Sekta ya Bima yatakiwa kuajiri wazawa -SERIKALI

ARUSHA.
Kampuni za Bima nchini zimetakiwa kuajiri watanzania badala ya mfumo wanayotumia kwa sasa ambapo makampuni mengi yamekuwa yakiajiri wafanyakazi wao kutoka nje yanakotoka, pia sekta hiyo ya bima imeagizwa kuwekeza mitaji yao katika viwanda kuendana na sera nchi ya uchumi wa kati na viwanda.
 
PHOTO: Naibun waziri wa Fedha Dkt Ashantu Kijaji akiongea wakati wa kufungua semina ya wadau wa sekta ya Bina inayofanyika jijini Arusha.
PHOTO: Baadhi ya wadau wa sekta ya Bina kutoka nchini za Afrika wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) alipokuwa akiongea.

PHOTO: Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro akimwakilisha
mkuu wa mkoa wa Arusha Gambo ambaye hakuwepo.

PHOTO: Kamishina wa Bima Saqware akiongwa wakati wa hotuba ya
ufunguzi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi mapema leo.

HABARI KWA UNDANI.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Fedha Dkt Ashatu Kijaji alipokuwa akifungua Semina ya siku mbili ya wadau wa Bima kutoka nchi 20 barani Afrika (African Insurance Organization) semina inayofanyika jijini Arusha ambapo amewaagiza wadau wa sekta hiyo kote afrika kuangalia ni njia gani zitumike kusaidia serikali za Afrika kuweza kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi.
"Sera ya serikali ya inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuri ni nchi kufikia uchumi wa kati, hii haitaweza kufanikiwa iwapo kila mmoja wetu hataweza kufanyakazi ikiwemo kupunguza tatizo la ajira hapa nchini nanyi ni wadau wakubwa na mna nafasi kubwa ya kuongeza wigo wa kupunguza tatizo hilo" aliongeza Dkt Kijaji.
Ameongeza kuwa maeneo mengi ya kiuchumi yanahitaji mitaji ikiwemo Afya kwenye jamii, Kilimo na ufugaji, hivyo sekta ya bima inaweza kuwa ni  muhimili mkubwa kufikia maendeleo, kwani imekuwa ikiwagusa wananchi wengi, “mna wajibu wa kuongeza wigo na wanachama wenu kuweza kupata mitaji ya uwekezaji”
Kwa upande mwngine Kamishna wa Bima hapa nchini Dkt.Baghayo Saqware amesema kuwa watanzania wengi bado hawajajiunga na bima ya maisha kwa kutokujua faida zake ikiwemo ya kujikinga na majanga, uwekezaji na kuondoa familia zao kwenye hofu pindi wanapopatwa na maafa mbali mbali kwenye maisha yao ya kila siku.
Amesema kuwa lengo lao kubwa ni kuweza kuifikia jamii kubwa na kuwa wadau wakubwa wa uwekezaji hapa nchini kama zilivyo taasisi nyingine za mifuko ya hifadhi za jamii na kuwaondoa hofu wale wasiojua faida za Bima waweza kuchukua hatua sasa za kujiunga iliwawe wanachama.

"Wananchi wengi bado hawana ufahamu na kujua faida za kujiunga na bima ila tunafanya kazi ya utoaji wa elimu kuweza kuwafikia wananchi wengi hususani Wafanyabiashara wadogo, Wafugaji, Wakulima na wananchi wa vipato vya chini hii itasaidia kuongeza mitaji itakayowasaidia uwekezaji mkubwa hapa nchini katika kufikia uchumi wa kati" alisema Dkt.Saqware

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni