NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MARY MWANJELWA ATEMBELEA KIWANDA CHA MBOLEA MINJINGU-MANYARA





Naibu Waziri wa kilimo Mhe
Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines
and Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky) mara baada ya kuzuru katika kiwanda hicho kilichopo katika eneo na Kata ya Minjingu Mkoani Manyara. (Picha Zote Na Mathias Canal)


Naibu
Waziri wa kilimo Mhe
Mary Mwanjelwa (Katikati) akisikiliza kwa makini taarifa kuhusu utekelezwaji wa maagizo ya waziri Mkuu mara baada ya kutembeleaa kiwanda cha Mbolea
cha Minjingu (Minjingu Mines
and Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
 Naibu
Waziri wa kilimo Mhe
Mary Mwanjelwa akisikiliza kwa makini taarifa kuhusu
utekelezwaji wa maagizo ya waziri Mkuu mara baada ya kutembeleaa kiwanda
cha Mbolea
cha Minjingu (Minjingu Mines
and Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
 Muonekano wa vitendea kazi vya kiwanda
cha Mbolea
cha Minjingu (Minjingu Mines
and Fertilizer Ltd).
 Naibu
Waziri wa kilimo Mhe
Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
  Naibu
Waziri wa kilimo Mhe
Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
  Naibu
Waziri wa kilimo Mhe
Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
  Naibu
Waziri wa kilimo Mhe
Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea Minjingu akiongozwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
Muonekano wa baadhi ya vitendea kazi vya Kiwanda cha mbolea cha Minjingu kilichopo eneo na Kata ya Minjingu Mkoani Manyara.
 
Na
Mathias canal, Manyara
Naibu Waziri wa kilimo Mhe
Mary Mwanjelwa ametembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and
Fertilizer Ltd) kilichopo katika eneo na Kata ya Minjingu Mkoani Manyara ambapo
pamoja na mambo mengine amejionea hali ya uzalishaji wa mbolea asilia ya
kupandia aina ya Minjingu.
Mhe Mwanjelwa alitembelea
kiwandani hapo ambapo miongoni mwa matakwa yake ilikuwa ni pamoja na kufatilia
maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa aliyoyatoa
mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu alitembelea eneo la machimbo ya mbolea ya
Minjingu na kupokea taarifa ya uendeshaji wa Kiwanda cha Mbolea cha Minjingu.
Mhe Mwanjelwa alishuhudia
uzalishaji ukiwa umeongezeka kufikia Tani 150,000 kwa mwaka ambapo uongozi wa
kiwanda hicho umetii agizo la Waziri Mkuu la kuwasihi kuboresha teknolojia ili
kuzalisha Tani zaidi ya 150,000 ambazo zitaongeza kiwango cha upatikanaji wa
mbolea hapa nchini kwwani bado upo chini kuliko mahitaji
Katika hatua nyingine
Uongozi wa kiwanda hicho ulitii agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye
aliwagiza kuandika barua kwa Mhe Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pomnbe Magufuli kuomba radhi kwani mifuko waliyokuwa wanatumia kuuzia Mbolea
hiyo ya Minjingu ilikuwa na nembo ya nchi ya Kenya licha ya kuwa inazalishwa
hapa nchini.
Hata hivyo Mhe Mwanjelwa
alijionea mifuko hiyo ikiwa imebadilishwa na kuwa na muonekano wa anuani ya
Tanzania kama uzalishwaji wake ulivyo.
Sambamba na hayo pia Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ameutaka uongozi wa kiwanda hicho cha mbolea
Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) kutoa elimu kwa umma juu ya ubora
na umuhimu wa mbolea hiyo ya kupandia.
Mbolea hiyo inatokana na
miamba inayochimbwa katika eneo la Minjingu Mkoani Manyara ambayo husagwa na
kufungashwa kwenye kiwanda kilichojengwa katika eneo hilo. Mbolea ya Minjingu
imeboreshwa kwa kuongezwa virutubisho vya Nitrogen, Salfa, Magnesi, Zinki na
Boron (N, S, Mg, Zn, na B). 
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd)
Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky) ameiomba serikali kupitia wizara ya kilimo
kuwaruhusu maafisa ugani kote nchini kupatiwa mafunzo maalumu yatakayowaimarisha
ili waweze kuwa sehemu ya kuitangaza mbolea bora ya Minjingu ambayo inazalishwa
nchini.
Alisema kuwa serikali
inapaswa kutazama upya utozaji wa VAT kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali hapa
nchini kwani tozo ya VAT ya asilimia 18 wanayotozwa ni kubwa huku waagizaji wa
mbolea nje ya nchi wao wanaingiza pasipo tozo kama hiyo.
Aidha, alisema kuwa tayari
makala za vipindi vya Redio, Televisheni na Magazeti mbalimbali zimeanza
kuandaliwa kwa ajili ya kuelimisha wakulima juu ya umuhimu wa mbolea hiyo ya
Minjingu ambayo ni bora kuliko mbolea nyingine yoyote nchini na nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Mary Mwanjelwa alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imejidhatiti katika
viwanda hivyo inathamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni