Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  John Pombe Magufuli kwa ujenzi wa vituo  vya afya 208 vilivyojengwa na Seriakli kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya nchini.
Wameyasema
 hayo mbele ya Kamati ya ufuatiliaji wa ukarabati wa vituo vya afya 
nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 
iliyofika katika kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri 
ya Wilaya ya Kongwa kukagua  maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kilichopatiwa shilingi bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi huo.
Wananchi hao wamesema Serikali imetambua shida za wananchi wa hali chini na kuona umuhimu wa kujenga vituo vya afya nchini  kwa lengo la kupunguza kero za utoaaji wa huduma bora kwa jamii maskini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo cha afya Mlali,kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw. Abbas Mkomwa  ameishukuru
 Serikali kwa kutoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo 
hicho ambacho kimeweza kujenga , Nyumba ya Mtumishi, Wodi ya wazazi, 
Maabara,  Jengo la upasuaji na jengo la kuhifadhia maiti.
Amesema
 huduma kama hizi zimekuwa zikifanyika lakini kwa sasa jamii imeweza 
kushirikishwa katika kila hatua za awali za ujenzi wa vituo vya afya 
hivyo kuweka uwazi kwa jamii na kuona kuwa nao wanawajibu wa kushiriki 
katika ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya nchini.
“Kwa
 mara ya kwanza Serikali imeweza kushirikisha wananchi katika shughuli 
za maendeleo, hii inaonyesha jinsi serikali ya awamu ya tano 
inavyojdhamini mchango wa wananchi katika kuleta maendeleo“ AmesemaBw. 
Mkomwa.
Naye
 Richard Mgulumu Diwani wa kata ya Mlali ameipongeza Serikali kwa ujenzi
 wa vituo vya afya nchini, hasa kituo cha afya cha Mlali ambapo anasema 
kuwa awali kituo hicho kilikuwa na wodi chache ambazo zilikuwa hazitoshi
 kuhudumia wananchi lakini kwa sasa zimeongezeka jambo ambalo litasaidia
 kuondoa kero za utoaji wa Huduma za afya katika Halamashauri hiyo.
Amesema
 kuwa Kituo hicho cha afya kimekuwa kikipata wagonjwa wengi kutoka 
Wilaya ya Kiteto, Wialaya ya Mpwapwa na Malali hivyo kwa ujenzi huo 
kutasaidia kuwahudumia wananchi maskini ambao wamekuwa wakitembea umbali
 mrefu kutafuta huduma bora za afya.
Naye
 Mganga Mkuu Hospitali ya Jiji la Dodoma Dkt. James Kiologwe ameipongeza
 Kamati ya Ujenzi ya kituo cha afya cha Mlali kwa usimamizi mzuri wa 
ujenzi wa kituo hicho na kuonyesha uzalendo wa kusaidia jamii.
Aidha
 timu ya Ufuatiliaji wa ujenzi wa vituo vya afya Jijini Dodoma imekagua 
maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya vya Mlali, Chamwino, Hombolo na 
Makole.
Capt
- Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt.James Kiologwe akifafanua jambo kwa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Mlali leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya afya kuona maendeleo ya ujenzi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma.
 - Timu ya Dodoma wakikagua miundombinu ya Kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma leo wakati wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho leo.
 
Majengo
 ya Upasuaji na wodi ya Wazazi iliyojengwa katika kituo cha afya cha 
Mlali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt.James Kiologwe  akifafanua
 jambo kwa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Mlali leo wakati wa ziara ya 
ukaguzi wa vituo vya afya kuona maendeleo ya ujenzi, katika Halmashauri 
ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni