Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matukio Burudani. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matukio Burudani. Onyesha machapisho yote

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AMTEMBELEA MWANARIADHA ANAYEHESHIMIKA DUNIANI MZEE JOHN STEVEN AKHWARI NYUMBANI KWAKE MBULU MKOANI MANYARA






Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akisalimiana na Mzee John Steven Akhwari Mwanariadha anayeheshimika Duniani mara baada kwasili alipomtembelea nyumbani kwake Eneo la Sani mjini Mbulu mkoani Manyara jana, John Steven Akhwari aliiwakilisha nchi katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika Mexco City mwaka 1968

John Steven Akwari aliyekuwa wa mwisho kumaliza mashindano ya marathon mwaka 1968 Mexico City katika mioyo ya mamilioni ya watu anakumbukwa kama shujaa ambapo mwaka 2008 katika mashindano ya Olimpiki ya Beijing nchini China miaka 40 baadaye, Akhwari aliteuliwa kuwa balozi wa heshima wa Olimpiki. Katika mashindano hayo ya mwaka 1968, Akwari akiwa na umri wa miaka 30 akiiwakilisha Tanzania alikuwa mwanariadha wa mwisho (57) kumaliza mashindano kati ya 75 walioanza.

Mshindi wa mashindano hayo Mamo Wolde wa Ethiopia alitumia saa 2:20:26 huku Akhwari akimaliza zaidi ya saa moja baadaye yaani alitumia saa 3:25:27 kukiwa na watazamaji wachache uwanjani na jua lilikwisha kuzama. Awali wakati anaanza mbio hizo, Akwari alianguka na kupata majeraha kwenye goti ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya hewa ya Amerika ya kati kuwa tofauti na nyumbani. Wanariadha wenzake walimpita moja baada ya mwingine na hivyo kukatiza ndoto yake ya kuiletea Tanzania medali ya kwanza kabisa ya Olimpiki, lakini hakukata tamaa bali alinuia kumaliza hayo mashindano.

Akiwa amefungwa bandeji mguuni huku akitokwa na damu, Akhwari alitokeza uwanjani saa moja baada ya mshindi kutangazwa, na kukiwa na watazamaji wachache na waandishi wa habari na giza likianza kuingia, uwanja ulizizima kuona Akhwari anachechemea akiwa na maumivu kuelekea mstari wa kumaliza mbio, wengi waliguswa baada ya kushuhudia tukio hilo. Alipoulizwa na waandishi kwa nini aliendelea na mashindano baada ya kuumia, aliwajibu kwa utulivu jibu rahisi ``Nchi yangu haikunituma maili zaidi ya 5000 kuanza mbio, bali kuzimaliza``
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akisalimiana na MZee John Steven Akhwari wakati alipoongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aliyemtembelea mzee huyo nyumbani kwake eneo la Sani mjini Mbulu.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza jambo na Mzee John Steven Akhwari.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Mee John Steven Akhwari alipokuwa aktoa maelezo kwake kuhusu mbambo mbalimbali aliyowahi kuyafanya katika masuala ya mchezo wa Riadha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakiangalia tuzo mbalimbali ambazo Mzee John Steven Akhwari kulia aliwahi kutumikiwa. 
 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakionyeshwa mwenge wa Olimpiki ambao Mzee John Steven Akhwari kulia kutumikiwa jijini Beijing China baada ya kuukimbiza akiwa Balozi wa Mashindano hayo mwaka 2008. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akionyeshwa moja ya tuzo ambayo Mzee John Steven Akhwari alitunukiwa nchini Uswisi .
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akionyesswa Nisahani ambayo Mzee John Steven Akhwari alitunukiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi 
Hapa wakionyeshwa vyeti mbalimbali ambavyo Mzee John Steven Akhwari aliwahi kutunikiwa kutambua mchango wake katika mchezo wa Riadha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga wakiwa katika picha ya pamoja na Mzee John Steven Akhwari mara baada ya mazungumza yao.

Kilele cha Tigo Fiesta 2017 chahitimishwa kwa burudani ya kukata na shoka jijini Dar Es Salaam


Msanii Madee kushoto akiwa na Janjaroo na TundaMan kwa pamoja kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam usiku wa kuamkia jana.

Ommy Dimpozi akiwa kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia jana

 Ommy Dimpozi akiendelea kuburudisha katika  jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia jana

Alikiba akiwa na kundi lake wakitumbuiza katika jukwaa la Tigo fiesta liliofanya hitimisho lake usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam.

Vanessa Mdee akiwa na dansa wake wakitoa burudani kwa maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika usiku wa jana  viwanja vya leaders.

Fid q akitoa burudani katika jukwaa la Tigo  fiesta jijini Dar es salaam katika kilele chake kilichofanyika katika viwanja vya Leaders.

Mashabiki wa muziki wakifurahia  burudani mbalimbali zilizotolewa katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam.

Fid Q akiendelea kuburudisha katika Jukwaaa la Tigo Fiesta .


Mwanamziki Mkongwa wa BongoFleva Afande sele akiwa  katika jukwaaa la Tigo fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaaam.

Maua Sama akiwa na kundi lake akitumbuiza katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders .

Benpol akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana 


Wasanii Kassim Mganga na Jux wakishirikiana kuimba pamoja kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam juzi.

Richie Mavoko akiwa na kundi lake akitumbuiza katika kilele cha tigo fiesta usiku wa kuamkia jana.

Chege Chigunda akipagawisha maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliojitokeza katika viwanja vya Leaders katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana.

Ubalozi wa Norway nchini Tanzania wachangia Milioni 300 Sauti za Busara 2018

Balozi wa Norway nchini Tanzania kupitia kwa Balozi wake Balozi Bi. Hanne-Marie Kaarstad leo wameweza kutiliana saini mkataba wa udhamini wa donge nono la kiasi cha Dola 128200(USD) ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania Milioni 300, ambazo zitaenda kusaidia Shirika lisilo la Kiserikali la Busara Promotion kwa ajili ya tamasha la Sauti za Busara 2018. Halfa hiyo ya kutiliana saini imefanyika mapema leo Novemba 2,2017 katika Ubalozi wa Taifa hilo la Norway, Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari. 

Awali Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud alishukuru Ubalozi wa Norway nchini Tanzania kwa kutoa udhamini huo ambao utasaidia uhai wa tamasha hilo ambalo limejizolea sifa kwa muda mrefu. “Sauti za Busara imepata msaada, shukrani kwa ubalozi wa Norway nchini Tanzania. Norway inaonyesha mfano mzuri wa kuigwa Duniani kwa kuchangia katika maendeleio ya kudumu na mazingira rafiki. Kama ilivyo katika malengo yake nchini Tanzania. 
Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad akizungumza katika tukio hilo mara baada ya kutiliana saini. Anayemfuatia ni Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na kulia ni Ofisa wa Busara Promotions.

Ubalozi wa Norway tangu mwaka 2009 unatoa mchango mkubwa wa kifedha kwa shirika la Busara Promotions, ili kuliwezesha kutimiza mpango mkakati wake hii ni pamoja na kusaidia shughuli za kiutendaaji wa tamasha kwa kila mwaka na tunafurahia kwani tunaamini utaendelea pia kwa mwakani” alieleza Mkurugenzi huyo Yusuf Mahmoud. Pia akifafanua umuhimu wa tamasha la Sauti za Busara, Mkurugenzi huyo Yusuf Mahmoud alibainisha kuwa, tamasha hilo limekuwa likiunganisha watu wa rika na asili tofauti huku pia likiheshimu uhuru wa kujieleza sambamba na kuleta umoja, Amani na kuimalisha jamii. 

“Tamasha la Sauti za Busara linatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sekta ya muziki kukutana na kujifunza. Linaimarisha utaalamu katika sekta ya Sanaa nchini hivyo yote haya lengo kuu la tamasha ili ni kuhakikisha kutangaza amani, mshikamano na kuheshimu tamaduni tofauti” alimalizia Yusuf Mahmoud. 


Kwa upand wake, Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad ameahidi kuendeleza ushirikiano na Busara Promotions katika kusaidia Sanaa na Utamaduni ambapo lengo kuu ni kukuza mashirikiano na maingiliano ya kitamaduni kupitia sanaa hasa muziki katika jamii kwa njia ya tamasha hilo la kila mwaka la Sauti za Busara. “Najisikia furaha sana katika siku ya leo katiliana saini udhamini huu mnono. 

Tumekuwa na Busara Promotion kwa muda mrefu kuanzia 2008 mpaka sasa tukiendelea kukuwa zaidi na kuleta mageuzi kwa jamii hasa kuleta mageuzi makunwa sana kwa jamii ya Wazanzibar, Tanzania Bara na Ukanda wa Afrika kwa ujumla. Tunaamini Sauti za Busara wamejijengea mizizi imara Visiwani Zanzibar na Tanzania Bara kwa ujumla kupitia tamasha lao ambalo linainua na kulinda utamaduni wa Mzanzibar huku pia likilinda hutu na utamaduni wake ndani ya visiwa hivyo vya Zanzibar.” Alieleza Balozi Bi. Anne-Marie Kaarstad. 


Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakitiliana saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017. Wengine wanaoshuhudia ni maafisa kutoka Ubalozi wa Norway na Busara Promotions.


Balozi huyo aliongeza kuwa, tamasha hilo pia limekuwa na nguvu kubwa ikiwemo kukusanya watu wengi zaidi kutoka pande mbalimbali za Dunia na kukutana mahala pamoja kufurahia. Aidha, Mkurugenzi wa Busara Promotions, Yusuf Mahmoud amebainisha kuwa, msimu wa Sauti za Busara kwa 2018, tayari wametangaza listi ya wasanii na vikundi ambapo jumla ya vikundi 20 kutoka Tanzania Bara, pia vipo kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, DRC, Nigeria, Morocco, Algeria, Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi, Misri Sudan, Gambia. 

Pia vipo vikundi kutoka nchi za Reunion, Norway, Denmark na Switzerland. Katika vikundi hivyo vinatarajia kuwa na Wasanii 400, ambapo wataonyesha uwezo wao kwenye majukwaa matatu tofauti, shoo 46 zote zikiwa asilimia 100 ‘live’ kwa siku nne mfululizo. Pia kutakuwa na mambo mbalimbali ikiwemo warsha na semina kwa wanamuziki wa ndani na nje ambao watapata kubadirishana ujuzi na mbinu za kukuza sanaa na masoko ya muziki wao. 

Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakibadilishana hati walizotiliana saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017. (PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE).

CECAFA SASA YARUDISHA MICHUANO YA CHALENJI, KUANZA NOVEMBA 25-9DEC


Baada ya kupita miaka miwili bila kuchezwa kwa mashindano ya kuwania Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki, michuano hiyo imerejea tena msimu huu na Tanzania imethibitisha kushiriki.


Nchi wanachama Tanzania Bara, Zanzibar, Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Eritrea na Ethiopia.

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amethibitisha kikosi cha kwanza cha ‘Taifa Stars’ kushiriki na matarajio ya kufanya vema michuano hiyo itakayofanyika kuanzia Novemba 25, 2017 hadi Desemba 9, mwaka huu.

Kidao amesema kwamba uteuzi wa timu za kwanza kwa kila nchi mwanachama wa Baraza la Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki ni makubaliano ya viongozi wa CECAFA waliokutana kwa pamoja huko Sudan, Septemba, mwaka huu.

Kutokana na makubaliano hayo ya kuita timu za kwanza, michuano hiyo itaathiri kidogot ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa kuwa wachezaji wengi wanaounda kikosi hicho, wanatoka timu za VPL.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura amesema: “Tutakaa kama kamati na kuangalia siku ya Jumatano na Alhamisi baada ya michuano hiyo na kupanga ratiba ya mechi ambazo zitapanguliwa wakati wa michuano ya Chalenji.”

Mbali ya michuano hiyo, Tanzania imethibitisha kushiriki michuano ya Chalenji ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 itakayofanyika Bujumbura nchini Burundi kuanzia Desemba 12, 2017 hadi Desemba 22, mwaka huu.

Kadhalika, Tanzania imethibitisha kushiriki michuano ya Chalenji kwa wanawake ikienda kutetea taji katika michuano itakayofanyika Rwanda mwezi Desemba, mwaka huu. Tarehe rasmi itatajwa baadaye.

CECAFA imeamua kurejesha hadhi yake kwani mara baada ya michuano ya Chalenji ya vijana huko Burundi, mwakani itakuwa ni zamu ya Tanzania ambako michuano hiyo inatarajiwa kuanza Agosti 11, 2018 hadi Agosti 25, mwakani.

Wakati huo huo Kidao amethibitisha Tanzania kuwa wenyeji wa mashindano ya Vijana ya Chalenji ya CECAFA/CAF kwa vijana chini ya miaka 17 mwakani na mashindano hayo yatatumika kama sehemu ya kufanya maandalizi Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (AFCON – U17).

Michuano ya mwakani ina baraka za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa sababu shirikisho hilo linataka kutumia michuano hiyo ya vijana ya Kanda mbalimbali za Afrika kupata timu saba katika michuano AFCON – U17 ya mwaka 2019.


Kanda hizo ni CECAFA (Afrika Mashariki), COSAFA (Nchi za Kusini mwa Afrika), WAFU – UFOA (Afrika Magharibi); UNAF (Afrika Kaskazini) na UNIFFAC (Afrika ya Kati).

MAJABA ALIVYOPOKELEWA KWENYE NYUMBA YAKE BUNJU B JIJINI DAR

 Nyumba iliyopo Bunju B ilivyokuwa kabla ya makabidhiano jana. Mkurugenzi wa Mkuu wa Global Group, Eric Shigongo (wa kwanza kulia) na George Majaba (wa pili kulia) pamoja na Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho wakijadiliana jambo. ... Shigongo akizungumza machache mbela ya nyumba hiyo kabla ya kumkabidhi George Majaba jana. Mara baada ya kukata utepe, Shigongo akifungua nyumba hiyo. Ndani ya nyumba kushoto, George Majaba, Afisa Masoko, Jimmy Haroub, Mkurugenzi Mtendaji, Eric Shigongo, mke wa Majaba, Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho na Mhariri Mwandamizi, Elvan Stambuli wakifurahia mandari ya nyumba. George Majaba akiwa na majirani zake wapya wa Bunju B kwenye nyumba yake mpya, hapo walikuwa wakimkaribisha. Majaba akizungushwa kuoneshwa mandari ya nje ya nyumba yake mpya.

Msafara wa magari ukiongozwa na pikipiki zaidi ya tano ulitokea makao makuu ya Global Group Sinza Mori Dar, huku Mshindi wa Shindano la Nyumba Awamu ya Pili, George Majaba akiwa kwenye gari la wazi aina ya BMW huku mke wake akiwa kwenye gari lingine na watoto wao . 

Msafara ulipita Barabara ya Shekilango, ukaingia Barabara ya Ali Hassani Mwinyi kisha ukaingia New Bagamoyo, njiani kwa kuwa kulikuwa na gari la matangazo, watu walikuwa wamejipanga kumshuhudi Majaba aliyejawa na tabasamu akipita akiwa kwenye gari hilo la wazi. 

 Msafara ulipofika Tegeta umati ulikuwa mkubwa na wengi waliokuwa wakimuona Majaba walikuwa hawaamini macho yao kwani yeye mshindi alikuwa akiwapungua mkono na msafara ukawa unaenda kwa mwendo wa polepole, hali iliyofanya baadhi ya wananchi kumkaribia mshindi na walisikika wakisema ‘Hongera, Hongera!” Lakini abiria waliokuwa kwenye mabasi ya daladala nao walionekana wakitoa vichwa vyao madirishani na kumpongeza Majaba ambaye mara zote alikuwa na tabasamu usoni. 

 Hali ilikua hivyo hivyo msafara ulipofika Boko na baada ya kufika Bunju msafara ulisimama kabla ya kuingia Barabara ya Mabwepande ambapo kwa mwendo mfupi tu msafara uliingia kwenye nyumba mpya ya Majaba. Mara baada ya kufika, Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho alitambulisha kwa wageni na wenyeji waliofika kushuhudia makabidhiano hayo na kisha akampa nafasi Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo kusema machache. “Kifupi leo tunamkabidhi nyumba yake Bwana Majaba. 

Ni jambo linalofurahisha kuona yupo hapa na familia yake ya mke na watoto watatu, hivyo bila kupoteza muda karibuni tufungue nyumba,” alisema Shigongo. Baada ya kusema maneno hayo Shigongo, Majaba na mkewe walishika utepe na Shigongo akaukata kuashirika kuwa sasa wamekabidhiwa nyumba yao. 

 Baadaye Majaba na watu wengine wakiongozwa na Shigongo waliingia ndani na kuoneshwa kila chumba, baadaye nje na uani ambako kulikuwa na nafasi kubwa na Shigongo alimuambia mke wa Majaba kwamba eneo hilo anaweza kufanyia miradi kama ya kufuga. Wenyeji walimkaribisha Majaba na baadaye wakapiga picha ya pamoja huku wakimpongesha kwa kushinda nyumba hiyo. Shughuli hiyo iliisha saa moja kasoro robo jioni. 

HABARI NA ELVAN STAMBULI, PICHA MUSSA MATEJA.

KATIBU WA ARUSHA PRESS CLUB(APC) AMIR MONGI AFUNGA NDOA NA BI MUNIRAH BAWAZIRI


Katibu wa Arusha Press Club Amir Mongi akiwa na mkewe siku ya ndoa yao katika ukumbi wa Mamba Complex Marangu Mkoani Kilimanjaro.Picha na Vero Ignatus Blog.

Bi Munira mke halali wa Amir Mongi akiwa na mumewe Amir Mongi siku ya sherehe ya ndoa yao jumamosi katika ukumbi wa Mamba Complex Marangu mkoani Kilimanjaro.Picha na Vero Ignatus Blog

 Amir Mongi akimvisha pete mewe Munirah Bawaziri siku ya ndoa yao ,katika sherehe iliyofayika kwenye ukumbi wa Mamba Complex Marangu Kilimanjaro januari 2017,Picha na Vero Ignatus Blog.
Katibu wa Arusha Press Club Amir Mongi akivishwa pete na mkewe Munirah Bawaziri katika sherehe ya ndoa yao ,iliyofanyika katika ukumbi nwa Mamba Complex  Marangu Mkoani Kilimanjaro.

Amiri Mongi akimkumbatia mkewe Munirah Bawazir .Picha na Vero Ignatus Blog
Maharusi wakiwa wanapata chakula pamoja na waandishi wa habari kuroka Jiji la Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.
Sherehe inaendelea.Picha na Vero Ignatus Blog
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka Jijini Arusha wakiwa wamesimama na mmoja wao aliyevaa gauni la njano Pamella Mollel akiwa anazungumza kwa niaba yao.Picha na Vero Ignatus Blog.


 Wakilisakata rumba katika sherehe hiyo pamoja na maharusi .Picha na Vero Ignatus Blog


MC Kiko akiwa anateta jambo na mmoja wa wazee wa upande wa bwana harusi katika sherehe hiyo,ambapo naye alikuwa msema chochote siku hiyo.Picha na Vero Ignatus Blog.

Pongezi mbalimbali zikiendelea kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki.picha na vero Ignatus Blog.