Sehemu ya wadau wakimsubiri spika wa bunge hayupo picha kuja kuzindua maonyesho hayo ya wadau wa sekta ya madini nchi kwenye viwanja vya bunge jijini dodoma leo picha zote na Mahmoud Ahmad Dodoma
Na Mahmoud Ahmad
Dodoma
Spika wa bunge Job Ndugai ameitaka sekta ya madini hapa
nchini kuhakikisha wanayapa thamani madini mbali mbali yanayopatikana hapa
nchini kwa kuyachakata kabla hayajaingia sokoni lengo likiwa ni kuongeza pato
na thamani.
Ndugai ameitoa Kauli hiyo wakati hotuba yake kwenye
maonyesho ya wadau wa sekta ya madini kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma,
na kuitaka kuhakuikisha wanaongeza thamani madini kabla ya kuingizwa sokoni
ndani na nje ya nchi.
Ndugai Ametanaibaisha kuwa uchenjuaji wa madini uende
sambamba na kuyapa thamani madini yetu lengo likiwa ni kuongeza ubora wake
utakaosaidia kuboresha madini yetu na kuacha kupeleka madini ghafi nje ya nchi.
Ameitaka wizara hiyo na wadau wake kuhamasisha uwekezaji katika
shughuli za utafutaji,uchimbaji na uongezaji thamani madini nchini ili kuongeza
mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa.
“ hapa mnatakiwa kuangalia suala zima la kuyapa madini yetu thamani
na kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata dhana bora na kujua maeneo bora ya
uzalishaji wa madini hili litasaidia ukuaji wa sekta hili na kuweza kuchangia
mapato ya Taifa”
Awali akimkaribisha spika ndugai Waziri wa Madini Anjela
Kairuki amesema kuwa wizara hiyo imejipanga kuhakikisha sekta ya madini
inanufaisha taifa na kuongeza kuchangia katika ukuaji wa pato la taifa sanjari na
kuongeza nafasi kwa vijana kujiajiri.
Hatua nyingine baada ya kufuguliwa kwa maonyesho hayo kwenye
viwanja vya bunge waziri huyo akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo bunge
ameliomba bunge kumuidhinishia kiasi cha tsh. Billion 58.908 kwa ajili ya matumizi
ya kawaida na maendeleo kwa mwaka 2018-19
Aidha amesema kuwa sekta ya madini ni muhimu katika kukuza
uchumi na kutoa mchango mkubwa kwa taifa na dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka
2025 ambapo mpango wa kuhakikisha sekta inanufaisha nchi hivyo wamejipanga
kuimarisha ulinzi na kudhibiti utoroshwaji wa madini.
Nae Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Dustan Kitandula
Amesema kuwa sekta hiyo itaendelea kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za
utafutaji,uchimbaji na uongezaji thamani madini nchini ili kuongeza mchango wa
sekta hiyo katika pato la taifa.
Mwisho…………………..
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni