Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Prosper Kiwigize akifungua mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Mtandao huo, Marko Mipawa, Afisa Miradi kwenye Kitengo cha Mawasiliano na Habari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO), Rose Mwalongo (wa pili kushoto), pamoja na Mkurugenzi wa MISA-TAN, Gasirigwa Sengiyumva (kushoto).
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Prosper Kiwigize akionyesha cheti cha usajili wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) unaohusisha Tanzania bara na Visiwani wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Afisa Miradi kwenye Kitengo cha Mawasiliano na Habari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO), Rose Mwalongo akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege akitoa salamu kwa wajumbe ambapo ameahidi kuendeleza ushirikiano na TADIO wakati wa mkutano mkuu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa akisoma ripoti ya mapato na matumizi kwa kipindi cha Januari 2017 mpaka Mei 2018 pamoja na taarifa ya bodi ya TADIO ya utekelezaji kwa kipindi cha Julai 28, 2017 mpaka Mei 3, 2018 wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa MISA-TAN, Gasirigwa Sengiyumva akizungumza na wajumbe wakati wa mkutano mkuu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Mjumbe wa TADIO kutoka Kahama FM, Maria Lembeli akichangia maoni wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Mjumbe wa TADIO kutoka redio Orkonerei FM, Baraka Ole Maika akiuliza swali na kuchangia maoni wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Sekretarieti ya TADIO kutoka kushoto ni Maratibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Samson Kamalamo, Afisa Tehama wa mtandao huo, Fatuma Rashidi, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege pamoja na Afisa Utawala na Mhasibu wa mtandao huo, Bakari Sungura wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Pichani juu na chini ni Wajumbe wa Bodi ya Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) walioshiriki mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Wajumbe wa Bodi ya Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) katika picha ya pamoja baada kumaliza mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Na Mwandishi wetu,
SERIKALI imeombwa ifikirie kutoa ruzuku kwa radio za jamii kupitia Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) ili waweze kuandika habari ya mambo yanayojiri vijijini badala ya kutegemea habari za matukio.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa TADIO, Prosper Kwigizewakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliosajiliwa mwaka jana na msajili wa mashirika ya kiraia na kuhudumu kwa takribani radio zote za jamii nchini.
Alisema kwa sasa wanajivunia kuhudumia watu takaribani milioni 35 lakini wana shida kubwa ya kuweza kuandika habari za maendeleo vijijini kutokana na tatizo la fedha.
Alisema wao kama radio za jamii zinasikilizwa vyema katika maeneo yao kwa kuwa wanaandika habari za wananchi wa huko katika ngazi ya mtaa na kijiji na kama mabadiliko yanatakiwa kufanywa katika nchi wao ndio wanaoweza kuwa chachu.
Hata hivyo alisema pamoja na kuwa karibu na wananchi wanalazimika kuandika zaidi habari za matukio kutokana na kukosa fedha za kutuma waandishi vijijini kupiga kambi kwa ajili ya habari za uchunguzi ambazo zitaibua masuala mbalimbali.
Alisema pamoja na kupata msaada mkubwa kutoka mataifa ya Sweden na Uswis kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO), msaada wao hautoshi na hivyo kuitaka serikali na wadau wa ndani kama Mifuko ya Hifadhi kuwezesha radio hizo kusimama zenyewe kimapato na kitendaji.
Alisema kuna masuala mengi ya vijijini katika mikoa ya pembeni ambayo radio hizo zikiwezesha zinaweza kusaidia kujulisha taasisi nyingine nini kinajiri na nini kinastahili kufanywa.
Alisema katika kuelekea uchumi wa viwanda taifa linaweza kunufaika sana na kusimama kwa radio hizo ambazo ndizo zinazoweza kutumika kufika kijijini badala ya radio za kitaifa ambazo hazina muda wa kutangaza masuala ya maendeleo ya vijijini.
Pamoja na kuwashukuru wadau mbalimbali waowezesha mtandao huo kuendelea kuwa na nguvu zaidi na kujitanua kufikia wanachama 35 toka walioasisi 27 alitaka watu wengi zaidi wanaojikita na habari za vijijini kujiunga na umoja huo ili kuwa na sauti moja.
Naye Afisa Miradi kwenye Kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco, Rose Mwalongo katika salamu zake kwenye mkutano huo aliwataka wanachama kushirikiana vyema na uongozi na bodi ili kuimarisha umoja wao.
Alisema wasipokuwa na ushirikiano na kuanzisha majungu wafadhili wataona shida kuendelea kuwa nao na hivyo kukwamisha malengo yao ya kipindi kirefu.
Aliwakumbusha kwamba hata viongozi wakuu duniani kama Rais wa Marekani Abraham Lincolin alisema kwamba nyumba yenye nyufa kati haiwezi kusimama na kuwataka kujenga umoja hasa ukizingatia mgogoro uliokuwepo katika taasisi ya awali ya Comneta.
Alisema fedha zinazoletwa katika asasi hiyo zisiwe chanzo cha mafarakano bali kiwe chanzo cha wao kukua zaidi kiutaaluma na kuweza kuwafikia watu wengi na kujenga imani ya wananchi kwao.
Aliwataka waendele kupaza sauti kwa niaba ya zaidi ya robo tatu ya watanzania wanaoishi vijijini na pembezoni mwa nchi wakitegemea kilimo kuboresha maisha.
Aidha katika mkutano huo Mkurugenzi wa MISA-TAN, Gasirigwa Sengiyumva aliwataka wananchama wa TADIO kuendeleza uhusiano uliokuwapo tangu awali na pia kufikiria siku ya habari kutoa tuzo ya radio bora kwa mwaka.
Alisema wao kama watetezi na wazengezi wataendelea kusaidiana na TADIO katika kazi zao ikiwa ni pamoja na kuwasimamia katika mashauri mbalimbali ya uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kupata habari.
Alisema kwa wao kuwa wanachama watakuwa na faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wafanyakazi wao kwa kuwaonesha njia za kupita katika mafunzo na utendaji kazi.
MISA-TAN ni sehemu ya Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika yenye makao makuu yake Windhoek Namibia na wajibu wake mkubwa ni kuangalia uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari na haki ya kupata habari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni