RC GAMBO:²WAAJIRI WACHENI KUWATISHA WAFANYAKAZI WENU

Na. Mahmoud Ahmad, Arusha

Mkuu wa mkoa mrisho Gambo amewataka waajiri kupokea changamoto za wafanyakazi na kuzitatua sambamba na wafanyakazi kuwa huru kusema   changamoto wanazokumbana nazo.

Gambo  amekemea kitendo cha baadhi ya waajiri wanaowatisha wafanyakazi,amesema kuwa jambo hilo halikubaliki ,atakapobainihatua stahiki zitachukuliwa.

"Nimepata taarifa kuna maeneo ambayo wafanyakazi waliweza kutoa kero zao na maoni yao na baadhi ya waajiri waliwatisha ,jambo hilo halikubaliki na atakapobainika sheria stahiki zitachukuliwa dhidi yake" alisema Gambo
Ameyazungumza hayo katika sherehe za mei mosi Jijiji Arusha ambapo alikuwa mgeni rasmi  na kutilia mkazo kuwa yapo malalamiko ya watumishi wa serikali kukamatwa na kuwekwa ndani kwa makosa ambayo ni ya kiutumishi,amewataka viongozi kufanya kazi kwa weledi,kwakuzingatia sheria na taratibu. 

"Kama mfanyakazi amefanya kosa la kiuhalifu,ashughulikiwe kama mhalifu,bali kama kosa ni la kiutumishi,zipo sheria na kanuni za kitumishi ni vyema zikazingatiwa" 

Amesema wafanyakazi wanatakiwa kuwa na ujasiri wa kufanya kazi kwani viongozi pekee wa mkoa hawawezi kusukuma gurudumu la maendeleo bila ya kushirikuana na wafanyakazi ambao ni wadau muhimu katika nchi.

Akijibu risala ya wafanyakazi Jijini Arusha iliyosomwa na Katibu wa Tughe  Samweli Magero amesema kuwa changamoto ya uhaba wa majaji tayari mhe.Rais alifanya uteuzi wa majaji kadhaa ikiwa ni sehemu ya jitihada ya kwenda kuziba mapengo yaliyokuwepo.

Mwisho aliwapongeza wananchi kwa ujumla pamoja na wafanyakazi kuwa wameweza kuonyesha uzalendo kwa mkoa kwani Arusha imebadilika kwa kuithamini amani kuliko chochote
Wakwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambae ni mgeni rasmi katika sherehe za mei mosi ,akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,,Katibu tawala wa Jiji la Arusha Charles Kwitega na Karibu wa Tughe Jijini hapo Samweli Magero.
Meza kuu wakiwa wanafurahia jambo wakati wakati Maandamano ya wafanyakazi yakiingia uwanjani .
Baadhi ya wafanyakazi kutoka kiwanda cha A-Z wakiwa wanapita mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za meimosi katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid Jijini Arusha.
Pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha Jijini Arusha katika uwanja wa  Shekh Amri Abaid bado wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali waliendelea kusalia uwanjani bila kuondoka katika sherehe za Mei Mosi mkani hapo.
Fedy Sanga( kulia)akikabidhiwa cheti na Hundi ya Sh, milioni 1 baada ya kuteuliwa kuwa mfanyakazi bora Kwa wafanyakazi wa Jiji la Arusha. Picha na


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni