Katibu
Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela amefungua mafunzo kwa wajumbe
wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa
Shinyanga yanayolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kupiga vita ukatili
katika jamii.
Mafunzo
hayo ya siku tatu yaliyoanza leo Jumatano Mei 30,2018 yanayofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga
yamekutanisha wadau mbalimbali wanaohusika katika kutokomeza ukatili
dhidi ya wanawake na watoto kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali
la Investing in Children and their Societies (ICS – Africa).
Awali
akizungumza,Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Glory Mbia
alisema lengo la mafunzo hayo ni kupata maoni na mapendekezo mbalimbali
katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. “Lengo
la mafunzo haya ni kupata uelewa wa pamoja na kutengeneza mkakati namna
gani tunafanya katika kutokomeza vitendo vya kikatili katika
mkoa”,alisema Mbia.
Akifungua
mafunzo hayo, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela ambaye ni
mwenyekiti wa kamati hiyo alisema mkoa wa Shinyanga bado una tatizo
kubwa la ukatili dhidi ya watoto na wanawake hivyo zinahitajika nguvu za
pamoja
“Tunamshukuru
mwenyezi Mungu mauaji dhidi ya albino yamebaki historia katika mkoa
wetu,lakini katika jamii kumekuwa na unyanyasaji hasa wa watoto,kupitia
kamati hii naamini kwa pamoja kama tutaamua kwenda pamoja hatua kwa
hatua tutaweza kutokomeza vitendo vya ukatili katika mkoa huu”,alieleza
Msovela. “Akina mama na watoto wengi wameathirika
kisaikolojia,kimwili,wapo watoto wamekosa elimu kutokana na unyanyasaji
wanaopitia kwa pamoja naamini sheria ambazo zipo na umoja huu tutaweza
kukabiliana na ukatili wanaofanyiwa wanawake na watoto”,alisema.
“Kwa
namna ya pekee niwashukuru sana wadau wetu wa maendeleo ICS ambao
wamejitolea kudhamini mafunzo haya,na hivi sasa kamati imeshaundwa
kutoka katika ngazi ya kata,halmashauri na sasa tunaendelea na mafunzo
kwa ngazi ya mkoa”,aliongeza Msovela.
Kwa
upande wake,Afisa Maendeleo Mwandamizi, Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mathias Haule alisema umaskini umekuwa
chanzo cha vitendo ukatili dhidi ya wanawake hivyo ili kutokomeza
vitendo hivyo ni vyema wanawake wanapaswa kuwezeshwa kiuchumi huku wadau
wote wakiweka nguvu pamoja katika kuwalinda na kuwatetea wanawake na
watoto.
Naye
Meneja wa shirika la ICS nchini,Kudely Sokoine Joram alisema ili
kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,shirika hilo
limekuwa likishirikiana na serikali ili kuhakikisha wanawake na watoto
wanakuwa salama katika jamii.
“Kupitia
mradi wetu wa masuala ya ulinzi na usalama wa watoto tunafanya mradi
huu katika manispaa ya Shinyanga,Shinyanga Vijijini na wilaya ya Kishapu
na baada ya serikali kumaliza kutengeneza mwongozo,ilituomba tunapokuwa
na rasilimali basi tuweze kusaidia serikali kuhakikisha kamati
zinaundwa na zinapata mafunzo ndiyo maana hata haya mafunzo
tumeyawezesha sisi”,alieleza.
Meneja
huyo wa ICS alisema katika ngazi ya halmashauri,kata na vijiji mpaka
sasa wamezisaidia kamati 25 wakishirikiana na serikali na wanaendelea
kuwezesha uundwaji wa kamati ili kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya
wanawake na watoto.
“Sisi
kama wadau wa maendeleo tunashughulika na masuala ya malezi na matunzo
bora ya watoto,masuala ya ulinzi wa watoto kwa mfano miongozo ya
serikali na sheria zilizopo lakini pia kuwezesha familia katika masuala
ya kiuchumi,kujenga uwezo wa taasisi ndogo ndogo na maeneo husika
yanayoshughulika na maendeleo ya jamii”,alisema Joram.
Katibu
Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifungua mafunzo ya kujengea
uwezo kwa wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na
watoto mkoa wa Shinyanga leo Mei 30,2018 - Picha zote na Kadama Malunde -
Malunde1 blog
Katibu
Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifungua mafunzo na kuwataka
wajumbe wa kamati hiyo kushirikiana katika kupiga vita vitendo vya
ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Afisa
Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Glory Mbia akielezea malengo ya
mafunzo hayo ambapo alisema lengoni kupata maoni na mapendekezo
mbalimbali kuhusu namna ya kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya
wanawake na watoto mkoani Shinyanga.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Meneja
wa shirika la ICS nchini Tanzania, Kudely Sokoine Joram akizungumza
wakati wa mafunzo hayo ambapo alisema wameamua kufadhili mafunzo hayo
ili kushirikiana na serikali katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi
ya wanawake na watoto.
Meneja wa shirika la ICS nchini Tanzania, Kudely Sokoine Joram akizungumza ukumbini.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon akielezea namna wanavyoshiriki
katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na
watoto mkoani Shinyanga.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Afisa
Maendeleo Mwandamizi, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na
Watoto, Mathias Haule akielezea Muhtasari kuhusu Mpango kazi wa taifa
wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Kushoto
ni Afisa Maendeleo Mwandamizi, Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,
Jinsia,Wazee na Watoto, Mathias Haule na Afisa Mradi wa kutokomeza
ukatili dhidi ya watoto kutoka shirika la ICS mkoa wa Shinyanga,Shadia
Nurdin wakiangalia nyaraka zinahusu masuala ya kuzuia ukatili dhidi ya
wanawake na watoto.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni