WIZARA, TAASISI ZA SERIKALI ZITUMIE NISHATI MBADALA – WAZIRI MKUU


PMO_3395
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuzindua Maadhisho ya Wiki ya Mazingira, Mei 31, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
PMO_3397
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es salaam, Kate Kamba wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam kuzindua Wiki ya Mazingira, Mei 31, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani , Mhandisi Evarest Ndikilo.
PMO_3433
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Space Engineering Limited, Bw. Philip Mtui kuhusu mkaa uliotengenezwa kutokana na takataka na kufungashwa kwenye kiroba tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. katikati ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo.
PMO_3441
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji  wa Kampuni ya  Space Engineering Limited, Bw. Philip Mtui kuhusu  mkaa uliotengenezwa kutoka na takataka na kufungashwa kwenye kiroba tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo na kushoto ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Neema Matemba.
PMO_3461
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipata Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Edosama Hardware Limited, Edward Maduhu kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotokana na miti ambazo zinatengenezwa na kampuni hiyo wakati alipotembelea mabada ya maonyesho  kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es salaam, Kate Kamba.
PMO_3464
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Edosama Hardware Limited, Edward Maduhu kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotokana na miti ambazo zinatengenezwa na kampuni hiyo wakati alipotembelea mabada ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba
PMO_3522
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Nimwagile Mwaijumba wakati alipotembelea banda la Kituo cha Utengenezaji magari cha Nyumbu  na kujionea mashine ya kutengeneza mkaa bora kwa kutumia takataka iliyobuniwa na kutengenezwa na kituo hicho. Waziri Mkuu alitembelea mabanda ya maonyesho  kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Opwani Mhandisi, Evarest Ndikilo.
PMO_3578
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya JHS , David Mwendapole  wakati alipotoa maelezo kuhusu majiko makubwa yanayotumia  gesi kidogo  katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Wanne kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.
PMO_3617
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018.
PMO_3658
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018.
PMO_3670
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi baada ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala, Mwenyekiti wa CC wa Mkoa wa Dar es alaam, Kate Kamba,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori  na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
………………
*Aagiza viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wabadilike
*Ataka wasimamie wananchi waachane na matumizi ya mkaa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara, mashirika na taasisi zote za Serikali na binafsi zianze kutumia nishati mbadala ili kuondoa kabisa matumizi ya kuni na mkaa.

“Wizara, taasisi na mashirika yote ya Serikali na binafsi pamoja na vikundi vya uzalishaji wanaotumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia au shughuli za uzalishaji waanze kutumia nishati mbadala ili matumizi ya mkaa yaishe na ikiwezekana yatoweke kabisa,” amesema.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Mei 31, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Mkaa ni Gharama: Tumia Nishati Mbadala.”

Waziri Mkuu amesema teknolojia bora ya uzalishaji wa mkaa mbadala ambayo ameiona kwenye maonesho hayo, ikuzwe na kusambazwa kote nchini ili kuwawezesha wananchi walio wengi waachane na matumizi ya mkaa wa kawaida na badala yake watumie mkaa-mbadala kwa lengo la kuhifadhi misitu na kupunguza uharibifu wa mazingira.

Ili kufanikisha matumizi ya teknolojia hiyo, Waziri Mkuu amesema vibali vya ujenzi wa majengo makubwa na taasisi kama shule, vyuo, hospitali navyo pia vianze kuzingatia ufungaji wa mifumo ya nishati ya gesi kwa ajili ya matumizi ya kupikia ili kurahisisha upatikanaji na matumizi ya nishati mbadala katika taasisi na majengo makubwa.

“Wahandisi na wachoraji ramani za majengo waweke njia za kupitisha kwenye michoro yao ili ujenzi wa nyumba na majengo haya ukikamilika, watumiaji waweze kutumia teknolojia hiyo,” amesema.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Mkoa wa Dar es Salaam ni lazima ubadilike na uachane na matumizi ya mkaa. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, mkoa huo unatumia tani 500,000 za mkaa kwa mwaka.

“Viongozi wa mkoa na wilaya ondokeni hapa na hili kama ajenda ya mkoa wa Dar es Salaam, mkaifanyie kazi na Wizara pia ifuatilie mmetekeleza kwa kiasi gani. Jitihada zilizofanywa na Jiji la Dar es Salaam kupitia kwa Mstahiki Meya, za kuanza kuwapa mtaji wajasiriamali hawa wanaotengeneza teknolojia mpya ni lazima ziigwe na nyie kwenye Manispaa zenu.”

“Meya ametoa fursa na amewaanzishia, na ninyi sasa endeleeni. Tengenezeni bajeti kupitia Mabaraza ya Madiwani na muwaunge mkono wajasiriamali wanaotengeneza haya majiko kwa kuwapa teknolojia hii kwenye maeneo yenu. Wanaotengeneza mashine za mkaa mbadala, wawezeshwe watengeneze mashine nyingi zaidi na zije kila Manispaa, ili kila Manispaa ianze kutumia teknonolojia hiyo kupikia,” alisisitiza.

Amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji la Dar es Salaam wafuatilie kwa karibu usambazaji wa teknolojia hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Yusuf Makamba amesema hali ya mazingira hapa nchini ni mbaya licha ya kuwa haionekani kwa haraka na watu waishio mijini.

“Hali ya mazingira nchini mwetu ni mbaya sana na inawezekana watu wanaoishi Dar es Salaam hawaioni kwa haraka kwa sababu mahitaji yao yote wanayapata sokoni na madukani,” alisema.

“Wenzetu wa mikoani na vijijii wanaotegemea mvua na udongo wenye rutuba wanataabika kwa sababu kipato chao kinaathirika kutokana na uharibifu wa mazingira,” alisema.  

Alisema mazingira yanafungamana na utalii, kilimo, ufugaji, nishati, maji na kwamba maendeleo ya nchi pia yamefungamana moja kwa moja na mazingira. “Asilimia 90 ya Watanzania wanatumia kuni na mkaa kupikia lakini asilimia 70 ya mkaa wote unaozalishwa nchini Tanzania, unatumika jijini Dar es Salaam,” alisema.

Waziri Makamba alisema taasisi za Serikali kama vyuo, magereza, hospitali na shule zinaongoza kwa matumizi ya kuni na mkaa na hivyo kuchangia uharibifu mkubwa wa mazingira.

Akitoa mfano, alisema Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kina wanafunzi wapatao 30,000 na kinalazimika kuandaa milo mitatu kila siku.

“Chuo hiki kina migahawa tisa, kule nyuma kumejaa magogo ya kuni. Kuna mgahawa mmoja mdogo unatumia magunia 17 ya mkaa kwa siku, sasa huo mkubwa unatumia magunia mangapi?” alihoji.

Maadhimisho hayo yaliyozinduliwa leo, yataendelea hadi Juni 5, mwaka huu ambayo ni siku ya kilele. Pia wiki nzima kutakuwa na makongamano, midahalo na mjadala wa kitaifa.

KINANA AMKABIDHI RASMI OFISI KATIBU MKUU MPYA DK. BASHIRU, LEO

Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkabidhi ‘zana’ Katibu Mkuu mpya wa CCM Dk. Bashiru Ally, katika makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally akiwasalimia baadhi ya viongozi alipowasili, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya makabidhiano hayo.
Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana kwa furaha na Katibu Mkuu CCM Dk. Bashiru Ally, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, Dk. Bashiru alipofika kwa ajili ya makabidhiano hayo, leo
Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally akiongozana na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Abdulrahman Kinana, wakati wakienda ofisini kufanya makabidhiano hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally akiongozana na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Abdulrahman Kinana kuingia ukumbini kuzungumza na watumishi wa Chama, katika Ofisi8 Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally akikiwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Abdulrahman Kinana baada ya kufika meza kuu kwa ajili ya kuzungumza na watumishi wa Chama, katika Ofisi8 Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humprey Polepole akitoa maneno ya utangulizi
 Baadhi ya watumishi wa CCM wakiwa ukumbini
 Baadhi ya watumishi wa Chama wakiwa ukumbini
  Baadhi ya watumishi wa Chama wakiwa ukumbini
  Baadhi ya watumishi wa Chama wakiwa ukumbini
 Makatibu Wakuu wa  Jumuia za Chama wa sasa na wastaafu wakiwa ukumbini
 Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Abdulrahman Kinana akikumbatiana kwa furaha na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally baada ya kuzungumza hotuba ya kuaga wafanyakazi wa Chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally akizungumza na wafanyakazi wa Chama
 Kinana akipongeza hotuba ya Dk Bashiru kwa wafanyakazi
 Picha ya pamoja
 Picha ya pamoja na Makatibu wasaidizi
 picha ya pamoja na watum ishji wa Chama

Serikali Kuendelea Kuchukua Hatua za Kisera Kuhakikisha Riba za Mikopo Zinapungua Nchini


PIX-4-6-1
Na: Mahmoud Ahmad, Dodoma.
Serikali imesema kuwa pamoja na huduma za bidhaa ya fedha kuamuliwa na nguvu ya soko  kwa upande wake imekuwa ikichua hatua za kisera ili kuhakikisha kuwa riba za mikopo zinapungua katika soko hapa nchini.
Hayo yameelezwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Konde, Mhe. Khatibu Haji juu ya Serikali inachukua hatua gani ili benki ziweze kupunguza viwango hivyo vya riba?
“Baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kupitia Benki Kuu ni pamoja na kuzitaka benki za biashara kutumia mfumo wa kuhifadhi na kutoa taarifa za wakopaji (Credit Reference Bureau System). Aidha, Benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo ya muda mfupi kwa benki za biashara kwa kiwango cha asilimia 6.89,” amesema Dkt. Kijaji.
Dkt. Kijaji amezitaja hatua nyingine zilizochukuliwa kuwa ni Benki Kuu kushusha riba (Discount Rate) kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0 pamoja na kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu na benki za biashara (Statutory Minimum Reserve Requirememnt (SMR)) kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0.
Vile vile Serikali imeendelea kulipa malimbikizo ya madai yaliyohakikiwa kwa lengo la kupunguza kiwango cha mikopo chechefu na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi.
Aidha, amesema baada ya hatua hizo za kisera kuchukuliwa na Serikali, baadhi ya benki za biashara hapa nchini zimeanza kupunguza riba za mikopo.
Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kuchukua hatua za kisera ili kuhakikisha kuwa riba za mikopo katika soko zinaendelea kupungua.

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA


1
Waziri wa Madini Mhe. Angellah   Kairuki akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019 leo Bungeni  Jijini Dodoma.
2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu  Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo  Bungeni kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali katika kuwalinda watoto wa kike ambapo ameahidi kuwa Serikali itatoa taarifa rasmi kuhusu kuwepo kwa baadhi ya watu wanaowadhalilisha kijinsia watoto wa kike  na hatua zilizochukuliwa na Serikali.
3
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kupambana na Janga la Ukimwi hapa nchini ikiwemo kuhamasisha upimaji wa Virusi vya UKIMWI  hasa kwa wanaume kote nchini ili wajue hali zao na kuchukua hatua stahiki.
4
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo (wakwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe Angellah Kairuki Bungeni Jijini Dodoma leo.
5
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula aliyesimama (kushoto) na Mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo Prof. Abdulkarim Mruma wakitambulishwa Bungeni leo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.
6
Sehemu ya Viongozi wa Tume ya Madini na wageni  mbalimbali wakiwemo wakuu wa Mikoa yenye madini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Bungeni Jijini Dodoma leo.
7
Sehemu ya Wanafunzi waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
( Picha zote na mahmoud ahmad)

SERIKALI YAAGIZA WAMACHINGA WATENGEWE MAENEO YA KUFANYIA BIASHARA

www.manyaraleotz.blogspot.com

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na wamachinga wakati  wa kufungua  Mkutano Mkuu wa Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania- SHIUMA leo uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Dodoma, Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na wamachinga wakati  wa kufungua  Mkutano Mkuu wa Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania- SHIUMA leo uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Dodoma, Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo  akiongea na baadhi ya viongozi wa shirika la umoja wa wamachinga Tanzania – SHIUMA leo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma, Jijini Dodoma.

Na Mahmoud Ahmad,

Wakuu wa Wilaya wameagizwa kuzisimamia halmashauri nchini kuhakikisha kuwa zinatenga maeneo maalum ya kufanyia biashara ndogondogo (machinga) ili  waweze kuendesha shughuli zao bila kuvunja sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali. 

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemeni Jafo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania – SHIUMA uliofanyika leo katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Dodoma, Jijini Dodoma.

Alisema Wakuu wa Wilaya wana wajibu wa kuratibu na kuhakikisha kuwa maeneo ya kufanyia bishara kwa wamachinga yanatengwa na Halmashauri ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa utaratibu bila kuvunja sheria za nchi. 

Aliongeza kuwa wamachinga ni watu muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania kwa kuwa wafanyabiashara wadogo ndio wanaoleta muunganiko wa watu katika kada mbalimbali wakiwemo wasomi wenye shahada, astashaada, kidato cha sita, kidato cha nne, darasa la saba na wasiosoma kabisa wote huunganika na kufanyabiashara kama wamachinga.

Alisema kati ya watanzania milioni 50, walioajiriwa serikalini na sekta ya umma ni 520,000, hivyo kundi kubwa ni la watu ambao ama wamejiajiri au wameajiriwa katika sekta binafsi.   
“Lakini kundi kubwa ni wale watu wanaojishughulisha kwa kutafuta riziki zao wenyewe ambao watu hao ndio unapata asilimia kubwa wako katika kundi la wamachinga,” alisema Mhe.Jafo na kuongeza:

“Utakuta mtu anafanyabishara katika mazingira magumu ambayo yanamfanya kila wakati kutokuwa na uhakika wa kupata kipato cha siku jambo ambalo linaathiri familia yake na kuongeza umaskini nchini, hivyo ifike mahali wakuu wa Wilaya waweke mikakati ya kuhakikisha wamachinga wote wanapatiwa maeneo bora ya kufanyia biashara ili wajikwamue kiuchumi,  “alisisitiza Waziri 

Aliongeza kuwa Serikali imejiwekea mkakati wa kutengeneza masoko mazuri na ya kisasa kwa kuweza kuweka mazingira bora kwa wamachinga kufanya biashara zao katika maeneo stahiki.

Aidha Waziri Jafo alisema kuwa Viongozi wanatakiwa kutafakari na kutatua kero ya maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara wamachinga, hivyo serikali imeanza mpango mkakati  wa ujenzi wa masoko mazuri ya kisasa ili wafanyabishara waweze kufanya kazi katika mazingira bora na tayari imetenga shilingi bilioni 149 kwa ajili ya ujenzi wa masoko, stendi za kisasa na viwanda vidogo.

“Nimetoa maagizo soko lolote litakalojengwa lazima mustakabali wa wafanyabiashara wadogo wadogo waliokuwepo awali umejulikana na kuwa kipaumbele kwa kupatiwa maeneo ya kufanyia biashara pindi majengo hayo yanapokamilika hivyo viongozi wa halmashauri wahakikishe wanatoa kipaumbele kwa wafanyabiashara waliokuwepo awali,” alisema Jafo.  
Alisema kuwa Serikali imekuwa ikiwekeza katika miradi mikubwa ikidhani inawagusa maskini lakini kwa bahati mbaya masoko mengi yanayojengwa wanaonufaika ni watu wenye fedha na kuwaacha wafanyabiashara waliokuwepo awali kabla soko kujengwa. 

Hivyo nawaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wananchi masikini wanapatiwa nafasi katika masoko hayo ili waweze kujiongezea kipato.Amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri wote nchini kuhakikisha kuwa kabla soko halijaanza kujengwa kufanyike tathmini ya wafanyabishara waliokuwepo awali ili wawe kipaumbele pale soko linapokamilika.

Wakati huohuo Mhe. Jafo amewataka wamachinga nchini kuhakikisha wanajiunga na bima iliyoboreshwa ili iwawezeshe kuwasaidia pale wanapokuwa wagonjwa wao na familia zao kwa kuwa afya ni uhai.

RAS SHINYANGA AFUNGUA MAFUNZO KWA KAMATI YA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela amefungua mafunzo kwa wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga yanayolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kupiga vita ukatili katika jamii.

Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza leo Jumatano Mei 30,2018 yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga yamekutanisha wadau mbalimbali wanaohusika katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Investing in Children and their Societies (ICS – Africa). 

Awali akizungumza,Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Glory Mbia alisema lengo la mafunzo hayo ni kupata maoni na mapendekezo mbalimbali katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. “Lengo la mafunzo haya ni kupata uelewa wa pamoja na kutengeneza mkakati namna gani tunafanya katika kutokomeza vitendo vya kikatili katika mkoa”,alisema Mbia. 

Akifungua mafunzo hayo, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo alisema mkoa wa Shinyanga bado una tatizo kubwa la ukatili dhidi ya watoto na wanawake hivyo zinahitajika nguvu za pamoja 

“Tunamshukuru mwenyezi Mungu mauaji dhidi ya albino yamebaki historia katika mkoa wetu,lakini katika jamii kumekuwa na unyanyasaji hasa wa watoto,kupitia kamati hii naamini kwa pamoja kama tutaamua kwenda pamoja hatua kwa hatua tutaweza kutokomeza vitendo vya ukatili katika mkoa huu”,alieleza Msovela. “Akina mama na watoto wengi wameathirika kisaikolojia,kimwili,wapo watoto wamekosa elimu kutokana na unyanyasaji wanaopitia kwa pamoja naamini sheria ambazo zipo na umoja huu tutaweza kukabiliana na ukatili wanaofanyiwa wanawake na watoto”,alisema. 

“Kwa namna ya pekee niwashukuru sana wadau wetu wa maendeleo ICS ambao wamejitolea kudhamini mafunzo haya,na hivi sasa kamati imeshaundwa kutoka katika ngazi ya kata,halmashauri na sasa tunaendelea na mafunzo kwa ngazi ya mkoa”,aliongeza Msovela. 

Kwa upande wake,Afisa Maendeleo Mwandamizi, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mathias Haule alisema umaskini umekuwa chanzo cha vitendo ukatili dhidi ya wanawake hivyo ili kutokomeza vitendo hivyo ni vyema wanawake wanapaswa kuwezeshwa kiuchumi huku wadau wote wakiweka nguvu pamoja katika kuwalinda na kuwatetea wanawake na watoto. 

Naye Meneja wa shirika la ICS nchini,Kudely Sokoine Joram alisema ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,shirika hilo limekuwa likishirikiana na serikali ili kuhakikisha wanawake na watoto wanakuwa salama katika jamii. 

“Kupitia mradi wetu wa masuala ya ulinzi na usalama wa watoto tunafanya mradi huu katika manispaa ya Shinyanga,Shinyanga Vijijini na wilaya ya Kishapu na baada ya serikali kumaliza kutengeneza mwongozo,ilituomba tunapokuwa na rasilimali basi tuweze kusaidia serikali kuhakikisha kamati zinaundwa na zinapata mafunzo ndiyo maana hata haya mafunzo tumeyawezesha sisi”,alieleza. 

Meneja huyo wa ICS alisema katika ngazi ya halmashauri,kata na vijiji mpaka sasa wamezisaidia kamati 25 wakishirikiana na serikali na wanaendelea kuwezesha uundwaji wa kamati ili kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 

“Sisi kama wadau wa maendeleo tunashughulika na masuala ya malezi na matunzo bora ya watoto,masuala ya ulinzi wa watoto kwa mfano miongozo ya serikali na sheria zilizopo lakini pia kuwezesha familia katika masuala ya kiuchumi,kujenga uwezo wa taasisi ndogo ndogo na maeneo husika yanayoshughulika na maendeleo ya jamii”,alisema Joram. 
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifungua mafunzo ya kujengea uwezo kwa wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga leo Mei 30,2018 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifungua mafunzo na kuwataka wajumbe wa kamati hiyo kushirikiana katika kupiga vita vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Glory Mbia akielezea malengo ya mafunzo hayo ambapo alisema lengoni kupata maoni na mapendekezo mbalimbali kuhusu namna ya kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga. 
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Meneja wa shirika la ICS nchini Tanzania, Kudely Sokoine Joram akizungumza wakati wa mafunzo hayo ambapo alisema wameamua kufadhili mafunzo hayo ili kushirikiana na serikali katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Meneja wa shirika la ICS nchini Tanzania, Kudely Sokoine Joram akizungumza ukumbini.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon akielezea namna wanavyoshiriki katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.


Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Afisa Maendeleo Mwandamizi, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mathias Haule akielezea Muhtasari kuhusu Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.

Kushoto ni Afisa Maendeleo Mwandamizi, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mathias Haule na Afisa Mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto kutoka shirika la ICS mkoa wa Shinyanga,Shadia Nurdin wakiangalia nyaraka zinahusu masuala ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog