Balozi
wa Norway nchini Tanzania kupitia kwa Balozi wake Balozi Bi.
Hanne-Marie Kaarstad leo wameweza kutiliana saini mkataba wa udhamini wa
donge nono la kiasi cha Dola 128200(USD) ambazo ni sawa na shilingi za
Kitanzania Milioni 300, ambazo zitaenda kusaidia Shirika lisilo la
Kiserikali la Busara Promotion kwa ajili ya tamasha la Sauti za Busara
2018. Halfa hiyo ya kutiliana saini imefanyika mapema leo Novemba 2,2017
katika Ubalozi wa Taifa hilo la Norway, Jijini Dar es Salaam na
kushuhudiwa na wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari.
Awali
Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud alishukuru Ubalozi wa
Norway nchini Tanzania kwa kutoa udhamini huo ambao utasaidia uhai wa
tamasha hilo ambalo limejizolea sifa kwa muda mrefu. “Sauti za Busara
imepata msaada, shukrani kwa ubalozi wa Norway nchini Tanzania. Norway
inaonyesha mfano mzuri wa kuigwa Duniani kwa kuchangia katika maendeleio
ya kudumu na mazingira rafiki. Kama ilivyo katika malengo yake nchini
Tanzania.
Balozi
wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad akizungumza katika
tukio hilo mara baada ya kutiliana saini. Anayemfuatia ni Mkurugenzi wa
Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na kulia ni Ofisa wa Busara Promotions.
Ubalozi
wa Norway tangu mwaka 2009 unatoa mchango mkubwa wa kifedha kwa shirika
la Busara Promotions, ili kuliwezesha kutimiza mpango mkakati wake hii
ni pamoja na kusaidia shughuli za kiutendaaji wa tamasha kwa kila mwaka
na tunafurahia kwani tunaamini utaendelea pia kwa mwakani” alieleza
Mkurugenzi huyo Yusuf Mahmoud. Pia akifafanua umuhimu wa tamasha la
Sauti za Busara, Mkurugenzi huyo Yusuf Mahmoud alibainisha kuwa, tamasha
hilo limekuwa likiunganisha watu wa rika na asili tofauti huku pia
likiheshimu uhuru wa kujieleza sambamba na kuleta umoja, Amani na
kuimalisha jamii.
“Tamasha
la Sauti za Busara linatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sekta ya
muziki kukutana na kujifunza. Linaimarisha utaalamu katika sekta ya
Sanaa nchini hivyo yote haya lengo kuu la tamasha ili ni kuhakikisha
kutangaza amani, mshikamano na kuheshimu tamaduni tofauti” alimalizia
Yusuf Mahmoud.
Kwa
upand wake, Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad
ameahidi kuendeleza ushirikiano na Busara Promotions katika kusaidia
Sanaa na Utamaduni ambapo lengo kuu ni kukuza mashirikiano na
maingiliano ya kitamaduni kupitia sanaa hasa muziki katika jamii kwa
njia ya tamasha hilo la kila mwaka la Sauti za Busara. “Najisikia furaha
sana katika siku ya leo katiliana saini udhamini huu mnono.
Tumekuwa
na Busara Promotion kwa muda mrefu kuanzia 2008 mpaka sasa tukiendelea
kukuwa zaidi na kuleta mageuzi kwa jamii hasa kuleta mageuzi makunwa
sana kwa jamii ya Wazanzibar, Tanzania Bara na Ukanda wa Afrika kwa
ujumla. Tunaamini Sauti za Busara wamejijengea mizizi imara Visiwani
Zanzibar na Tanzania Bara kwa ujumla kupitia tamasha lao ambalo linainua
na kulinda utamaduni wa Mzanzibar huku pia likilinda hutu na utamaduni
wake ndani ya visiwa hivyo vya Zanzibar.” Alieleza Balozi Bi. Anne-Marie
Kaarstad.
Mkurugenzi
wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini Tanzania
Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakitiliana saini udhamini huo mapema leo
Novemba 2, 2017. Wengine wanaoshuhudia ni maafisa kutoka Ubalozi wa
Norway na Busara Promotions.
Balozi
huyo aliongeza kuwa, tamasha hilo pia limekuwa na nguvu kubwa ikiwemo
kukusanya watu wengi zaidi kutoka pande mbalimbali za Dunia na kukutana
mahala pamoja kufurahia. Aidha, Mkurugenzi wa Busara Promotions, Yusuf
Mahmoud amebainisha kuwa, msimu wa Sauti za Busara kwa 2018, tayari
wametangaza listi ya wasanii na vikundi ambapo jumla ya vikundi 20
kutoka Tanzania Bara, pia vipo kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, DRC,
Nigeria, Morocco, Algeria, Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi, Misri Sudan,
Gambia.
Pia
vipo vikundi kutoka nchi za Reunion, Norway, Denmark na Switzerland.
Katika vikundi hivyo vinatarajia kuwa na Wasanii 400, ambapo wataonyesha
uwezo wao kwenye majukwaa matatu tofauti, shoo 46 zote zikiwa asilimia
100 ‘live’ kwa siku nne mfululizo. Pia kutakuwa na mambo mbalimbali
ikiwemo warsha na semina kwa wanamuziki wa ndani na nje ambao watapata
kubadirishana ujuzi na mbinu za kukuza sanaa na masoko ya muziki wao.
Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway
nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakibadilishana hati
walizotiliana saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017. (PICHA ZOTE
NA ANDREW CHALE).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni