Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Amina Shaban (kushoto)
akiupokea ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya, ukiongozwa na Kamishna wa
Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo Bw. Neven Mimica (katikati) na
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Bw. Roeland van de Geer,
walipokuwa wanawasili Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya kutoa msaada wa Euro milioni 50 kwa Tanzania.
Ujumbe
kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango
wakimsikiliza kwa makini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw.
Doto James akitoa maelezo ya ujio wa ugeni huo kuwa ni neema kwa nchi ya
Tanzania kwani Umoja wa Ulaya wametoa msaada wa Euro Milioni 50
utasaidia vijijini 3600 nchini kupata umeme.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) na akimweleza
jambo Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa
Ulaya Mr. Neven Mimica wakati wa hafla fupi ya Umoja wa Ulaya (EU)
kutiliana saini makubaliano ya msaada wa Euro milioni 50 kwa ajili ya
kusaidia usambazi wa umeme vijijini kupitia Mradi Kabambe wa Kusambaza
umeme Vijijini (REA).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akiwa pamoja na
Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Bw.
Neven Mimica wakisaini Mkataba wa msaada wa fedha za kusaidia usambazaji
wa umeme Vijijini (EURO milioni 50) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na Kamishna wa
Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Mr. Neven
Mimica, wakibadilishana hati za makubaliano ya msaada wa ruzuku ya kiasi
cha EURO Milioni 50 katika ukumbi wa wizara ya Fedha na Mipango, Jijini
Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akiwa na Ujumbe
kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na
Mipango wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mkataba wa
msaada wa utekelezaji wa nishati ya umeme vijijini katika ukumbi wa
Wizara ya fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akiagana na Kamishna
wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Bw. Neven
Mimica, baada ya kusaini mkataba wa msaada wa Euro milioni 50 ambazo
Umoja huo umeipatia Tanzania kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini
kupitia Wakala wa Umeme Vijijini REA.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango
………………
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
TANZANIA
imezidi kupata neema kutoka Jumuiya ya Kimataifa ambapo Novemba 2,
2017, Umoja wa Ulaya (EU) umeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 50,
takriban Shilingi bilioni 130 kwa ajili ya kufadhili Mradi Kabambe wa
Kusambaza Umeme Vijijini unaoendeshwa na Wakala wa Nishati Vijijini
(REA).
Mkataba
wa Makubaliano hayo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu
Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto
James na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa
Ulaya (EU) Bw. Neven Mimica.
Msaada
huo umelenga kuwasaidia raia wa Tanzania kufikiwa na huduma nafuu ya
nishati ya umeme kwa kupanua uwezo wa gridi ya Taifa pamoja na mtandao
wa usambazaji umeme.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James ameushukuru Umoja wa
Ulaya kwa msaada huo mkubwa utakaoiwezesha nchi kuwa na umeme wa
uhakika utakaochangia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya watu
wake.“Umoja
wa ulaya ni wadau wetu muhimu wa maendeleo kutokana na misaada muhimu
na mikubwa wanayotupatia, na kusadia agenda yetu ya maendeleo” alisema
Bw. James
Alisema
kuwa kiasi cha msaada wa Euro milioni 50 kilichotolewa na Umoja huo
bila masharti yoyote si kidogo, na kwamba kitasaidia kutatua changamoto
ya upatikanaji wa nishati ya umeme utakaochangia kuimarika kwa sekta ya
viwanda itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Bw.
Doto James alisema kuwa tangu Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini
REA uanze miaka 9 iliyopita, idadi ya vijiji vilivyounganishiwa umeme
imeongezeka kutoka vijiji 400 mwaka 2008 hadi kufikia vijiji 4395 hivi
sasa.
Alisema
kuwa ni matarajio ya Serikali kwamba ifikapo mwaka 2020, vijiji vyote
12,000 hapa nchini vitakuwa vimeunganishwa na nishati hiyo hivyo
kuchochea shughuli za uzalishaji viwandani na kiuchumi kwa wananchi,
vitaimarika.
Kwa
upande wake, Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja
wa Ulaya (EU) Bw. Neven Mimica, amesema kuwa msaada huo wa Euro milioni
50 wanaoutoa ni sehemu ya msaada wa Euro milioni 207 ambazo wanachama
wengine wa Umoja huo, ikiwemo Sweden, Uingereza, Norway na Benki ya
Dunia, watatoa kufanikisha mradi huo wa usambazaji umeme vijijini
kupitia REA.
“Nguvu
hizi za pamoja zitaviwezesha takriban vijiji 3,600 vilivyoko maeneo
mbalimbali ya nchi ambapo watu zaidi ya milioni 1 wanatarajiwa kunufaika
na mradi huo” Alisema Bw. Mimica.Alisema
hatua hiyo itachangia kuimarika kwa ubora wa maisha ya wananchi wa
Tanzania, kuimarika kwa sekta za afya, elimu na kuleta faida za kijamii
na kiuchumi zinazoonekana kwao moja kwa moja hususan wanawake na watoto.
Misaada
ya Umoja wa Ulaya kwa Tanzania imejikita katika Nyanja tatu za Utawala
bora, Umeme na Kilimo endelevu ambapo Umoja huo kupitia Mfuko wake wa
Maendeleo (EDF) umetenga kiasi cha Euro milioni 626 katika kipindi cha
kuanzia mwaka 2014-2020
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni