WALIMU WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA UJASIRIAMALI KWA AJILI YA KUJIINUA KIUCHUMI


Walimu wa wilaya ya Geita wakiwa kwenye  Kikao cha kujadili maendeleo na changamoto ndani ya chama cha walimu Wilaya ya Geita.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Mji wa Geita ,Leornad Kiganga Bugomola akizungumza na Walimu wakati wa kikao hicho uku akiwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa kujituma na pia aliwapongeza kwa kuweza kufanya vizuri kufikia hatua ya Mkoa kuchukua nafasi ya Pili kwenye mtihani wa darasa la saba Kitaifa.

Katibu wa chama cha Walimu Wilaya ya Geita,John Kifimbi akisoma risala kwa Mgeni rasmi.

Baadhi ya wageni waalikwa ambao wanatoka taasisi mbali mbali wakifuatilia kikao hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitoa vyeti kwa walimu ambao wamefanya vizuri ndani ya chama hicho.


Mwenyekiti wa chama cha walimu(CWT)Wilaya ya Geita,Alfred Alexander akiwasisitiza walimu kuendelea kuwa na mshikamao ndani ya chama hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasisitiza walimu kujingea tabia ya kuwa na vitega uchumi mbali mbali kwenye mazingira ambayo wanafanyia kazi.    
                                                      (PICHA NA JOEL MADUKA)
Walimu
Wilayani Geita wametakiwa kutumia nafasi walizonazo katika kujiinua kiuchumi
kwa kuwekeza kwenye Shughuli za ujasiriamali.

Rai
hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Geita,wakati wa Mkutano mkuu wa chama cha
Walimu (CWT)Wilaya ya Geita ambao  umefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
halmashauri ya Mji lengo likiwa  kuangalini ni kipi chama kimefanya ndani ya
miaka Miwili.
 alisema kuwa  wakati umefika kwa walimu kuwekeza katika fursa
za ujasiriamali na kutokuogapa kukopa na kwamba kama kuna mtu ambaye anampiga
vita mwalimu kuwekeza na huku anatekeleza majukumu yake ya msingi ni sawa na
kutokumtendea haki.
“Lengo
la kuandaa vitega uchumi kabla ya uzee na manufaa ya uwekezaji ni kwa manufaa
ya jamii kwa hiyo walimu kama kuna mtu anakupiga vita kwa ajili ya uwekezaji na
unafundisha kwa wakati sahihi mtu huyo nipeni taarifa”Alisema Kapufi.
Mwenyekiti
wa chama cha walimu Mkoani Humo,Mwl Lusato Zabron Mashauri ,ameelezea kuwa hali
ya kiuchumi bado ni mbaya kwa walimu hususani wale ambao wanaishi vijijini
wengi wao wamekuwa wakishindwa kufanya biashara kutokana na viongozi wengi wa
kisiasa kutokuwa na uelewa juu ya haki za walimu.
“Hali
ya kiuchumi kwa walimu hairidhishi hususani wale ambao wanaishi vijijini kwani
wengi wao wamekuwa wakipigwa vita na viongozi wa kisiasa mwalimu anapojaribu
kuinuka kiuchumi anapigwa vita na viongozi ao”Alisema Lusato.
Kemilembe
Gerigori ambaye anawawakilisha walimu wanawake Mkoani Humo,alisema hali ya
mazingira ya walimu ni magumu kutokana na namna ambavyo wamebanwa katika suala
la muda wa masomo hivyo wengi wao wamekuwa wakishindwa kujishughulisha na
ujasiriamali kwa kukosa muda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni