KONDOA CHEMBA KISIWA CHA WATENDAJI WA MAZOEA MAJIBU YAO NTAFUATILIA HADI MIAKA NENDA RUDI

Ahmad Mahmoud
Mwaka huu Namshukuru mungu kunijaalia kuweza kutembelea maeneo ya vijijini ikiwa ni katika kutekeleza majukumu yangu ya utafiti wa habari kwa jamii zilizopo pembezoni na kuchaguwa wilaya za Chemba,Kondoa Mji na Vijijini.

Suala la kutembelea maeneo hayo ni kufanya utafiti wa kihabari ambao utasaidia kuibua kero mbali mbali wanazokutana nazo wananchi na kujua miradi ya maendeleo ambayo serikali imetekeleza sahemu hizo,za pembezoni mwa jamii hususani vijijini.

Kumekuwa na Changamoto kubwa ndani ya wilaya hizo kiasi kunatakiwa juhudi za mara kwa mara kwa waandishi kufika huko, ambapo waandishi wengi ni nadra sana kufika maeneo ya vijijini sio Kondoa pekee na maeneo mengine hapa nchini kusaidia kuibua matatizo na juhudi za serikali kuatatua kero zao,

Hapa nawashukuru sana Muungano wa klabu za Waandishi wa Habari hapa nchini(UTPC)  kwa kuja na mpango wa mafuzo ya wandishi wa habari za vijijini hii naona ni wakati muafaka na msingi wa kuweza kuwasidia wananchi kuziunganisha na mamlaka zao kuweza kuibua kero zao, japo mimi sio mmojawapo niliepata mafunzo hayo ila natekeleza wajibu.

Mwezi wa 3 mwaka huu tarehe 8 nikiwa mkoani Arusha ambapo ni kituo changu cha kazi Napata simu ikiniomba kwenda kondoa kwenye tukio la Kampuni ya madini ya Kondoa Minning na Kikundi cha wachimbaji wadogo wa madini ya Dhahabu(KUMUCHA) kwenye Kijiji cha Changaa.

Nilifika kondoa majiba ya saa 7 mchana kwa basi la kampuni ya Champion na kupokelewa na wenyeji wangu viongozi wa kikundi cha kumucha na mara moja kuelekea maeneo ya Mtaa wa Tumbelo ambapo yapo machimbo wanaogombea na kampuni ya Kondoa Minning T Ltd kwa mda mrefu sasa bila kupatiwa ufumbuzi wa suala hilo ambapo mamlaka hadi sasa zipo kimya kutoa tafsiri ya nani hasa mmiliki wa eneo hilo la migodi iliyopo Changaa.

Leo Sintazungumzia mgogoro huo ambao kwa sasa upo katika hatua za kutolewa majibu ya kina na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kondoa Ndugu yangu Fallesy Kibasa kwanza nampa Hongera kwa utekelezaji wa majukumu pili namwambia sheria ifuate mkondo wake katika kuhakikisha wananchi wanyonge wanapata haki yao bila kujali maslahi mapana ya wenye nacho.

 Bila kusahau Ofisi ya madini kanda ya kati na Afisa Madini Makazi Dodoma nao pia wapo katika mikakati hiyo ya kutatua mgogoro huo, Japo wao ndio chanzo cha mgogoro huo kwa kushindwa kutafsiri sheria ya madini ya mwaka2010 kwa vitendo na kuichukulia maamuzi kwa wakati ambayo ingeondoa sintofahamu iliyopo katika ya wachimbaji na kampuni ya Kondoa Minning.

Suala nalotaka kulizungumzia leo ni suala la kampuni za simu za mikononi ambazo zipo hapa nchini zikiwaunganisha wananchi katika suala zima la mawasiliano ili waweze kujiletea mendeleo yao kupitia mawasiliano ya kibiashara na hata sasa wakati serikali inatekeleza sera ya Uchumi wa kati wa Viwanda nayo ni kiungo muhimu wa kufikia malengo hayo.

Kumekuwepo na sintofahamu kubwa katika suala zima la fedha za huduma ambazo makampuni ya simu yanatakiwa kurudisha kwa wananchi na sheria zinazoyataka makampuni hayo kuingia mkataba na vijiji kwenye maeneo ya vijiji hususani hifadhi za milima.

Na maeneo mengi ya Vijijini viongozi wa serikali wanatakiwa kulifuatilia hilo kwenye maeneo mengi ya vijiji kubaini mihutasari mingi walioingia viongozi wa serikali za vijiji mingi haipo kwa maslahi ya wananchi wa kurudisha fedha za huduma na malipo ya maeneo.

Utakuta maeneo mengi yana migogoro ambayo kama viongozi au mwanasheria wa Halmashauri angeshiriki katika kuandaa mchakato mzima wa miongozo ya kisheria, basi kusingetokea matatizo kama hayo ambayo kuna vijiji Takribani 10 ndani ya wilaya ya Kondoa ambavyo havinufaiki na fedha za huduma wala maeneo yao waliowekewa minara ya simu za mkononi na makampuni hayo.

Sehemu nyingine utakuta hawajalipwa Takribani miaka mitano sasa na haijulikani Fedha zinaingia kwa nani na vijiji vimeibua miradi ya maendeleo ambapo kama fedha hizo zingeingia kwenye vijiji hivyo ingasaidia kukuza miradi hiyo na kujikuta vijiji vinapata maendeleo Tarajiwa ikiwemo miradi ya Afya,elimu na maji.

Hapa ntaizungumzia moja ya Kata na Kijiji ambacho kitakuwa mfano wa vijiji hivyo 10 Thawi ni mojawapo ya vijiji hivyo na inakabiliwa na changamoto kubwa ya huduma muhimu ya kijamii Maj,i hawa wanatumia maji ya Mto Bubu, maarufu ndani ya wilaya hiyo, lakini changamoto kubwa wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko wanatumia maji hayo kuongea kufulia na mifugo humo humo kwa wakati mmoja hii inaonyesha ni kwakiasi gani fedha hizo zingeweza kuwasaidia kuondokana na adha hizo japo kidogo ingeondoa

 Aidha kama sio Afisa wa Kampuni hiyo na viongozi wachache kuingia makubaliano ya kinyemela kwa afisa wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kufika na kuuhadaa uongozi na wananchi kuwa kampuni hiyo inanunua maeneo ya kuweka minara kinyume na sera ya kampuni hiyo kukodisha kwa wananchi aua kijiji husika, hilo ni  ukiukaji wa mkataba na kuuziwa eneo la mlima  AMASASOO uliopo kijiji cha Thawi kata ya Thawi wilayani Kondoa ,

Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani sheria bado nataratibu hazikutumika, na hata viongozi walipohoji waliwaambia ntapeleka eneo lengine hivyo msukumo wa wananchi waliokuwa wanahitaji huduma hiyo ndio uliopelekea maamuzi ya kuumuuzia aliedai ni Afisa kutoka kampuni ya Tigo kwa  makubaliano ya shilingi za kitanzania 500,000 kwa eneo la hifadhi ya mlima huo wa Amasasoo, hapa utaona jinsi misitu inavyouzwa kinyume na sheria.

Narudia ndugu yangu suala hilo lilifuatiliwa na mbunge wa jimbo la Kondoa kaskazini dkta. Ashatu Kijaji ambaye pia ni Naibu waziri wa fedha na Mipango lakini hadi naandika makala haya wananchi hao bado mnara unasumbua huduma walizotarajia hawapati kwa uhakika jambo linalotia simanzi kama kampuni hizo zipo kwa ajili ya kutoa huduma au zipo zipo tu.

Sijaongelea Fedha za Huduma ambazo ni haki yao kisheria kurudishwa kwa ajili ya maendeleo utaona ni kwa jinsi gani utaratibu huo unavyotumika kurisha maendeleo nyuma ndani ya kijiji na hapa utaona na kujua naongelea nini katika suala zima la makubaliano ya makampuni ya simu za mikononi

kwani nina uzoefu wa masuala haya ndani ya ulipaji mfano upo wazi kule Salanka nilifuatilia Fedha walizokuwa wakiidai Kampuni ya Vodacom na Airtel zilikwama kwa mda hadi walipolipwa Stahiki yao baada ya kulifuatilia tena kwa Gharama Hadi Dar es Salaam nikiwa na mwenyekiti wa kijiji hicho wakati huo.

Hata hivyo ilibidi nifike kwa mwanasheria na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Kondoa Vijijini kupata ufafanuzi kuhusiana na mbunge wa jimbo hilo alifikia wapi baada ya kumuachia suala hilo mwanasheria wa halmashauri kulifuatilia juhudi ambazo hadi sasa hazijapatiwa ufumbuzi wowote hadi naandika makala hii

 Japo hapo awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa Vijijini Fallessy Kibassa tulitofautiana kimtazamo baada ya mimi kuandika story kuhusiana na suala hilo na mkurugenzi huyo kuniita muungo mbele ya Katibu mkuu wa Tamisemi Mussa Iyombe juu ya suala hilo wakati nikizungumza nae akiwa morogoro kwa njia ya simu tena simu ya Bosi ofisini kwa katibu mkuu Dodoma

Ilibidi nifike kwa mwanasheria wa Halmashauri ya Kondoa Vijijini Kuulizia suala hilo na kunieleza kuwa suala hilo wameliachia vijiji kuandaa muhtasari upya na makubaliano mapya ilikuweza kuliendea jambo hilo na majibu yatakuwa hivi karibu kwani juhudi zinaendelea kuhakikisha mbunge anapatiwa majibu ya suala hilo na wananchi wanapata fedha za huduma.

“Ndugu mwandishi hapa kuna mkanganyiko wa kisheria ila vijiji vina mamlaka yake kisheria kuamua matumizi ya ardhi hivyo suala hili wao watakuwa na maamuzi ya kutuletea sisi tuweze kufuatilia” aliongeza mwasheria huyo.

Utaona ni jinsi gani huduma za simu za mikononi zilivyokuwa changamoto vijijini hususani ambapo bado wengi wao taratibu kanuni na sheria kwao vimekuwa ni kama jua na kiza hivyo kukuta sheria zinawapitia kando hata wakuongoza nao wanatoa majibu ya kufikirika zaidi kuliko kisheria.

Kwa upande mwingine nataongelea suala la Tigo pesa huku vijijini ni mwiba mchungu kuna watu wamelizwa fedha zao na wahudumu wa kampuni ya tigo hapa namzungumzia Bi Ziada Abdi Ally mwenye no 0711480481 aliehamishiwa Fedha kiasi cha 970 000 tokea mwezi wa nane na mfanyakazi wa idara ya mauzo ya kampuni ya Tig joseph maginga kwenye namba zake Tofauti 0716123207 na 0710040034.

ambapo Kampuni hiyo  imekuwa ikimzungusha bila majibu wala kumlipa fedha zake za huduma imekuwa deni, wanamwambia aende polisi nako wanamzungusha hadi leo upelelezi haujakamilika na mtuhumiwa anadunda mitaani hapa utaona nayo yazungumza ujue ni kiasi gani wananchi vijijini wanavyoumia.

Hiyo ni tigo kama zitafuatiliwa na kampuni nyingine utaona mlolongo wa matukio hayo yalivyo mengi waswahili wanasema ‘panapofoka moshi ujue moto upo karibu” huo ni msemo wa Kiswahili na una maana kwa serikali yetu kutupia macho sio kondoa tu kwa Tanzania nzima kwa kila aliye na dhamana kuhakikisha anawajibika sio mpaka viongozi wa kitaifa kufika maeneo yao.
Unaweza kusema Kondoa na Chemba zipo Kisiwani kwani kumekuwepo na matukio mengi tena ya ubadhirifu wa miradi ya mendeleo na serikali imekuwa kimya licha ya kutakiwa kutolea maelezo kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa huu ucheleweshaji wa majibu na kutofika kwa wakati ndio matatizo yanakuwa makubwa na malengo ya mendeleo yanakuwa hayajafikiwa.

Kama masuala ya kisheria yangefuatwa na miongozo kwa viongozi wa serikali za vijiji ingekuwepo hapa suala zima la migogoro mingi ya Ardhi na masuala ya mbalimbali yahusuyo maendeleo na migogoro isingekuwepo na ingekuwa historia naomba viongozi taasisi za kisheria na serikali kutembelea ndani ya wilaya hizo kuwasaidia wananchi katika masuala ya kisheria na kutoa elimu ya mausala hayo na mengine mbalimbali lengo likiwa ni kuondoa dhana ya migogoro iliyopo ambayo inafukuta chini kwa chini na serikali ndani ya wilaya ikidai imetatua migogoro 8 kati ya kumi na tatu

 Endelea kunifuatilia katika makala inayofuatia kuhusu ziara yangu kwenye wilaya hizo.

Ahmad Mahmoud ni mwandishi wa habari Anapatika kwa No.0745159196
Email.ahmad2mahmoud@gmail.com

Mwisho………………….

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni