Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
JESHI la polisi
mkoani Pwani, lina mshikilia Mariam Joakim mwenye miaka (52),kwa kosa la
kudaiwa kusababisha kuteketeza kwa moto ofisi ya mbunge wa jimbo la
Chalinze ,Bagamoyo Ridhiwani Kikwete .
Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna ,alithibitisha juu ya taarifa hiyo .
Alisema tukio hilo
limetokea June 17 majira ya saa ya 18:00 ambapo jeshi hilo lilipokea
taarifa kutoka kwa raia mwema kwa njia ya simu ,kuwa jengo la ofisi ya
mbunge huyo inawaka moto.
“Katika tukio hilo ofisi yote imeteketea kwa moto na kuokolewa vitu vichache” alisema kamanda Shanna.
Kwa mujibu wa kamanda
hiyo chanzo cha moto kimesababishwa na mtuhumiwa Mariam,ambae anaeleza
aliwasha moto eneo la nyuma ya jengo hilo kwa lengo la kuchoma majani
kisha moto ukamzidi na kushika majani na mabomba yaliyokuwa kando ya
jengo hilo.
Anasema hatimaye moto uliunguza jengo lote.
Thamani ya uharibifu na vitu vilivyoungua haijajulikana na mtuhumiwa yupo mbaroni kwa mahojiano zaidi.
Nae mbunge wa jimbo hilo ,Ridhiwani aliwashukuru wote walioguswa na mtihani alioupata.
“Mtihani unapita,
asubuhi saa tano june 19 ,mungu akipenda nitakwenda angalia athari ya
moto, na kueleza kwa ujumla tukio hili na hasara iliyotokea” alielezea
Ridhiwani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni