OFISA UTUMISHI TRA AIELEZEA MAHAKAMA KUWA MALI ALIZOJAZA MSHTAKIWA NI ZA FAMILIA NA ZINA UMILIKI WA NUSU KWA NUSU


Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

OFISA Utumishi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Evans Emil (53) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mali ambazo alijaza mshtakiwa Jenifa Mushi kwenye fomu za rasirimali na madeni ni za familia ambapo amedai mali nyingi zilizojazwa kwenye fomu hizo, zina umiliki wa nusu kwa nusu mshtakiwa na mkewe na watoto wao.

Evans ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka amedai hayo wakati akitoa ushahidi katika kesi inayomkabili, Aisa Msaidizi wa Forodha Wa  (TRA), Jennifer Mushi ya  kukutwa akimiliki magari 19 mali ambayo hailingani na kipato chake,

Akitoa ushahidi wake leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Shaidi huyo alidai, yeye aliajiliwa TRA mwaka 1996 akiwa na majukumu ya kushughulikia ajira, kusimamia nidhamu, maslahi ya wafanyakazi, utawala na majukumu mengine atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

Alidai taratibu moja wapo kwa mtu ambaye atakuwa ameajiriwa na kuthibitishwa pamoja na mambo mengine anatakiwa kujaza fomu ya tamko ya rasilimari na madeni  ambazo anatakiwa kuijaza kila mwaka wa kalenda na isizidi ndani ya miezi mitatu.

Alidai,  fomu hizo ujazwa chini ya sheria ya maadili ya viongozi wa umma na kanuni ya utumishi ya TRA pale mtumishi anapoajiriwa na kuripoti kazini.

Amedai, lengo kubwa la kujaza fomu hiyo ni kujua mali na madeni ya mfanyakazi na kufahamu uadilifu wa mtumishi, kutokana na mazingira ya kazi ya TRA ikiwa ni kudhibiti vitendo vya rushwa na kujilimbikizia mali.

Alidai anamfahamu Jeniffer kama Ofisa Forodha Msaidizi wa TRA  tangu mwaka 2010 ambapo alikuwa akifanya kazi ya kuthaminisha bidhaa zinazoingia na kutoka nje ya nchi.

Alidai mwanzo aliajiriwa TRA kwa mkataba wa miezi mitatu mitatu kuanzia Januari Mosi, 2011 mpaka Machi 2011 baada ya hapo Juni 30 mwaka 2011 aliongezewa mkataba na Julai Mosi mwaka huo huo, alipatiwa mkataba wa kudumu ambapo alijazaa fomu mbalimbali  ikiwamo fomu ya Tamko ya Rasilimali na madeni.

Alidai, mwaka 2016 Mkuu wake wa kazi alimuelekeza kuwa kulikuwa na uchunguzi unaendelea kuhusiana na fomu ya tamko ya rasilimari na madeni ya Jeniffer ambayo  haikuwa sawa na kumtaka awapatie Takukuru na kufanya hivyo.

Alidai katika mkataba wa kidumu ilionyesha anaajiriwa na mshahara wake ulikuwa Sh 800,000 ambapo ungekuwa ukiongezeka hadi milioni 2.

Shahidi Evans aliisoma fomu ya tamko ya rasilimari ya Machi 30/2012 ambayo inaonyesha Jeniffer alieleza kuwa anamiliki Sh. 600,000, zilizopo katika benki na taasisi za fedha Sh 800,000.

Alikuwa na Hisa na gawio la thamani ya Sh 600,000. Pia alikiwa na nyumba kinyerezi  kichangani yenye thamani ya milioni 30  ambayo yeye mshtakiwa alikuwa akimiliki kwa asilimia 50 na mumewe asilimia 50.

Aidha Shamba la heka moja eneo la Mabwepande lenye thamani ya sh. 700,000 umiliki wake yeye asilimia 50 mumewe asilimia 50. Pia Kiwanja heka moja kipo kigamboni chenye thamani ya Sh. Milioni 9 milioni ambapo umiliki wake wake ni asilimia 50 yeye na mume wake 50.
 Mali zingine ni gari aina ya Van,  yenye thamani ya Sh milioni 8 umiliki wake mke asilimia 50 mume asilimia 50. Pia katika upande wa madeni alikuwa na deni la bodi ya mikopo ya vyuo vikuu.

Katika fomu ya tamko ya rasilimali na madeni ya Februari 20/ 2013 Jeniffer alijaza alikuwa na fedha taslimu Sh 800,000 Kiwanja fedha zilizopo katika benki na taasisi za fedha Sh 1,040,000, nyumba kinyerezi yenye thamani ya Sh 35milioni, umilikiwake mke asilimia 50 mume asilimia 50.

Pia alijaza kuwa na kiwanja eneo la Bunju chenye thamani ya Sh milioni 1.7 ambacho mmliki wake ni yeye,  Kiwanja kilichopo Kigamboni chenye thamani ya Sh milioni 9 wamiliki watoto.


Magari  RV 4 lenye thamani ya Sh  milion 8,  RV 4 lenye thamani ya Sh, milioni 13 umiliki wake asilimia 50 mke na asilimia 50 mume. Pia anadeni la bodi ya mikopo ya vyuo vikuu.

Katika fomu ya tamko ya rasilimari na madeni ya Desemba 11/ 2015 inaonyesha Jeniffer anafedha taslimu Sh 550,000, fedha zilizopo benki na katika taasisi za fedha Sh milioni 2.7

Kiwanja Kigamboni cha sh. Milioni 9 umiliki wake wake asilimia 50 mume asilimia 50, magari Toyota la Sh milioni 18 na Toyota ya Sh  milioni 14


Deni  la saccos ya TRA la Sh 6, 168,513 na deni la  mkopo Wa bodi ya mikopo ya vyuo vikuu la Sh 1.5 milioni. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 6 mwaka 2018

Katika kesi hiyo mshtakiwa Jenifer alikutwa akimili magari 19.


yakiwa na thamani ya Sh 197,601,207 Mali ambayo hailingani na kipato chake halali, pia alikutwa akiishi maisha ya kifahari  yenye thamani ya Sh 333,255,556.24 fedha ambayo hailingani na Kipato chake halali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni