Nyumba iliyopo Bunju B ilivyokuwa kabla ya makabidhiano jana. Mkurugenzi
wa Mkuu wa Global Group, Eric Shigongo (wa kwanza kulia) na George
Majaba (wa pili kulia) pamoja na Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho
wakijadiliana jambo. ... Shigongo akizungumza machache mbela ya nyumba hiyo kabla ya kumkabidhi George Majaba jana. Mara baada ya kukata utepe, Shigongo akifungua nyumba hiyo. Ndani
ya nyumba kushoto, George Majaba, Afisa Masoko, Jimmy Haroub,
Mkurugenzi Mtendaji, Eric Shigongo, mke wa Majaba, Meneja Mkuu, Abdallah
Mrisho na Mhariri Mwandamizi, Elvan Stambuli wakifurahia mandari ya
nyumba. George Majaba akiwa na majirani zake wapya wa Bunju B kwenye nyumba yake mpya, hapo walikuwa wakimkaribisha. Majaba akizungushwa kuoneshwa mandari ya nje ya nyumba yake mpya.
Msafara
wa magari ukiongozwa na pikipiki zaidi ya tano ulitokea makao makuu ya
Global Group Sinza Mori Dar, huku Mshindi wa Shindano la Nyumba Awamu ya
Pili, George Majaba akiwa kwenye gari la wazi aina ya BMW huku mke wake
akiwa kwenye gari lingine na watoto wao .
Msafara
ulipita Barabara ya Shekilango, ukaingia Barabara ya Ali Hassani Mwinyi
kisha ukaingia New Bagamoyo, njiani kwa kuwa kulikuwa na gari la
matangazo, watu walikuwa wamejipanga kumshuhudi Majaba aliyejawa na
tabasamu akipita akiwa kwenye gari hilo la wazi.
Msafara
ulipofika Tegeta umati ulikuwa mkubwa na wengi waliokuwa wakimuona
Majaba walikuwa hawaamini macho yao kwani yeye mshindi alikuwa
akiwapungua mkono na msafara ukawa unaenda kwa mwendo wa polepole, hali
iliyofanya baadhi ya wananchi kumkaribia mshindi na walisikika wakisema
‘Hongera, Hongera!” Lakini abiria waliokuwa kwenye mabasi ya daladala
nao walionekana wakitoa vichwa vyao madirishani na kumpongeza Majaba
ambaye mara zote alikuwa na tabasamu usoni.
Hali
ilikua hivyo hivyo msafara ulipofika Boko na baada ya kufika Bunju
msafara ulisimama kabla ya kuingia Barabara ya Mabwepande ambapo kwa
mwendo mfupi tu msafara uliingia kwenye nyumba mpya ya Majaba. Mara
baada ya kufika, Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho alitambulisha kwa wageni
na wenyeji waliofika kushuhudia makabidhiano hayo na kisha akampa nafasi
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo kusema machache.
“Kifupi leo tunamkabidhi nyumba yake Bwana Majaba.
Ni
jambo linalofurahisha kuona yupo hapa na familia yake ya mke na watoto
watatu, hivyo bila kupoteza muda karibuni tufungue nyumba,” alisema
Shigongo. Baada ya kusema maneno hayo Shigongo, Majaba na mkewe
walishika utepe na Shigongo akaukata kuashirika kuwa sasa wamekabidhiwa
nyumba yao.
Baadaye
Majaba na watu wengine wakiongozwa na Shigongo waliingia ndani na
kuoneshwa kila chumba, baadaye nje na uani ambako kulikuwa na nafasi
kubwa na Shigongo alimuambia mke wa Majaba kwamba eneo hilo anaweza
kufanyia miradi kama ya kufuga. Wenyeji walimkaribisha Majaba na baadaye
wakapiga picha ya pamoja huku wakimpongesha kwa kushinda nyumba hiyo.
Shughuli hiyo iliisha saa moja kasoro robo jioni.
HABARI NA ELVAN STAMBULI, PICHA MUSSA MATEJA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni