Mhandisi Dk Richard Masika |
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Isack Kamwele amemteua Mhandisi Dk. Richard Masika kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jiji la Arusha(AUWSA) kuanzia April 23 hadi April 22, 2021.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini,Athumani Shariff ilisema Dk Masika alikua Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha hadi alipostaafu Septemba 30,2017.
Pia Mhandisi Kamwele amewateua wajumbe tisa wa bodi ya AUWSA ambao ni Richard Kwitega(Katibu Tawala mkoa),Athumani Kihamia(Mkurugenzi wa Jiji),Francis Mbise(Diwani wa Kata ya Muriet,Vincent Lasway(Mfanyabiashara) na Elishilia Kaaya(Mkurugenzi Mtendaji-AICC).
Wajumbe
wengine ni Jackiline Mkindi(Mkurugenzi wa (TAHA),Mhandisi Ruth
Koya(Mkurugenzi Mtendaji wa AUWSA),Edward Mrosso(Wakili) na Agnela
Nyoni(Mwakilishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji).
Katika
uteuzi mpya Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha kwa nafasi yake huingia
moja kwa moja lakini wakati huu hakuteuliwa baada ya Bodi iliyopita
kuvunjwa Januari 19,2018 na Waziri wa Maji kwasababu ya kutoridhishwa
kiutendaji.
Bodi iliyopita Mwenyekiti alikua Dk Job Laizer,Richard Kwitega,Athumani Kihamia,Kalist Lazaro,Agnela Nyoni,Charles Marunda,Thomas Mosso,Halima Mamuya,Mhandisi Felix Godfrey na Mhandisi Ruth Koya.
Bodi iliyopita Mwenyekiti alikua Dk Job Laizer,Richard Kwitega,Athumani Kihamia,Kalist Lazaro,Agnela Nyoni,Charles Marunda,Thomas Mosso,Halima Mamuya,Mhandisi Felix Godfrey na Mhandisi Ruth Koya.
Pia Dk Masika ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Michezo Malya katika uteuzi uliofanywa na Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo,Dk Harrison Mwakyembe April 4 mwaka huu.
Akizungumza na Mwananchi jana,Dk Masika alisema bado ni mapema kuzungumzia mikakati ya Bodi mpya kwakua haijazinduliwa ila atajitahidi kuongeza tija,ufanisi na kutoa huduma bora zaidi.
"Bodi ikishazinduliwa na kuanza kazi tutajitahidi kutekeleza wajibu wetu kwa weledi,ubunifu,bidii na uaminifu kwaajili ya kuwahudumia wananchi wetu,"alisema Dk Masika.
Serikali imetoa kiasi cha Sh 514 bilioni kwaajili ya kuhakikisha kero ya maji katika jiji la Arusha na viunga vyake linakua historia na utekelezaji wa mradi umeshaanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni