Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi ameipongeza Halmashauri ya Mji
wa Geita kwa kusimamia vizuri fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa
vilivyo chini ya mpango wa lipa kwa matokeo shule ya msingi Nguzo
mbili.
Akizungumza
wakati wa ziara yake katika shule hiyo Mheshimiwa Robert Gabriel
alisema kuwa ameridhishwa na kiasi cha fedha kilichotumika katika ujenzi
wa madarasa kwa ubora wa hali ya juu katika shule hiyo. " Inashangaza
sana kuona maeneo mengine wanatumia fedha zote kiasi cha shilingi 20
milioni katika ujenzi wa darasa moja lakini kuna mapungufu mengi hivyo
lazima kuwe na nidhamu ya matumizi ya fedha katika miradi ya
Serikali"Alisema Lughumbi.
Akiwa
shuleni hapo Mkuu wa Mkoa ameagiza wakurugenzi kuunda na kutumia vikundi
vya ujenzi vilivyo katika maeneo ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa
madarasa pia kuishirikisha jamii ili kupunguza gharama kwa serikali na
hatimaye fedha zinazobaki ziwezekufanya mambo mengine katika huduma za
jamii.
Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akiongozana na viongozi mbalimbali
wa Mkoa wa Geita na Wilaya ya Geita wakati wa ukaguzi wa majengo
yaliyotekelezwa kwa mpango wa lipa kwa matokeo Halmashauri ya Mji Geita.
Katika
hatua nyingine Mhandisi Robert Gabriel aliutaka uongozi wa Shule ya
Msingi Nguzo Mbili kusimamia suala la usafi na kumuagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Geita kuhakikisha anasimamia uimarishaji wa
miundombinu hiyo ambayo mingine imeanza kupasuka. Aidha, ameagiza shule
hiyo kupelekewa miundombinu ya maji ili vyoo vilivyojengwa vianze
kutumika badala ya kufungwa.
Pamoja
na kutembelea Shule ya Msingi Nguzo Mbili Mkuu wa Mkoa pia ameitembelea
shule ya Sekondari na kukagua ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa
vilivyojengwa kupitia mpango wa lipa kwa matokeo. Shule ya Msingi Nguzo
mbili imejenga madarasa nane kwa kutumia shilingi milioni 13 kwa kila
darasa, Ofisi 4, kisima cha maji na vyoo vya kisasa pamoja na ukarabati
wa madarasa mengine katika shule hiyo kutokana na fedha iliyobaki katika
bajeti ya darasa moja.
Mkoa
wa Geita una upungufu wa vyumba vya madarasa 8600 hivyo serikali
imeandaa mpango kabambe wa kutokomeza tatizo hili kwa kushirikiana na
jamii na wadau wote wa Mkoa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mhandisi
Robert Lughumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Mkoa na
Wilaya Geita na kamati ya usalama ya Mkoa wakikagua miundombinu ya
shule ya Msingi Nguzombili wakati wa ziara ya Mkuu huyo wa Mkoa
Halmashauri ya Mji Geita.
Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa maelekezo kwa Mkuu wa
Wilaya ya Geita(Wakwanza kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Nguzombili wakati wa ziara yake katika Shule hiyo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji Geita Mhandisi Modest Apolinary akifafanua
jambo kuhusu utekelezaji miradi ya lipa kwa matokeo kwa Mkuu wa Mkoa
wakati wa ziara yake shule ya msingi Nguzombili iliyopo Halmashauri ya
Mji Geita.
Vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia mpango wa lipa kwa matokeo Halmashauri ya Mji Geita. PICHA NA JUMAPILI MAGESA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni