Mkuu
 wa Mkoa Paul Makonda akiashiria kuzinduliwa kwa zoezi la ujenzi wa 
Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema 
kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo.
Mkuu
 wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ,amezindua zoezi la ujenzi wa 
Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema 
kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo na 
kuongeza kuwa ujenzi wa Ofisi utafanka kwa haraka, chini ya Vijana wenye
 morali ya kazi kutoka JKT, Magereza na Jeshi la Polisi.
Ramani
 ya ofisi hizo inaonyesha kuwa na Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu Mkuu 
Msaidizi, Ofisi ya Walimu wa kawaida, Mhasibu, Karani, Chumba cha 
kuhifadhi Mitihani, Vyoo vya kisasa, Stoo, Jiko, Chumba cha Mikutano na 
sehemu kuweka Mafaili ambapo ndani ya ofisi zitafungwa AC, Feni, Samani,
 Taa za kisasa na Umeme.
Akizungumza
 Katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na upandaji wa Miti RC Makonda 
amesema kuwa lengo la ujenzi huo ni kuwezesha Walimu kufanyakazi katika 
Mazingira mazuri yatakayowapa morali na hamasa ya kufundisha Wanafunzi.
Sanjali
 na hayo Makonda amewapongeza Walimu wa shule za msingi kwakuwezesha 
Mkoa wa Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya
 mtihani wa Darasa la saba ukilinganisha na nafasi ya nne waliyo pata 
mwaka jana na amewaomba kutoichia nafasi hiyo , pia walimu wa shule za 
sekondari nao wajitahidi ili waongoze katika matokeo ya mtihani kitafa.
"Rais
 ,ameshatuonyesha dira kwa kutoa elimu bure na sisi wasaidizi wake ni 
lazima tuendeleze maono yake, mimi sio kiongozi wa kusubiri kuagizwa 
ndio nifanye kazi kama ilivyo kwa Remote hadi ibonyezwe ndio ifanye 
kazi, mimi ni kiongozi wa kujiongeza, sijachaguliwa kuwa mzigo kwa 
serikali bali kuleta matumaini kwa wananchi"alisema.
Amewataka
 Viongozi kuacha Siasa kwenye mambo ya Msingi yanayolenga kuleta 
maendeleo kwakuwa Maendeleo hayana chama wala ubaguzi wa Dini."walimu 
hawa wanapowafundisha watoto wetu hawawaulizi vyama vyao wala dinizao 
tena watoto wenyewe hawa hawana vyama naombambeni ndugu zangu tuwe 
wamoja katika mambo ya maendeleo ,nashangaa kuna Wilayamoja wao 
hawatamani jambo jema nikupinga tu ,madai yao eti watanipa kiki,mmi 
sitafuti kiki nafanya kazi".
Awali
 mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza wakati wa ukaribisho 
amemshukuru Rc Makonda kwa moyo wake wa kuwajali walimu kwa kuona shida 
yayao na kuahidi kufanya naye kazi begakwabega i kuendelea kutatua kero 
za wali na wananchi kwa ujumla ,Uzinduzi huo umehudhuriwa na Wakuu wa 
Wilaya, Kamanda wa Polisi kanda maalumu Dar es Salaam Lazalo Mambosasa, 
Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu, Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule 
,Diwani, Pamoja na wanachikutoka maeneo mbalimbali ya wilaya Ilala.
Naye
 Diwani wa kataya Majohe Mwenyevyake Waziri amepongeza hatua ya mkuu wa 
koa wa Dar es salaam kwa juhudi anazozifanya katika shuguli za maendeleo
 na kusema kuwa anamuuga mkono aendelee mbele zaidi."kwakweli
 hatamimi ilikuwa ni shauku yangu kuona walimu wakifanya kazi katika 
mazingira mazuri wanakuwa naofisi nzuri na anachokifanya Makonda 
kitukizuri napia kama kiongozi wa serila anatimiza wajibu wake mimi 
nimtakie kilalakheri" Alisema Waziri.
Nao
 baadhi ya wananchi walihudhuria uzinduzi huo wamesema weshukuru hatua 
hiyo na kusema kuwa walimu walikuwa wanadharirika ,walidharaulika 
walikuwa kamawametengwa ukienda ofisi za wizara zingne wanaofisi lakini 
wao walisahaulika sasa watafanya kazi kwa moyo kwakuwa watakuwa huru na 
maboyao .
Kwa
 upande wake Mwenyekti wa kamati ya ujenzi Canal Mbuge amewataka 
watanzani kuendelea kuchagia ujenzi huo ilikujenga mshikamano na utaifa 
kwa kujitolea katika mambo ya maendeleo na kuahidi kuwa wao kama 
wasimamizi wa ujenzi huo watahakikisha ujenzi huo unafanyika kwa ubora 
na viwango na kukamilika kwa wakati.
Mkuu
 wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akilakiwa na baadhi ya viongozi 
wa majeshi pamoja na wakuu wa wilaya za mkoa wa Dar alipokwenda kuzindua
 zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam 
ambapo amesema kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu
 mkoa hapo.
Mkuu
 wa Mkoa Paul Makonda akizungumza na wananchi wa kata ya Majohe wakati 
wa uzinduzi wa zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa 
Dar es Salaam ambapo amesema kukamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua 
kiwango cha elimu mkoa hapo
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akipanda mti.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa kazini kuashiria uzinduzi wa ujenzi za ofisi hizo ukiwa tayari umepamba moto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni