Mkurugenzi wa Mashitaka nchini DPP
 Bw. Biswalo Mganga aliesimama akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa 
mwaka wa fedha 2016/2017 na kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha
 2017/18 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. 
Kabudi wa pili kushoto akingalia nyaraka wakati taasisi zilizo chini ya 
wizara zilipokuwa zikiwasilisha
taarifa ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma
taarifa ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma
Baadhi wa Wabunge wajumbe wa 
Kamati Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza taarifa za 
utekelezaji kutoka kwa watendaji wa serikali mjini Dodoma
…………….
Serikali imetaifisha mali zenye 
thamani ya Shilingi 1,200,000,000 kufuatia kushinda maombi sita (6) ya 
urejeshaji wa mali zilizotokana na uhalifu nchini ambayo yaliendesha 
katika mahakama mbalimbali nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi
 wa Mashitaka nchini (DPP) Bw. Biswalo Mganga alipokuwa akiwasilisha 
taarifa ya utekelezaji wa majukumu kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na 
Sheria mjini Dodoma.
DPP Mganga alisema mali hizo 
zilitaifishwa kutoka katika mashauri mawili yaliyokamilika ni Injini 
aina ya Yamaha, jahazi (ark), pampu mbili (2) za maji, lita 15,885 za 
mafuta ya diesel, magari (5) aina ya Range Rover Sport EVoque na gari 
moja (1) aina ya Audi.
Amesema pamoja na kutaifishwa kwa 
mali hizo maamuzi mbalimbali yalitolewa kuhusiana na maombi hayo ikiwa 
ni pamoja na wahusika kutakiwa kutokufanya miamala yoyote ya kibenki kwa
 mashauri matatu (3) na shauri moja (1) linasubiri kusikilizwa.
Amesema Divisheni ya Mashtaka 
iliendelea kutekeleza jukumu lake la kuendesha mashauri ya jinai kwa 
kusimamia shughuli za utenganishaji wa uendeshaji wa mashtaka na 
upelelezi na uratibu wa kesi kubwa katika Mahakama mbalimbali chini.
Amesema jumla ya mashauri 180 ya 
jinai yalifunguliwa katika Mahakama ya Rufaa, kati ya mashauri hayo 129 
yalihitimishwa na mengine 51 yanaendelea katika hatua mbalimbali na 
kuongeza kuwa kati ya mashauri ya jinai 6,678 yaliyofunguliwa, 4,006 
yalihitimishwa na mengine 2,672 yanaendelea kusikilizwa.
Amesema mashauri yanayohusu 
wanyamapori yaliendeshwa katika mahakama mbalimbali nchini na katika 
kipindi cha Julai hadi Septemba, 2017 kulikuwa na mashauri 386, kati ya 
mashauri hayo 52 yalihitimishwa na watuhumiwa kupewa adhabu mbalimbali 
ikiwemo faini ya shilingi 228,035,080 na mashauri 334 yanaendelea 
kusikilizwa.
Amesema Divisheni ya Mashtaka ina 
mashauri 200 ya dawa ya kulevya ambayo thamani yake inazidi shilingi 
milioni 10 kwa kila shauri lililopo Mahakamani nchini huku mashauri 10 
yalihitimishwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni