa nchini zinadaiwa kupoteza umaarufu nchini kiasi cha kusababisha soko lake kuangukia pua, huku waandaaji na wasambazaji wake wengi wakiamua kujitoa na kutafuta shughuli zingine za kufanya.
Mwenyekiti wa Taifa wa umoja wa wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini, yaani ‘Tanzania Audio Visual Works Distributors,’ Baraka Nyanda, pamoja na katibu wa shirika hilo Frank Martin wamelaumu kushuka kwa ubunifu miongoni mwa wasanii nchini ambako kumepelekea uwepo wa sinema na miziki hafifu isiyoweza kusahimili ushindani wa soko la kazi za burudani duniani.
“Tathmini kutoka wasambazaji waliochini ya ‘Tanzania Audio Visual Works Distributors,’ ambao wanafikia 200 kwa sasa, imeonesha kupungua kwa kazi za Sanaa yaani muziki na filamu kwa asilimia Zaidi ya 50 na hii imesababishwa na kukosekana kwa masoko ya kazi hizo nchini,” alisema Katibu wa chama hicho, Frank Martini.
Wakizungumza jijini hapa wakati wa kikao maalum kati ya wasambazaji na wasanii, viongozi hao wamebainisha kuwa tasnia ya filamu na muziki nchini ilikuwa na mafanikio kuanzia mwaka 2005 ambapo kazi Zaidi ya 300 zilikuwa zinafyatuliwa kila mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Media for Development International ya 2011.
“Kipindi hicho tulishihudia filamu mpya takriban 10 zikitolewa kila wiki, lakini hali ni tofauti kwa sasa ambapo tunashuhudia chini ya filamu 10 kwa mwezi mzima huku idadi hiyo kwa mwaka ikiwa ni wastani au chini ya sinema 120 tu hii ni kwa mujibu wa rekodi ya wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini kwa mwaka huu wa 2015,” aliongeza Martini.
“Wasambazaji na waandaaji (producers) wa sinema na muziki wameamua kujitoa kwenye tasnia hii na kutafuta shughuli mbadala za kufanya,” alisema mwenyekiti wa taasisi hiyo Baraka Nyanda.
Wakizungumzia muziki wamesema eneo hili ndilo limeathirika Zaidi kwa sababu watu hawanunui tena nyimbo zilizorekodiwa kwenye santuri za CD ambazo ndizo chanzo kikuu cha mapato kwa wasanii na wasambazaji.
“Wasanii wengi wa muziki wamekuwa wakisambaza kazi zao kupitia mitandao kama You-Tube ambako mashabiki wao huzipakua bure, wengine huthubutu hata kugawa CD za nyimbo zao mpya bure kabisa mitaani alimradi kujenga jina tu huku wasambazaji wakikosa kipato,” walisema wasambazaji hao.
Msanii mkongwe wa filamu, Simon Mwapangala maarufu kama ‘Rado,’ amesema kuwa hata kampuni za usambazaji  filamu zinachangia kuua tasnia hiyo kwa kuwapa waandaaji malipo finyu; “Hawa wananunua master ya sinema moja mpya kwa shilingi milioni 10 tu, ambazo utakuta ndio gharama za ktengenezea filamu sasa hapo unabaki na nini?” aliuliza.
Kwa mujibu wa Rado, maadam wasambazaji wameamua kiwango cha kununua sinema mpya ni milioni 10, basi watengenezaji huamua kulipua kazi zao kwa kuwatumia waigizaji rahisi na maprodyuza kwa kuokoteza alimradi tu kupunguza gharama za uandaaji ili mwisho wa siku wapate faida.
Lakini kwa mwenzake, Hussein Rajab Usichonge, tatizo ni kwamba wasanii chipukizi hawathaminiwi na matokeo yake tasnia inakosa vitu vipya; “Wao wanaangalia ma-super star tu, ingawa wengi wamechoka na wamekosa ubunifu, sisi chipukizi ndio tungeleta mabadiliko lakini tunabaniwa,” alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni