Eneo la Kitongoji cha Mferejini lililotengwa na Serikali kwa ajili ya kuanzisha kambi kwa ajili ya Wahanga wa Mafuriko .
Wahanga wa Mafuriko wakianza ujenzi wa nyumba za Miti kwa ajili ya kujisitiri katika eneo la Ruvu Mferejini.
Makazi
ya wananchi hawa kwa sasa wanalala nje ,wakiteseka na Baridi,Mbu na
wanyama wakali kama Nyoka hali ambayo inatishia Afya zao.
Hata
hivyo tayari serikali imeanza kufikisha huduma mbalimbali za kijamii
ikiwemo ya Maji kwa ajili ya kunywa pamoja na kupikia.
Mkuu
wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule akiwa ameongozana na Katibu
Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Mhandisi Aisha Amour wakitembelea moja ya
Kaya ya Jamii ya Wafugaji walioanza maisha mapya katika maeneo
yaliyotengwa na Serikali.
Kama
ilivyo ada kwa tamaduni za Mila za jamii ya Maasai kina mama ndio
watendaji wakubwa wa shughuli za Nyumbani kiwemo ujenzi wa Nyumba kama
anavyoonekana Bibi huyu.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
SERIKALI
imetoa siku mbili kwa wananchi waliosalia katika Vijiji vya Ruvu
Mferejini na Ruvu Marwa wilayani Same ,Mkoani Kilimanjaro
vilivyozingirwa na maji kuondoka mara moja na kwamba watakao kaidi
wataondolewa kwa kutumia nguvu na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Zaidi
ya watu wapatao 2000 wamelazimika kuyahama makazi yao baada ya kufikwa
mafuriko kutokana na mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha huku
eneo lililoathirika zaidi na mvua hizo ni ukanda wa tambarare wa wilaya
ya Same unaopakana na Bwawa la Nyumba ya Mungu.
Licha
ya Idadi hiyo ya watu kuyahama makazi yao lakini bado wapo waliokaidi
kuondokana na hapa Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Same ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Wilaya hiyo ,Rosemerry Senyamule
,ikatoa agizo.
Serikali
imetenga maeneo kando ya milima iliyopo katika kitongoji cha Mferejini
kwa ajili ya Kambi za Muda kwa watu waliokosa Makazi ,Clouds Habari
imefika katika Kambi hizo na kujionea maisha mapya ya wahanga wa
mafuriko huku misaada ya kibinadamu ikihitajika zaidi .
Licha
ya kukosekana kwa baadhi ya huduma katika eneo hili bado wananchi hawa
wanahitaji msaada wa hali na mali ili angalau kuweza kunusuru Maisha yao
kutokana na Baridi kali ,Mbu na hata wanyama wakali wakiwemo Nyoka.
Katibu
tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi ,Aisha Amour ni miongoni mwa baadhi
ya viongozi waliowatembelea wahanga wa mafuriko kwa ajili ya kutoa pole
.
Mafuriko
katika vijiji hivi yanatajwa kuwa hutokea kila baada ya Miaka 10 na
kwamba mara ya mwisho yalitokea mwaka 2008 huku chanzo kikitajwa kuwa ni
kujaa kwa Bwawa la Nyumba ya Mungu ambapo ujazo ulifikia Mita za ujazo
689.88 ambazo kwa sasa zimeanza kupungua hadi kufikia mita za ujazo
689.80 baada ya maji kuanza kuelekea kwenye maeneo ya makazi kwa kupitia
mto Pangani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni