JAFO AAGIZA KUREKEBISHWA MAZINGIRA YA SOKO LA FERI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo  akikagua soko la samaki Feri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo  akiagana na viongozi mara baada ya kukagua soko la samaki Feri.
……………………………………………………..
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo ameiagiza Bodi ya Soko la samaki Feri pamoja na Manispaa ya Ilala kufanya marekebisho ya soko hilo ndani ya siku 45 ili wafanya biashara waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki na salama.


Jafo ametoa maagizo hayo alipotembelea sokoni hapo leo hii na kukutana na baadhi ya mambo hayapo sawa ikiwemo ubovu wa mifumo ya maji taka, uchakavu wa meza za kuzuia samaki, kukosekana kwa mapanda ya kuuzia samaki kwa wavuvi wadogo, na kusitishwa kwa huduma ya mamalishe na babalishe kwa upande wa wavuvi wadogo.


Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo ameagiza kufanyike marekebisho ndani ya siku hizo 45 sambamba na kuwarejesha wafanyabiasha wa chakula katika eneo la wavuvi wadogo ili nao wajipatie mahitaji yao ya kimaisha kama ilivyokuwa hapo awali.


Aidha, Waziri Jafo amewataka wavuvi na wafanya biashara wa soko la feri kuzingatia sheria kwa kutoruhusu watu wanaojishughulisha na shughuli haramu za uuzaji wa madawa ya kulevya kujiingiza katika maeneo yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni