Arusha
Taasisi
isiyokua ya kiserikali ya Wanaume inayojulikana kama Men At Work
imeendesha zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kinamama wanaojifungua
na majuruhi wanaonusurika na ajali na kufikishwa katika hospitali ya
mkoa ya Mount Meru .
Mkurugenzi
wa Taasisi hiyo Maxwell Stanslaus amesema kuwa wameamua kuwa wameamua
kuchangia damu kama mchango wanaume kujitoa kwa ajili ya jamii na
kuisaidia jami kwasababu wanaume ni nguzo ya familia,jamii na taifa kwa
ujumla.
Max aliwataka wanaume wote nchini kuwajibika na kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii .
“Kwa
sasa tumeamua kushirikiana na kitengo cha damu salama kuchangia damu
ili kupunguza changamoto ya upungufu wa damu katika benki ya damu “
Alisema Max
Max
alisema kuwa taasisi hiyo ina kazi kuwa ya kuwahasisha wanaume kuwa
wawajibikaji na kushiriki katika nafasi za malezi familia na jamii ili
kujenga familia imara na hatimaye taifa imara.
Kwa
upande wake Mwanachama wa Men At Work Rodgers Nelson alisema kuwa
anajisikia faraja kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya kinamama
wajawazito ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
Naye
Shemeji Melayeki alieleza kuwa ni mara yake ya kwanza kutoa damu hivyo
amewatoa hofu wananchi kutokua waoga wa kuchangia damu kwani zoezi hilo
linafanyika kwa umakini na halina madhara yoyote.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Maxwell Stanslaus akizungumza na
Mkazi wa Arusha katika zoezi la uchangiaji wa damu lililoensheshwa ma
taasisi yake.Picha na Ferdinand Shayo
Mwanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work akichangia damu
Mwanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Rodgers akichangia damu katika viwanja vya Sheikjh Amri Abeid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni