Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati
akifuatilia maelekezo yanayotolewa na mfanyakazi wa NHIF alipotembelea
Taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini Bw. Bernard Konga.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa pili kulia
akiangalia moja ya mafaili ya kuhifadhia kumbukumbu za madai katika
ofisi za NHIF alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam, wa
kwabnza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini Bw.
Bernard Konga.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa pili kulia
akipata maelekezo kuhusu kitengo cha huduma kwa wateja kutoka kwa Mkuu
wa kitengo hicho Bi. Anjela Mziray wa kwanza kushoto juu ya huduma
zitolewazo na kitengo hiko alipotembelea NHIF leo jijini Dar es salaam,
wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini Bw.
Bernard Konga.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile aliyesimama
akiongea na watumishi wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF hawapo pichani
alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto
ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini Bw. Bernard Konga.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima
ya Afya nchini NHIF Bw. Bernard Konga aliyesimama akiongea na watumishi
wa taasisi hiyo hawapo pichani anayefuata aliyekaa ni Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile .
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima
ya Afya nchini NHIF Bw. Bernard Konga aliyesimama akimuonesha Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile baadhi ya tuzo walizopata katika kutoa huduma bora leo jijini
Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia kitabu
kinachohusu huduma za NHIF alichokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
huo Bw. Bernard Konga katikati wakati ziara yake katika taasisi hiyo
leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa
Bima ya Afya nchini NHIF wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
hayupo pichani wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es
salaam.
Picha na WAMJW
……………..
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
MFUKO wa Bima ya Afya NHIF
imetakiwa kufanya bidii katika kuongeza wanachama wa mfuko huo ili
kufanya huduma za matibabu kupatikana kwa urahisi na gharama nafuu kwa
watanzania wote.
Akizungumza na uongozi pamoja na
watumishi wa Taasisi hiyo leo jijini Dar es salaam Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
amesema kuwa kuna umuhimu wa NHIF kuongeza wanachama wa mfuko huo.
“NHIF waweke uwezekano wa
kuanzisha bima ya afya kwa wajawazito kwa bei nafuu hadi kufikia Julai
2018 na pia huduma hii kuwa ya lazima kwa wananchi wote ili kuwasaidia
kuepuka gharama kubwa za matibabu” alisema Dkt. Ndugulile
Aidha Dkt. Ndugulile alisema kuwa
NHIF wanatakiwa kutengeneza mpango wa kuondoa adha kwa wagonjwa wenye
kadi za bima za mfuko huo kunyanyapaliwa kwa kuwa hawana hela ya malipo
papo hapo ili waweze kupata matibabu stahiki kwa wakati.
Kwa mujibu wa Dkt. Ndugulile
amesema kuwa sio lazima wananchama wa mfuko huo wawe watumishi wa umma
bali waangalie hata sekta binafsi ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa
maendeleo ya sekta ya afya nchini.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile
amesema kuwa ili kuweza kufanikiwa kuondoa rufani za nje kunatakiwa
kutengenezwa sheria ya kupandikiza viungo kama vile figo,moyo,vifaa vya
usikivu na vinginevyo ili kuleta mabadiliko katika sekta ya afya hivi
sasa na miaka ijayo kwani wataalamu watazalishwa hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa Bima ya Afya nchini NHIF Bw. Bernard Konga amesema kuwa
wamejidhatiti kuongeza wananchama wa mfuko huo kwa sekta mbalimbali na
katika kutekeleza hilo wameanza mazungumzo na vyama vya ushirika ili
kujua namna ya kuwasaidia wanachama wake.
“Tulishajipanga katika kutekeleza
agizo hilo kwani mpaka hivi sasa tumeanza kuongea na vyama vya ushirika
ikiwamo vyama vya wazalishaji korosho ili kuona uwezekano wa kuwasaidia
katika kupata huduma hiyo” alisema Bw. Konga.
Aidha Bw. Konga amesema kuwa wapo
bega kwa began a Seikali katika kutekeleza sera ya afya kwa kutoa
huduma ya kulipia matibabu kwa kila mtanzania aliyejiunga na mfuko huo
ili kuweza kufikia malengo ya sera hiyo mpaka kufikia 2020.
Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo alitembelea
makao ya Mfuko wa Bima ya Afya NHIF na kuongea na Uongozi,watumishi
pamoja na kutembelea sehemu ya kuhifadhia kumbukumbu za wadai,kituo cha
huduma kwa teja na sehemu ya Tehama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni