Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman
Jafo akiongea na wamachinga wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa
Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania- SHIUMA leo uliofanyika katika
ukumbi wa shule ya Sekondari Dodoma, Jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman
Jafo akiongea na wamachinga wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa
Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania- SHIUMA leo uliofanyika katika
ukumbi wa shule ya Sekondari Dodoma, Jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman
Jafo akiongea na baadhi ya viongozi wa shirika la umoja wa wamachinga
Tanzania – SHIUMA leo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu uliofanyika
katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma, Jijini Dodoma.
Na Mahmoud Ahmad,
Wakuu
wa Wilaya wameagizwa kuzisimamia halmashauri nchini kuhakikisha kuwa
zinatenga maeneo maalum ya kufanyia biashara ndogondogo (machinga) ili
waweze kuendesha shughuli zao bila kuvunja sheria, kanuni na taratibu
zilizowekwa na serikali.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhe. Selemeni Jafo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa
Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania – SHIUMA uliofanyika leo katika
ukumbi wa shule ya Sekondari ya Dodoma, Jijini Dodoma.
Alisema
Wakuu wa Wilaya wana wajibu wa kuratibu na kuhakikisha kuwa maeneo ya
kufanyia bishara kwa wamachinga yanatengwa na Halmashauri ili
kuwawezesha kufanya kazi zao kwa utaratibu bila kuvunja sheria za nchi.
Aliongeza
kuwa wamachinga ni watu muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania kwa
kuwa wafanyabiashara wadogo ndio wanaoleta muunganiko wa watu katika
kada mbalimbali wakiwemo wasomi wenye shahada, astashaada, kidato cha
sita, kidato cha nne, darasa la saba na wasiosoma kabisa wote huunganika
na kufanyabiashara kama wamachinga.
Alisema
kati ya watanzania milioni 50, walioajiriwa serikalini na sekta ya umma
ni 520,000, hivyo kundi kubwa ni la watu ambao ama wamejiajiri au
wameajiriwa katika sekta binafsi.
“Lakini
kundi kubwa ni wale watu wanaojishughulisha kwa kutafuta riziki zao
wenyewe ambao watu hao ndio unapata asilimia kubwa wako katika kundi la
wamachinga,” alisema Mhe.Jafo na kuongeza:
“Utakuta
mtu anafanyabishara katika mazingira magumu ambayo yanamfanya kila
wakati kutokuwa na uhakika wa kupata kipato cha siku jambo ambalo
linaathiri familia yake na kuongeza umaskini nchini, hivyo ifike mahali
wakuu wa Wilaya waweke mikakati ya kuhakikisha wamachinga wote
wanapatiwa maeneo bora ya kufanyia biashara ili wajikwamue kiuchumi,
“alisisitiza Waziri
Aliongeza
kuwa Serikali imejiwekea mkakati wa kutengeneza masoko mazuri na ya
kisasa kwa kuweza kuweka mazingira bora kwa wamachinga kufanya biashara
zao katika maeneo stahiki.
Aidha
Waziri Jafo alisema kuwa Viongozi wanatakiwa kutafakari na kutatua kero
ya maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara wamachinga, hivyo serikali
imeanza mpango mkakati wa ujenzi wa masoko mazuri ya kisasa ili
wafanyabishara waweze kufanya kazi katika mazingira bora na tayari
imetenga shilingi bilioni 149 kwa ajili ya ujenzi wa masoko, stendi za
kisasa na viwanda vidogo.
“Nimetoa
maagizo soko lolote litakalojengwa lazima mustakabali wa
wafanyabiashara wadogo wadogo waliokuwepo awali umejulikana na kuwa
kipaumbele kwa kupatiwa maeneo ya kufanyia biashara pindi majengo hayo
yanapokamilika hivyo viongozi wa halmashauri wahakikishe wanatoa
kipaumbele kwa wafanyabiashara waliokuwepo awali,” alisema Jafo.
Alisema
kuwa Serikali imekuwa ikiwekeza katika miradi mikubwa ikidhani
inawagusa maskini lakini kwa bahati mbaya masoko mengi yanayojengwa
wanaonufaika ni watu wenye fedha na kuwaacha wafanyabiashara waliokuwepo
awali kabla soko kujengwa.
Hivyo
nawaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wananchi masikini wanapatiwa
nafasi katika masoko hayo ili waweze kujiongezea kipato.Amewaagiza
wakurugenzi wa Halmashauri wote nchini kuhakikisha kuwa kabla soko
halijaanza kujengwa kufanyike tathmini ya wafanyabishara waliokuwepo
awali ili wawe kipaumbele pale soko linapokamilika.
Wakati
huohuo Mhe. Jafo amewataka wamachinga nchini kuhakikisha wanajiunga na
bima iliyoboreshwa ili iwawezeshe kuwasaidia pale wanapokuwa wagonjwa
wao na familia zao kwa kuwa afya ni uhai.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni