Halmashauri ya Wilaya ya Karatu imefanikiwa kujenga ghala
bora la kisasa kwa wakulima wa vitunguu na ukarabati wa barabara vilivyogharimu
kiasi cha bilioni 3 katika kijiji cha Mang’ora.
Akitoa taarifa hiyo kwa timu ya ukaguzi kutoka taasisi
ya Marketing Infrastricture,Value Addition and Rural Finance Support ( MIVARF)
na Benki ya maendeleo Afrika, Mkurugenzi wa halmashauri bwana Waziri Mourice amesema halamshauri yake
imefanikiwa kutoa 5% katika ujenzi wa ghala la vitunguu na ukarabati wa
barabara.
“Kweli tumejitaidi sana kama halmashauri kutoa 5% ya
makusanyo yetu ya ndani na kufanikisha ujenzi wa ghala na ukarabati wa barabara
zenye urefu wa kilomita 27”.
Ukarabati wa barabara
katika bonde la Eyasi umegharimu kiasi cha bilioni 1.5 na ujenzi wa ghala umegharimu
kiasi cha bilioni 1.5 ambapo na halmashauri ilichangia milioni 153.
Amesema ghala hilo limekuwa msaada mkubwa sana kwa
wakulima kwa kuwaunganisha kwa pamoja kupitia chama chao,pia ghala hilo
litawawezesha wakulima kupanga bei moja ya manunuzi na kuwawezesha kupata
masoko ya ndani na nje ya nchi.
Bwana Waziri ameishukuru MIVARF kwa mchango wao mkubwa
katika kufanikisha shughuli hizo za maendeleo katika halmashauri hiyo na kuomba
zaidi ushirikiano katika kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo zikiwemo ujenzi
wa kiwanda cha kuchakata mahindi,kufufua kiwanda cha kusindika maziwa na ujenzi
wa hospitali ya wilaya.
Akifafanua zaidia bwana Salum Ramadhani mtaalamu wa
mambo ya kilimo kutoka Benki ya maendeleo Afrika,amesema lengo la timu hiyo
kutoka MIVARF makao makuu ni ukaguzi wa miradi inayofahiriwa na taasisi hiyo
ambao unafanywa kila baada ya miezi 6.
Amesema mradi wa ghala la vitunguu ulilenga zaidi kuweka
utaratibu wa kuwa na soko la pamoja kwa wakulima wenyewe wa vitunguu na hii
itasaidia kupunguza uuzaji wa kiholela kwenda nchi jirani.
Ameipongeza halmashauri kwa kufanikiwa kutoa asilimia 5
ya mapato yake katika ujezi wa ghala hilo na ukarabati wa barabara kwani ni
halmashauri nyingi zimeshindwa kufanya hivyo.
Aidha, amewashauri wakulima kutafuta masoko ya vitunguu
vyao kwa kutafuta taarifa za bei na masoko kutoka sehemu mbalimbali ili wawe na
uweleza mpana zaidi.
Mwenyekiti wa halmashauri mheshimiwa Jublate Gerson
Mnyenye amesema Changamoto kubwa wanayoipata kama halmashauri ni ujazaji wa
maguni kwa lumbesa inayopelekea wakulima kupata hasara.
Hata hivyo amesema bado wakulima wa vitunguu
wanachangamoto ya mafuriko kuingia kwenye mashamba yao inayopelekea hasara kwa
kupata mavuno hafifu.
Bado halmashauri inaendelea kuandaa utaratibu wa
kuwasaidia wakulima kuweza kusafirisha mazao yao kutoka mashambani hadi kwenye ghala.
Akisisitiza zaidi mratibu wa MIVARF upande wa
miundombinu ya masoko Bwana Jacob Mwambene amesema, wakulima hao wanatakiwa
kulitumia hilo ghala kama malengo yalivyokusudiwa kwa kuwa mradi huo ulilenga
kumwinua mkulima mdogo na wakati katika kilimo cha vitunguu.
Nae katibu wa chama cha wakulima wa vitunguu (LECOFANET)
Elia Bacheng, amesema bado kuna uhaba wa visanduki vya kuwekea vitunguu kwani
vilivyopo havikidhi mahitaji ya sasa.
Aidha,wameiomba serikali iongeze mizani yakupimia
magunia yanapokuwa yanaingia katika ghala hilo .
Pia Changamoto nyingine ni kutokuwa na bei maalumu kwa
uuzaji wa vitunguu kwani wanaopanga bei kwa sasa ni madalali ambao baadhi yao
ni wakulima wenzao inayopelekea wakulima kuuza vitunguu vyao kwa hasara.
Ujenzi
wa ghala la vitunguu lilifunguliwa rasmi Novemba 2017 kwa lengo la
kuwasaidia uuzaji wa vitunguu kwa wakulima wa vijiji vya
Mang’ola na Baray kuwa na soko moja la pamoja na ujenzi wake
umefadhiliwa na
taasisi ya MIVARF kwa kushirikiana na halmshauri ya wilaya ya Karatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni